CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Sunday, February 28, 2010

MAULIDI NJEMA


WAPENZI WOTE WA BLOG HII YA CHAKULA SAFI NA SALAMA NAWATAKIA WEEKEND NJEMA NA MAPUMZIKO MEMA YA SIKUKU YA MAULIDI BAADAE KIDOGO RECIPE MPYA NYINGI TU ZINAKUJA USIKOSE

Saturday, February 27, 2010

KEKI YA MACHUNGWA NA ZABIBU KAVU

KUNA MPENZI WA MAPISHI AMEULIZA JE UKITUMIA SELF RAISING FLOUR KUNAHAJA YA KUTUMIA BAKING POWDER? UKITUMIA SELF RAISING FLOUR HUNA HAJA YA KUWEKA BAKING POWDER TENA

 
KEKI HII NI TAMU SANA NA UNAWEZA KUIPIKA KATIKA KILA UMBO NA UKAFURAHIA NA FAMILIA AU HOTELINI WATEJA WAKO WAKAFURAHI SANA


MAHITAJI

• 1 kilo ya unga wa ngano

• 2 kijiko kidogo cha chai baking powder

• 2 Kijiko kidogo cha chai mdalasini ya unga (cinamon powder)

• 1 kijiko kidogo cha chai kungu manga ya unga (Nutmeg)

• 240 gram siagi (butter)

• 480 gram sukari

• 2 Mayai

• 300gram korosho iliyokaangwa ukaikata kata vipande (chopped Cashewnuts)

• 480gram zabibu kavu (raisins)

• 200 gram Maji ya machungwa


JINSI YA KUANDAA NA KUPIKA

Washa oven yako katika moto wa 325 degree F au 165 degree C paka siagi chombo chako unachotumia kuokea keki kisha weka pembeni.

Changanya unga wa ngao, baking powder, unga wa mdalasini, na unga wa kungu manga kisha weka pembeni.

Chukua bakuli nyingine chukua sukari na siagi kisha piga mapaka ilainike na kua safi kabisa kisha chukua ulemchanganyiko wako wa unga na uchanganye katika mchanganyiko huu wa mayai mimina unga wako kidogo kidogo mpaka umalize wote kisha changanya zile korosho na zabibu kavu na maji wa machungwa ndani ya mchanganyiko wa unga. Kama unga utakua mzito ongeza maji ya machungwa mpaka upate mchanganyiko safi.

Kisha mimina mchanganyiko wako kwenye chombo chochote kile ulichoanda kwa kuokea keki yako. choma keki yako katika oven tayari inamoto kwa dakika 40 hadi 45 chukua kijiti cha kutolea nyama katika meno toothpick choma katikati ikitoka kavu basi keki yako imeiva ikitoka na maji maji bado acha kidogo katika moto iive vizuri.

Toa keki yako katika oven iache ipoe tayari kwa kuliwa.

Friday, February 26, 2010

JINSI YAKUTENGENEZA CROISSANT SAAFIMAHITAJI

240 siagi (Butter au Magarine yeyote kama blue band)

60 gram maziwa ya maji baridi

180 gram sukari

1/2 chumvi kijiko kidogo cha chai
2 mayai mabichi chapa katika bakuli yachanganyike

720 gram unga wa ngano

1.5 amira ya chenga kijiko kidogo cha chai

60gram Maji ya barafu

 
JINSI YA KUTENGENEZA

Chukua maziwa baridi changanya na maji baridi katika bakuli moja lengo la kutumia maji na maziwa baridi yakusaidie wakati unaanda unga wako amira isiumuke kirahisi.

Chukua unga kiasi sio kwenye mahesabu ya huo hapo juu chukua toka nje kabisa ya mahesabu hayo juu kiasi cha gram mia kisha changanya na siagi ya hapo juu kwenye mahitai kiasi cha gram 120 yaani nusu kisha changanya na huo unga hii itakusaidia wakati unasukuma mchanganyiko wako siagi na unga visiachane ili upate urahisi wa kusukuma. ikishachanganyika safi weka katika freezer igande.

