CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Monday, September 23, 2013

JIFUNZE KUANDAA WALI NA KUKU WA KUKAANGA PAMOJA NA MBOGA MAJANI NDAI YA DAKIKA 15

 
NDUGU ZANGU MNAOISHI PEKE YENU BILA FAMILIA KUBWA AU UNAISHI UGHAIBUNI KUTOKANA NA MAJUKUMU MENGI NA KUANA NA MUDA MCHACHE WA KUWEZA ANDAA CHAKULA KIZURI KWA NJIA HII UNAWEZA KUANDAA CHAKULA KIZURI KWA MUDA MFUPI KWA KUTUMIA MBOGA MAJANI ILIZOANDALIWA NA KUGANDISHWA KATIKA JOKOFU.
 
MAHITAJI
 
2 pc vifua vya kuku (Kata kata vipande vidogo)
60 gram soy sauce kwajili ya marinating
3 pc kwajili ya scrambled eggs ( yai la kuvuruga)
120 gram carrots mchanganyiko na njegere za kwenye mfuko
120 gram kitunguu cha kwenye mfuko au 2pc fresh kata kata
60 gram siagi iliyoyeyushwa
1 kitunguu swaumu kisage au 1 kijiko kidogo cha chai garlic powder
Nusu kilo ya wali uliokwisha pikwa ukaiva safi.
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
 
 
Huu ni mchanganyiko wa mboga mboga kama unaovyoona katika picha kuna vitunguu mfuko mmoja na njegere na karoti katika mfuko mwingine.
 

 
Mwagia soy sauce katika bakuli safi lenye vipande vya kuku.

 
Kisha weka katika moto kikaango kikubwa, kabla ya kuweka kuku pia unatakiwa uweke mafuta kiasi yapate moto kasha mwagia kuku hao pamoja na mchanganyiko wake wa soya sauce kumbuka hutakiwi kuweka chumvi kwani soya sauce tayari inaladha ya chumvi.

 
Endelea kukaanga pole pole na hakikisha nyama zinageuka zachini kuja juu ili zote ziweze kuiva ila zisikauke, hakikisha ule mchanganyko wa soya sauce upungue kiasi nao usikaukie. kisha mwagia kitunguu na njegere pamoja na karoti na uendelee kukaanga na kugeuza. Pika mpaka mboga mbga zinukie harufu safi na kua laini.

 
Kisha weka wali wako uliokwisha iva pamoja na scrambled eggs pamoja na siagi na kitunguu swaumu hakikisha unakoroga vizuri na mchanganyiko wako uchanganyike vizuri.

 
Baada ya kuchanganya mchanganyiko wako safi kabisa utapata muonekano huu lakini naimani ladha bado itakua haijakaa safi, Kisha ongezea kijiko kimoja kidogo cha chai soy sauce kuweka ladha sawa kasha wewe na rafiki yako au family enjoy!
 Tuesday, September 17, 2013

JIFUNZE NJIA HII YA KUTENGENEZA TIKITI MAJI KWA MUUNDO KAMA KEKI

 
NI RAHISI SANA ENDAPO UTAFATA MAELEZO VIZURI KWANI HAIITAJI UTAALAMU SANA NA INAMUONEKANO NADHIFU SANA
 
MAHITAJI

1 lita ya fresh cream
1 pc tikiti maji kubwa
250 gram ya matunda aina ya blue berry(unaweza tumia zabibu za bluu au nyekundu mbichi)
250 gram ya zabibu mbichi za kijani
250 gram pia unaweza tumia korosho au karanga za kuoka
250 gram pia unaweza tumia machicha makavu ya Nazi
 
 JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
 

1. Kama muonekano ulivyo katika picha kwanza kata pande zote mbili za tikiti maji kwenye kitacho chini na juu.
 
2. Menya kwa mtindo wa duara pole pole hata ganda likikatika hamna neon  cha msingi tikiti liwe safi na mviringo.
 
3. chukua cream fresh piga piga kwa kutumia mashine au mchapo mpaka ie nzito kabisa.
 
4. Chukua crema fresh uliyokwisha piga pakaza kuzunguka sehemu zote za tikiti maji lako hakikisha hamna sehemu hujapaka cream ya kutosha.
 
