CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Sunday, April 15, 2012

JIFUNZE KUPIKA WALI WA SAUSAGE NA MBOGA MAJANI MCHANGANYIKO


JIFUNZE KUPIKA MBOGA MAJANI NA MCHANGAKO WA WALI NA SAUSAGE
MAHITAJI

3 vipande vya sausage
1 fungu la majani ya vitunguu
1 kitunguu kikubwa
100 gram njegere
500 gram chele basmati
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
JINSI YA KUANDAA FATIKLIA PICHA NA MAELEZO

Muda wa mapishi dakika 45
Muda wa maandalizii dakika 15

 

Huu ndio muonekano wa majani machanga ya vitunguu


Kaanga vitunguu maji katika kikaango kwa kuweka mafuta ya kupikia kiasi


Kisha ongezea majani mabichi ya vitunguu kama inavyoonekana katika picha


Baada ya kukaanga kwa dakika mbili vitunguu pamoja na majani vitoe tu harufu na sio kuungua kubadilika rangi kisha weka mchele na endelea kukaanga


Kaanga mchele kwa dakika 3 mpaka 4 kisha weka maji ya wastani yazidi mchele wako kiasi na uendelee kukoroga ili maji yachanganyike na mchele wako


Kisha funikia na weka moto wa wastani ili wali wako uive taratibu


Kisha chukua sausage zako na kata kata vipande vidogo


Huu ndio muonekano wa vipande vya sausage baada ya kukata


Kisha tupia juu ya wali wako njegere zilizochemshwa pamoja na vipande vyoote vya sausage


Kumbuka kuendelea kukoroga ili kila kitu kichanganyike, pia kama mpenzi wa blue band au samli unaweza weka kiasi ili kuongeza ladha na harufu safiu sana katika wali wako


Safi sana hapa kila kitu kimechanganyika na ninaimani baada ya dakika 45 wakli wako utakua umiva kama haujaiva basi ongezea maji kidogo na endelea kupika katika moto mdogo


Ukimaliza pakua na mpatie mlaji chakula hiki kikiwa chamotowaandalie famili au hotelini kila atakae kula atafurahia sana

Sunday, April 1, 2012

JIFUNZE JINSI YA KUPIKA PILAU YA MBOGA MAJANI


KAA TAYARI KABISA KWA KUJIFUNZA KUPIKA PIALU HII YA MBOGA MAJANI

MAHITAJI

250 gram mchele wa basmati
1 kijiko binzali nyembamba (cumin seeds)
1/2 kijiko kidogo cha chai garam masala
1/2kijiko kidogo cha chai coriander powder
1/4 kijiko kidogo cha chai turmeric powder
60 gram njegere za kuchemshwa
1 kitunguu maji chop chop
3 nyanya za kuiva nazo chop chop
1 kijiko kidogo cha chai tangawizi ya kusagwa
1kijiko kidogo cha chai kitunguu swaumu cha kusagwa
2 pili pili mbuzi, kisha kata vipande vidogo vidogo
60 gram korosho au karanga za kukaanga (sio lazima)
1 kijiko kidogo cha chai siagi au mafuta ya samli kwa ladhamajani ya giligilani na majani ya mint kwa kupambia na kuongeza ladha


JINSI YA KUPIKA FATILIA PICHA NA MAFUNZO HAPO CHINI


Muda wa maandalizi : Dakika 15
Muda wa mapishi : Dakika 30
Idadi ya walaji : Watu 2

 

Kwenye kikaango weka kijiko kimoja cha mafuta ya kupikia kama ni samli au siagi, kisha graham masala, unga wa manjano, binzali nyembamba na unga wa corienda kaanga kidogo kisha weka kitunguu swaumu, kitunguu maji, tangawizi, pilipili mbuzi na nyanya zote ziwe chop chop vipande vidogo kama inavyoonekana kweny picha. Kisha weka chumvi, karafuu na pili pili manga endelea kukaanga.UKisha pata harufu ya kunukia saafi imeenea jiko zima hahahahaaaa !! na mboga zako ziwe zimeanza kuiva na hazijaregea basi anza kumimina mchele kidogo.Endelea kukaanga wali wako na ukiuchanganya uchanganyike vizuri kabisa na mboga kwa dakika 2 au 3inategemea na moto wa jiko lako au ubora wa sufuria yako.Kisha weka gram 600 za maji ni sawa na nusu lita na 100 gram za maji kisha koroga na funika na mfuniko acha iive kwa dakika 10 kwa moto wa wastani.Baada ya dakika 10 itakua imekaribia kabisa kuiva, kisha weka njegere za kuiva na koroga kidogo ichanganyike kisha pika kwa dakika 2 tena.


Baada ya pilau yako kuiva basi juu yake rushia majani ya mint au giligilani kuongeza uzuri wa rangi, ladha na harufu safi sana katika pilau yako.


Mwisho kabisa pia ukiwa mpenzi wa siagi mwagia kwajuu kiasi au unaweza mwagia samli hii nikuongeza harufu nzuri na ladha zaidi.Usisahau kwajuu kabisa mwagia karanga au korosho za kukaangwa.  Kumbuka kuaandaa mchuzi mzito kabisa pembeni kwajili ya kulia chakula chako. Kwamapishi haya haya unaweza pika ikawa pilau ya nyama ya kuku, mbuzi au ng'ombe kumbuka kuikata kata nyama na unaiweka mwanzo kabisa wakati unakaanga viungo itaiava sambamba na wali wako na itapendeza sana.