Kisha chukua unga, sukari, amira, chumvi na siagi gram 120 kisha changanya kama unamashine kama hauna kanda kwa mkono mpaka upate mchanganyiko safi kabisa na laini.


 
Maji baridi ya barafu

 


Mchanganyiko wa siagi na unga itoe katika freezer tayari kwa kutumia


 

Ipakaze juu ya mchanganyiko wako wa unga baada ya kusukuma na kupata usawa mzuriBaada ya kusambaza funika upande wa kwanza kama picha inavyoonyeshaKisha funika upande wa pili kama picha inavyoonyeshaKisha funika kwa mara ya tatu utapata umbo kama hili


 

Geuza vizuri unga wako ili usukume upate usawa mzuri zaidi


 

Kisha sukuma na upate usawa safi kabisaBaada ya kusukuma na kupata usawa safiKama kawaida funika upande wa kwanza kama inavyoonyesha picha sasa hapa unaanza kuzitafuta kurasa au layers wakati ukakula croissant unaona huwa kama inakurasa  basi hapa ndio unazipanga zipangikeKisha funika upande wapili kama kawaidaFunika upande wa tatu kisha weka katika freezer kwa muda wa nusu saa toa nje unga wako fanya kama mwanzo sukuma upate usawa na kisha funika unga wako mara 3 na rudisha tena kwenye freezer baada ya hapo rudia tena zoezi hilo kwa mara ya tatu na ya mwisho kisha uache unga wako kwenye freezer kwa masaa 4 siagi ikamate vizuri.
Baada ya masaa hayo kupita toa nje na iache iyeyuke kidogo kisha sukuma kupata usawa na anza kukata katika umbo maalumu la croissant

 

Huo ndio muonekano wa hatua ya kwanza ya mkato wa croissant
Baada ya kukata safi pia hapo kwa nyuma lazima ukate kidogo ili kupata unafuu wa kukunja upate umbo halisi la mkunjo wa croissant.Jinsi ya kukata kwa nyumaShika mwisho hadi mwisho kunja pole pole mpka umalize mzungukoHapa ndio mwisho wa mzunguko wa croissant yako
Unaweza kuiacha katika umbo hili pia ni sawa tu na itakua saafi kabisaWengi tumezoea umbo hili halisi sasa ipo tayari kwa kuchomwa ipake ute wa yai ulichanganywa na maji kidogo ili kuongezea nakshi na mng'aro baada ya kuiva
Hii ni croissant iliyoiva na haikupakwa mayai kabla ya kuchomwa imepakwa siagi baada ya kuchomwaHii ni croissant safi iliyopakwa mayai kabla ya kuchomwa katika oven inang'aa laini na ni kau kau kwa juu'

FURAHIA NA FAMILIA YAKO AU KAMA NI MPISHI HOTELINI TENGENEZA KWA KIWANGO SAFI WATU WAFURAHI.


Thursday, February 25, 2010

JINSI YAKUTENEGEZA SHAAMI KABAB
MAHITAJI:

500 gm nyama ya ngombe

100 gm chickpeas ( )

400 gm maji

1 kitunguu kata kidogo dogo sana

4 Pili pili ya kijani mbichi

1 Tangawizi mbichi

3 mayai

3  hiliki kavu

3 (pieces cinnamon sticks) miti ya mdalasini kavu

4 karafuu

8 Mbegu za pili pili manga

1 fungu la majani ya girigilani (corienda)

1 kijiko kidogo cha chai pili pili ya unga nyekundu (red chilli powder)

 1/2 chumvi kijiko kidogo cha chai

2 lita mafuta ya kula


JINSI YA KUTENGENEZA

Loweka njegere kavu kwa masaa 24

Kisha Chemsha nyama ya ng'ombe, njegere, hiriki, karafuu, mdalasini, pilipili manga na chumvi mpaka iive na maji yaanze kukauka katika sufuria yako.