5. Mwagia karanga au korosho au machicha ya Nazi makavu kwa upande wa pembeni.
 
6. Kisha juu yake panga matunda hayo inategemea msimu na unamatunda gani unaweza weka aina yeyote ile ya matunda kwajuu ilimradi upate muonekano wa rangi tofauti toka katika aina ya matunda uliyonayo au uliyoyapenda.

HII NI NJIA BORA SANA YA KUWASHAWISHI WALE WOTE WASIOPENDA KULA MATUNDA IWE MTU MZIMA AU MTOTO WAANDALIE FAMILIA WAFURAHIE.Monday, September 9, 2013

JIFUNZE NJIA MBADALA YA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME NDANI YA DAKIKA 10 KWA CHAKULA

 
KWA KULA SAMAKI HUYU MWENYE GAMBA GUMU AINA YA OYSTER UNAWEUWEZEKANO ASILIMIA 99 KUONGEZA NGUVU ZAKO ZA KIUME NDANI YA DAKIKA 10 NA UTAKUA NA NGUVU ZA KAWAIDA TU KAMA BINADAMU WENGINE BILA MADHARA KWA MWILI WAKO AU MWILI WA MWENZI WAKO BADALA YA KUTUMIA DAWA ZENYE MADHARA NA MWILI WAKO NA KWA MWENZI WAKO
 
FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Huna nguvu za kutosha kufanya tendo la ndoa? Unakosa kabisa hamu ya kufanya tendo la ndoa au mara kwa mara inakutokea? "Basi tatizo lako ni 'low T' au low testosterone," na ni tatizo kubwa kwa wanaume wengi.
Testosterone ni hormone inayozalishwa katika vifuko vya mbegu za uzazi wa mwanaume, inasaidia sana sana katika kuhamasisha uwezo na msukumo wa tendo la ndoa. Inasaidia sana pia kumaintain strong bones, muscle mass and strength,
Testosterone inaanza kujitengeneza na kuongezeka katika mwili wa mwaume wakati wa adolescence na unapopevuka, na hupoteza ubora au kushuka kiwango hasa pale unapofikia umri wa miaka 30 kwa kiwango cha asilimia 1 kila mwaka.  Kukosa ubora au kushuka kwa kiwango kunasababishwa na stressau mzongo wa mawazo ya maisha, mlo usio kamili , obesity na sababu nyingine. Inaposhuka ndio balaa inapoanza nawe kukosa hamu au kupungukiwa nguvu za tendo la ndoa mfano uume kutosimama imara na kukosa hamu pengine hata kufanya tendo chini ya kiwango kabisa na kusababisha kutomridhisha mwezi wako.
Oysters wana Protein, magnesium na madini ya zinc  kwa wingi sana kuliko chakula chochote duniani, ambayo zinc hiyo inasaidia sana kuongeza  testosterone, kukuimarisha na kukuza misuli katika mwili, ukakamavu wa hisia za kimwili na kuzalisha manii ya kutosha (sperm). Chakula kingine chenye zinc nyingi kinachoweza kukusaidia ni maini ya kuku na mbegu za maboga.
 
 HUYU NDIO OYSTER MWENYEWE AKIWA MZIMA
 
 PICHA HII NI BAADA YA KUMFUNUAHIZI NI HATUA JINSI YA KUMFUNUA OYSTER MWENYEWE 
 
 
UNAONA NYAMA TAMU KABISA BAADA YA KUMFUNUA AKIWA BADO MZIMA NA MBICHI


 
KAMA UNAONA KINYAA BASI MWAGIA CHUMVI NA LIMAO KISHA MLE TARATIBU

 
 PIA UNAWEZA MMWAGIA BALSAMIC VINEGAR AU SIKI KUONGEZA LADHA


VIPANDE VIWILI AU VITATU VINATOSHA KABISA KWA DOZI UNASHAURIWA KULA MARA MOJA KWA WIKI, KAMA MBICHI INAKUSHINDA UNAWEZA KULA WALE WA KWENYE MAKOPO, AU WA KUCHEMSHWA LAKINI USILE WA BBQ AU WA KUKAANGA KABISA UKIMALIZA KULA TU BAADA YA DAKIKA 10 MAJIBU UTAYAONA.

TEMBELEA www.facebook.com/ActiveChef click like ukurasa upate habari nyingi za mapishi