Kisha weka mchanganyiko wako katika blender saga mpaka upate mchanganyiko mzito kama tope.

Kisha changanya yai 1 tu lililopigwa vizuri katika mchanganyiko wako wa nyama uliosagwa kisha ongezea unga wa pili pili nyekundu, pili pili ya kijani, kitua nguu, majani ya girigilaninkisha changanya kwa mkono au mwiko vizuri.

Kisha weka kiaango chako katika jiko mafuta kwajili ya kukaangia yapate moto,chukua mayai mawili yaliyobakia piga vizuri weka pembeni

Chukua mchanganyiko wako wa nyama na tengeneza maumbo ya mvirngo au umbo lolote lile upendalo kisha kandamiza kwa juu upate umbo bapa ili iweze kuiva chovya katika mayai kisha tumbukiza katika mafuta ya moto kwenye kikaango. Kaanga mpaka upate rangi nzuri ya kahawia pande zote nzuri.
Kula ikiwa ya moto kwa kutumia sosi ya ukwaju na salad unaweza kula kama snack pia unaweza kula kama mlo kamili kwenye pilau au biriyani.

Inatosha kwa watu 6 mapaka 8 Furahia chakula na familia yako.
PILI PILI SIO LAZIMA PIA KAMA KUNAKIUNGO HUTUMII AU HUKIPENDI USIWEKE NA KABAB YAKO BADO ITAKUA SAFI TU.

BEEF SEEKH KABABHISTORIA YA SEEKH KABAB:

Seekh kababs zina ladha safi sana kutokana na mchanganyiko wa viungo husika. Kawaida zinachomwa kwa makaa ya moto uliowaka vizuri na kua mekundu kabisa na ndio maana huwa zina harufu safi ya moshi wa kawaida. Kuchoma katika makaa kunasababisha kuleta ladha halisi.

Kebab hii hupendelewa sana na huliwa sana na watu wa Peshawar na kaskazini ya Pakistan na India. Wanapendelea kula na Mkate wa  nani, mint sauce na salad. Kawaida ya watu hawa wanapenda sana BBQ na kawaida ya BBQ lazima uchome katika eneo la wazi katika matamasha yao na sherehe zao na ndugu na jamaa hujumuika maeneo ya wazi ninaimani nawe mdau utafurahia sana chakula hiki.

MAHITAJI:

1kilo nyama ya kusaga ya ng'ombe

2 vitunguu
4 pilipili ndefu za kijani

1 corienda kavu kijiko kidogo cha chai

1ground garam masala kijiko kidogo cha chai

1 yai

Maji

½ Chumvi kijiko kidogo cha chai


2 pili pili nyekundu ya unga kijiko kidogo cha chai
1 jira (cumin seeds) kijiko kidogo cha chai


120gram tangawizi mbichi 

150gram Mafuta ya kupikia

JINSI YA KUTENGENEZA

Weka mchanganyiko wako wa kitunguu , pili pili ya kijani, coriender kavu, jira na tangawizi katika blender saga upae mchangyiko safi uwe mzito kama tope.

Chukua mchanganyiko huo mzito wa mboga weka katika nyama ya kusaga ongeza na yai changanya vizuri kabisa.

Kisha changanya chumvi, unga wa pili pili nyekundu na garam masala katika mchanganyiko wa nyama.

KIsha chukua vijiti virefu vya mwanzi au cha chuma maalumu kwajili ya mshikaki au BBQ kisha weka nyama yako kuzunguka huo mshikaki mapaka ishikamane vizuri na kutengeneza umbo zuri weka katia jiko la mkaa la kuokea au kama hutumii mkaa weka katika oven.

kwa anetumia oven ili vijiti vya mwanzi vya mshikaki (bamboo skwers) tumia aluminium foil kuzungushia havitaungua kabisa. Kumbuka kugeuza mara kwa mara mshikaki wako ili uive pande zote.

Msikaki wako ukishakua mwekundu saafi pande zote mbili nyunyizia mafuta pande zote weka kidogo katika moto tena kwa dakika 3 tu kisha toa utakua umengaa na muonekano safi kabisa.

KUMBUKA

Tumia mkono wako kuweka nyama katika mti wa mshikaki

Loanisha mikono yako ili nyama ising'ang'anie mikononi kama itatokea hali hiyo

Kama utaona haishikani vizuri na ni kavu unaweza ongeza yai

UNAWEZA LISHA FAMILIA YA WATU 12 KWA MCHANGANYIKO HUU. WAWEZA KULA NA UGALI, WALI AU CHIPS NA SALAD.

Wednesday, February 24, 2010

JINSI YAKUPIKA KEKI YA ZABIBU KAVUTengeneza keki ya zabibu kavu kisha ongezea ladha mbali mbali kutokana na upendavyo fata maelekezo hapo chini


Mahitaji:


240gram zabibu kavu

240garm maziwa ya maji

240garm siagi (butter)

½ chumvi kijiko kidogo cha chai

240gram sukari

240gram korosho au walnuts au karanga chochote ulichonacho

500gram unga wa ngano

1 kijiko kidogo cha chai baking soda (Baking powder)

2 mayaiJINSI YAKUTENGENEZA

Washa oveni yako katika joto 325 degree F (165 degree C) kisha kipake chombo chako siagi utakacho tumia kuokea keki yako.

Chukua bakuli changanya unga wa ngano, zabibu na baking soda kasha weka pembeni.

Chukua bakuli nyingine weka siagi na sukari ndani kisha piga mapaka ichanyanyike vizuri na kua laini kabisa kisha vunjia mayai ndani piga paka mchanganyiko wako uwe laini kabisa.

Kisha chukka mchanganyiko wa unga mimina kwenye mchanganyiko wa mayai changanya pole pole mpaka upate mchanganyiko mzito wa wastani kama itakua nzito sana ongeza maziwa kama itakua nyepesi sana ongeza unga.

Kwa kuongeza ladha unaweza kuongezea vitu hiyo hapo chini.

½ kijiko kidogo cha chai kungu manga ya unga (nutmeg)

½ kijiko kidogo cha chai Mdalasini ya unga (cinnamon)

1 kijiko kidogo cha chai vanilla ya maji

Kisha mimina mchanganyiko wako wa keki kwenye chombo utakachotumia kuokea na oka kwa dakika 40 hadi 45 kwa moto ule ulioelekezwa pale juu kama oven yako inamoto mkali zaidi unaweza choma kwa dakika 30 ila hatari ya kuunguza na keki isiive kati kati ni kubwa sana.

Baada ya dakika 40 chukua toothpick choma keki yako katikati toa angalia kama itakua kavu basi keki yako imeiva kama itakua na maji maji keki yaki bado haijaiva hivyo iache katika oven kwa muda kidogo kisha angalia tena.

Toa keki yako iache ipoe tayari kwa kuliwa. 

Monday, February 22, 2010

GREETINGS

WAPENZI WOTE WA BLOG YA CHAKULA SALAMA NAOMBA RADHI KWA KUCHELEWA SANA KUWEKA MAFUNZO KAMA WENGI WENU MLIVYOOMBA SASA KAZI INAENDELEA KILA SIKU MTAPATA MAFUNZO MBALI MBALI MFULULIZO BILA KUKOSA MAONI YENU NI MUHIMU SANA ILI KILA MMOJA APATE KUFAHAMU KAMA HUJAELEWA ULIZA UPATE UFAFANUZI ZAIDI WAPENZI WA BITES, KEKI, SALAD SOON MTAFURAHI NAWASHUKURU WOTE KWA USHIRIKIANO WENU NAWATAKIA KAZI NA SIKU NJEMA CHEF ISSA.

JINSI YA KUPIKA WALI WA BIRYAN YA KUKU, NG.OMBE AU MBUZI

Mahitaji
1 kilo mchele wa basmati mrefu

1 kilo nyama iwe ya kuku au ng'ombe au mbuzi kata katika umbo dogo la kutosha kula kisha ichemshe na tangawizi na kitunguu swaumu, unga wa binzari (turmeric powder) pili pili manga na chumvi ili kuweka ladha nzuri. Ikisha iva itoe iweke pembeni na mchuzi wake uweke pembeni utautumia baadae.

1 kilo ya vitunguu kata slice ( mviringo)

1 kilo nyanya nyekudu zilizoiva, osha vizuri kisha katakata saizi ndogo ndogo sana

240 gram ya mafuta ya kupikia

240 gram ya samli au mafuta yeyote ya kupikia

2 maggi chicken soup cubes

3 kijiko kidogo cha chai unga wa pilipili mwekundu

1/2 kijiko kidogo cha chai unga wa binzari (turmeric powder)

3 kijiko kidogo cha chai unga wa girigilani (coriander powder)

2 kijiko kikubwa cha chakula mchanganyiko wa tangawizi na kitunguu swaumu vilivyosagwa (ginger-garlic paste )

50 gram korosho iliyo kaangwa usizisage zibaki nzima

50 gram majani ya girigilani (fresh coriander leaves, washed and chopped)

8-12 mbegu za nzima ya hiriki (green cardamoms)

4 bay leaves ( sifahamu kiswahili chake)

15 mbegu nzima ya pili pili manga (whole black peppercorns)

30 gram majani mabichi ya minti ( mint leaves )

salt kulingana na ladha yako binafsi

Jinsi ya kuanda

Weka mafuta katika sufuria yako iliyo juu ya moto tayari, kisha kaanga nyama yako iliyokwisha chemshwa mpaka iwe na rangi ya kahawia (golden brown)

Kisha itoe nyama hiyo na ichuje mafuta ili mafuta yanayobaki weka kitunguu na endelea kukaanga kwa dakika 7-10 kisha weka unga wa binzali, unga wa pili pili mwekundu, unga wa girigilani, bay leaves, mbegu za hiriki na nusu ya mbegu za pili pili manga.

Changanya vizuri mpaka utapata mchanganyiko mzuri mkavu miminia humo maji uliyotunza baada ya kuchemshia ile nyama yako na kuiweka pembeni ipoe. kisha weka nyanya fresh ndani ya sufuria yako pika mpaka maji yakauke na mafuta yaanze kuoneka kwa juu ndani ya sufuria.

Kisha weka nyama yako ndani ya sufuria pole pole halafu punguza moto acha ijipike kwa muda mpaka mchuzi wako na nyama vikamate ladha pia usisahau kuweka chumvi kulingana na ladha unayopenda.

Chukua sufuria nyingine weka mafuta ya samli na vitunguu ilivyoslice kisha kaanga na majani ya girigilani, majani ya mint na korosho funika kwa dakika 10 picha inaonyesha hapo chini, kisha weka wali wako mkavu uliokwisha oshwa vizuri na uchanganye vizuri ongeza vikombe 5 vya maji na chumvi kidogo mchele ukishaanza kuchemka funika sufuria lako na punguza moto maji yakisha kauka kiasi weka mchanganyiko wa ile nyama yako nusu tu juu ya wali wa basmati acha wali uive kabisa kisha itakua tayari kula na pakua chakula chako kikiwa cha motoWali wa pishori ( Basmati rice) uliokwisha iva


Wali wa pishori ( Basmati rice) uliokwisha iva ukakaangwa na vitungu na korosho


muonekano wa majani ya girigirani wakati wa kukaangwa


Nyama ya kuku iliokaangwa vizuri na viungo na nyanya ukapata mchanganyiko mzuri mzito

Muonekano halisi wa biriyani yako baada ya kuiva ikiwa imechanganyikana na nyama pia kumbuka kunamchuzi mzito na nyma ilibaki pembeni mlaji ataweza kujongezea kiasi apendacho.

Furahia chakula hiki pamoja na familia yako.

JINSI YAKUTENGENEZA CHICKEN SANDWICH


Muonekano chicken sandwich baada ya kuikataMchanganyiko halisi wa chicken mayonaise ukiwa juu ya jani la saladunaweza tumia mkate wa aina yeyote ile slice au huu mrefu
Muonekano halisi wa sandwich ya kuku baada ya kukatwa tarayi kwa kula. kama unapenda kula ikiwa ya moto weka katika sandwich toaster funika ipate rangi ya kahawia toa na kula ikiwa ya moto kwa chipi na tomato sauce na salad saafi kabisa.

 
CHICKEN MAYONISE SANDWICH

Mahitaji:

Jinsi ya kupika kuku ya sandwich:

1 kilo ya kifua cha kuku au miguu  ya kuku toa ngozi ili kukwepa mafuta.
1 tangawizi kubwa
3 mbegu za  pili pili manga
Chumvi kulingana na ladha unayotaka

Chemsha mchangayiko huo wote pamoja na kuku mpaka kuku iive vizuri na iwe laini kabisa kisha toa katika jiko na uache upoe.


Mahitaji kwajili ya sandwich:

1 loaf of wholemeal bread or French wholemeal loaf (sliced)

1 pili pili hoho iliyokatwa saizi ndogo ndogo

1 kitunguu kilichokatwa saizi ndogondogo

3 au 4  mayonaisi kijikokikubwa cha chakula
3 nyanya nyekundu kata mviringo nyembamba (sliced)

1 tango zuri kata mviringo nyembamba (sliced)

1 lettuce salad nzuri ya kijani

Jinsi ya kuandaa:

Chukua  kuku aliepoa nyofoa nyofoa nyama ya kuku weka mifupa pembeni kisha weka ile nyama katika bakuli changanya mayonaise, chumvi, kitunguu, pili pli hoho na pili pili manga ya unga changaya vizuri kabisa.

Kama mchanganyiko wako ni mkavu ongeza mayonaise na lemon juice kidogo kuongeza ladha zaidi.

Chukua mchanganyiko wako wa kuku weka juu ya jani la salad panga vizuri usijaze sana ili uweze kufunika na kipande kingine cha mkate kilichobaki kisha weka slice ya tango na ya nyanya juu ya mchanganyiko wako wa kuku na mayonise.

Chukua kipande kingine cha mkate kilichobaki na funika kwa juu unaweza kula tayari au kama unapenda kau kau unaweza weka mkate wako huo kwenye toaster mashine na kuukausha kwa muda mapaka ukapata rangi ya kahawia na kua na ladha tofauti na ukala sandwich ya moto.

Sunday, February 21, 2010

JINSI YA KUPIKA MAPISHI MBALI MBALI YA WALI

KWA WALE NDUGU ZANGU MLIOKO UGHAIBUNI MCHELE ASILIMIA 90% HAUNA LADHA NA HARUFU NZURI KAMA TULIOUZOEA NYUMBANI CHUKUA UJANJA HUU ILI UFANYE WALI WAKO UWE WA KUNUKIA NA LADHA SAFI KABISAKaroti iliyokwaruzwa vizuri, nyanya na vitunguu vilivyokatwa katika umbo dogo dogo rahisi kwa kuiva


Mchanganyiko wa karoti, kitunguu na nyanya katika kikaango chenye mafuta na moto mkali pika kwa dakika 5 tu usiache ziive sana kisha changanya wali wako ambao umeshaiva.Huu ni wali ulioiva na ukachanyanywa na mchanyiko wako wa caroti, utapata harufu nzuri na ladha nzuri sana kwa kupata harufu na ladha nzuri zaidi unaweza ongezea pilipili hoho au girigilani ( Corriender leaves).


Mahitaji
720gram caroti iliyokwaruzwa

480gram Basmati rice ( mchele wa pishori) iliyopikwa

2 vitunguu vikubwa vikate katika size ndogo

1 Nyanya moja kubwa ikate katika size ndogo

1 fungu la majani ya girigilani

2 kijiko kikubwa cha chakula karanga zilizokaangwa kwajili ya kupambia

3 kijiko kidogo cha chai cha mafuta ya kula

Chumvi weka kulingana na ladha na mahitaji yako

Jinsi ya kuandaa:

Pasha moto sufuria lako au kikaango weka mafuta kisha weka vitunguu kaanga kiasi tu visiungue au kua na rangi ya kahawia vilainike tu inatosha.

kisha weka nyanya zikaange mpaka zichanganyike kabisa zitengeneze rojo rojo
Kisha weka caroti zilizokwaruzwa katika mchanganyiko wako kaanga na zichanganyike vizuri

Kisha weka wali wako wa basmati ulioiva katika mchanganyiko wako wa karoti changanya vizuri kisha mimina majani ya girigilani na changanya pole pole mwisho kabisa weka karanga zako ambazo zimekaangwa vizuri kama unatumia.

Mapishi haya unaweza tumia mchele wa aina yeyote ile sio lazima mchele wa basmati

JINSI YA KUPIKA MKATE WA MCHELE


Mkate wa mchele mwekundu


Mkate wa mchele pori
Mahitaji

540gram unga mweupe wa mchele
240 gram unga wa kahawia wa mchele
1 kijiko kidogo cha chai gelatin isiyo na ladha
3 Sukari kijiko kikubwa cha chakula
1 1/2 kijiko kidogo cha chai chumvi
2 kijiko kikubwa cha chakula corn starch
120 gram maziwa ya unga
2 1/4 kijiko kidogo cha chai amira ya chenga
3 mayai
1 kijiko kidogo cha chai vinegar
3 Kijiko kikubwa cha chakula cha mafuta ya alizeti au ya karanga au ya mahindi chaguo lako.
12omls maji ya vugu vugu (110 degrees F/45 degrees C)

Maelekezo ya Upikaji

Changanya unga wa mchele mweupe, unga wa mchele wa kahawia na chumvi. Changanya vizuri sana uchanganyike kabisa katika bakuli moja.

Chukua bakuli nyingine changanya gelatin isiyo na ladha, sukari, corn stach, maziwa ya unga, mayai yaliyopigwa, vinegar na mafuta changanya mapaka ichanganyike vizuri zaidi.

Kisha Changanya ulemchanganyiko wa unga na ule mchanganyiko wa bakuli la pili lenye mayai na maziwa pia weka amira ya chenga iwe changanya vizuri mpaka upate mchanganyiko wa kati sio kimiminika kama mchanganyiko wa keki na sio ngumu kama mchanganyiko wa mkate kama bado nzito tumia maji salama ya baridi kiasi ili kulainisha mchanganyiko wako.

Weka katika sufuria au chombo maalumu kwa kuokea chenye urefu wa inchi 9 na upana wa inchi 5 acha katika joto la chumba mchanganyiko wako uvimbe na kua mara mbili ya ulivyokua mwanzo. washa oven yako katika joto la 325 Degree F au sawa na 165 degree C mpaka mkate wako utengeneze gamba gumu la kahawia saafi. Kisha toa mkate wako katiak oven uache kwa dakika 10 katika chombo ulichopikia kisha utoe uache nje katika joto la chumba kwa dakika tano kisha mkate wako uko tayari kwa kuliwa.

FURAHIA NA FAMILIA YAKO KWA KUBADILISHA LADHA YA MKATE PIA KWA WALE WENYE MATATIZO WASIO TUMIA NAFAKA ZENYE GLUTEN MTAKUA MMEFAIDIKA PIA MAKATE HUU UNAWEZA UKAUBADILISHA LADHA TOFAUTI KWA KUONGEZEA VITU MBALI MBALI KAMA ZABIBU KAVU, STRAWBERY, KARANGA, MBEGU ZA MABOGA, MBEGU ZA ALIZETI, MBEGU ZA UFUTA.

Thursday, February 4, 2010

WAJUA DAWA YA MAFUA SAFI KABISA

Ndugu zangu watanzania kinywaji hiki ni dawa ya mafua safi kabisa unatumia siku moja tu unakua na nafuu kabisa ila dozi yake inataka utumie mwezi mmoja hadi mwezi mmoja na nusu mfululizo bila ya kuacha.

MAANDALIZI
Chukua maji lita moja
Chukua asali vijiko 3 vikubwa vya chakula
Chukua tangawizi ya unga kijiko kimoja kikubwa cha chakula au chukua tangawizi mbichi itwange upate mchanganyiko uliopondeka kijiko kimoja kilichojaa.

Chemsha mchangyanyiko wako wote huo kwa pamoja mpaka ichemke vizuri inategemea na moto wa jiko lako lakini mpaka utakapoona imechemka vizuri usiache ikakaukia jikoni nashauri dakika 15 hadi 20 inatosha.

Kisha iache ipoe kunywa nusu glasi mara tatu kwa siku yaani asubuhi , mchana na usiku.

Kwa wale walio na mafua sugu yanadondoka muda wote na kupiga chafya nyingi sana zisizo na idadi basi zitakata mara moja na siku ya pili zitaisha kabisa kumbuka kunywa dawa hii mwezi mzima au hadi miezi miwili utapona kabisa.

Wednesday, February 3, 2010

USHAURI KWA MTOTO ASIEPENDA KULA

Mdau mmoja ameomba ushauri kwa mtoto asiependa kula, matatizo ya mtoto kutopenda kula ni mengi yanaweza kusababishwa na tabia binafsi au maradhi. Kama mtoto yuko salama hana maradhiila hapendi tu kula kazi ni ndogo sana kumbadilisha ili apende kula.

Inawezekana unandaa chakula safi sana lakini bado mtoto anasumbua kula ili kumbadilisha tabia apende kula unatakiwa kumtengenezea kwanza hamu ya kula maana bila ya kuwa na hamu ya kula hata chakula kiwe kizuri vipi huwezi kula vizuri.

Hamu ya kula inatakiwa kuanzia asubuhi unapofungua kinywa, tengeneza chai iwe ya rangi au ya maziwa weka tangawizi ya unga kwenye nusu lita ya maji au maziwa weka tangawizi kijiko kidogo cha chai mzoweshe mwanao chai hii kila siku asubuhi tangawizi ni kiungo kizuri kinachosaidia kumengenya chakula tumboni na kusababisha njaa haraka na hamu ya kula.

Hapo utakua umemtengenezea mtoto hamu ya kula mchana, kwa kumuandalia mtoto hamu ya kula chakula cha usiku tengeneza juisi ya Pasheni au Embe au Nanasi au tunda lolote lile kumbuka kuchanganya tena kijiko kidogo cha chai kilicho jaa tangawizi na usage pamoja na mchanyanyiko wako mpe mtoto glasi moja saafi kabla ya kula na mabadiliko utayaona usimpatie baada ya kula maana itamsababishia njaa.

Fata maelekezo vizuri mabadiliko utayaona ndani ya siku moja tu.

Mdau umeuliza swali zuri sana kuhusu mtoto anaweza kutumia juice yenye tangawizi?
kawaida mtoto akiwa ameanza kula chakula tofauti ingawa bado anaendelea kunyonya maziwa ya mama yake.

Katika mchanganyiko wa juice yako weka tangawizi mbichi ni nzuri zaidi weka kidogo sana ambayo haitaweza kumuwasha onja mpaka uone mchanganyiko ni sahihi kisha mpatie itafanya kazi safi sana sio lazima iwashe hata kwa mtu mzima weka kiasi tu iwe na ladha na itafanya kazi safi kabisa dada Shamimu utakua umenielewa vizuri.