CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Saturday, July 20, 2013

JIFUNZE KUTENGENEZA KITAFUNWA HIKI CHA UNGA WA MAHINDI NA MAJNI YA KITUNGUU

 
 RECIPE SAFI KABISA YA KITAFUNWA HIKI CHENYE MCHANGANYIKO WA UNGA WA MAHINDI NA MAJANI YA KITUNGUU

MAHITAJI 
120 gram unga wa ngano
120 gram unga wa mahindi wa njano
1/4 kijiko kidogo cha chai Baking Soda
1 pc yai
120 gram maziwa
60 gram majani ya vitunguu maji
1 pili pili hoho
5 gram chumvi
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
 
 
Pasha mafuta katika kikaango kwajili ya kukaangia. Kisha changanya unga wa ngano, unga wa mahindi, chumvi na baking soda.
 
 
Kisha changanya majani ya kitunguu maji na pili pili hoho.
 
 
Chukua bakuli safi, Changanya vizuri maziwa na mayai mpaka ichanganyike vizuri kabisa.
 
 
Kisha mwagia mchanganyiko wako wa maziwa kwenye mchanganyiko wa unga na changanya vizuri kabisa.
 
 
Mimi huwa natumia icecream scoop wewe unaweza tumia pia ua ukatumia kijiko 
 
 
Kisha chota tupia katika mafuta yamoto na uendelee kukaanga.
 
 
Kumbuka kugeuza geuza wakati zinaendelea kuiva.
 
 
Kumbuka kuweka moto wa kati ili mafuta yasiwe yamoto sana zitababuka na zisiive vizuri au mafuta yakiwa sio yamoto safi itasababisha zisiive na ziwe chini ya kiwango.
 
 
Ukitoa katika mafuta zikaushe katika towel zichuje mafuta.
 

Enjoy zikiwa zamoto na ndio zinakua bado hazijapoa na fresh.


Pata kitafunwa hiki kwa chai ya saa 4 asubuhi au chai ya saa 10 jioni safi sana.
 


Friday, July 19, 2013

JIFUNZE KUTENGENEZA KITAFUNWA HIKI CHA MCHAGANYIKO WA NGANO NA UFUTA

 
HAPO CHINI NI KITAFUNWA CHA MCHANGANYIKO WA MBEGU ZA UFUTA NA UNGA WA NGANO.

MAHITAJI
240 gram maji ya vugu vugu
 2-1/2 kijiko cha chai amira ya chenga
1-1/2 kijiko kikubwa cha chakula sukari
600 gram unga wa ngano
1 kijiko kidogo cha chai chumvi
1 kijiko kidogo cha chai mafuta ya kula
 1 kijiko kikubwa cha chakula mbegu za ufuta
 1 Kitunguu kikubwa

JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
 

 
Chukua bakuli safi kisha weka maji, amira ya chenga, na sukari. Iweke pembeni kwenye joto la kawaida kisha iache mpaka ianze kutoa mapovu ndani ya dakika 5.

 
Kisha mwagia unga pole pole na uchanganye  kwa kutumia mwiko wa mbao pole pole pamoja na chumvi weka unga kidogokidogo huku ukichanganya mpaka mchanganyiko wako uwe safi kabisa( Ukipenda unaweza kuchanganya kwa kutumia mikono haina neno).


Baada ya kuchanganya safi kabisa huu ndio utakua muonekano. Hamishia katika sehemu uliyomwagia unga wa ngano hasa juu ya meza kisha endelea kukanda mpaka mchanganyiko uwe mgumu na usio nata katika mikono yako kwa dakika 5 tu, kama bado itakua laini unaweza kuongezea unga.


Chukua bakuli kavu kisha lipake mafuta ya wastani na weka humo ule mchanganyiko wa unga na funika kwa juu na karatasi ya nailoni ili kuongeza joto na isaidei kuumuka.

 
Ukifunika safi unga wako utakua umeshaumuka ndani ya saa 1 tu.

 
Baad ya kuumuka kata unga huu katika vipande sawa 6. Tengeneza katika umbo la duara na toboa kwa kidole kati kati kama muonekano katika picha. .Paka mafuta juu ya meza kisha weka hapo hiyo miduara na funika kwa kitambaa laini juu yake, acha mpaka iumuke ndani ya dakika 20 hadi dakika 30.


Chukua kikaango kikubwa au sufuria yenye maji mengi na kisha yachemshe yapate moto . Weka kijiko kimoja kikubwa chachakula sukari katika maji ya moto kwenye kikaango. KIsha tupia katika maji hiyo miduara ya unga uliyoandaa kwa dakika 1 kisha geuza upande mwingine kwa dakika 1 tena.
 
 
KIsha toa na weka katika baking sheet au baking tray ambayo umeipaka mafuta.

 
Kwasababu imetoka katika maji moto hapa unaweza mwagia juu chochote unachopenda wewe mimi nilitumia ufuta lakini pia unaweza weka hata karanga au korosho.
 
 
Oka katika ovena yenye moto tayari kwa dakika 5 hadi 10 hakikisha imekua ya kahawia safi kabisa au golden/crusty on the surface. Muda wa kuoka unategemea oven na oven inaweza kuchukua hata dakika 20 pia. Kipimo cha kujua sasa imeiva hakikisha upande wa chini wa kitafunwa hiki unakua mkavu na wa mgumu kabisa na rangi ya kahawia.
 
 
KIsha toa katika ovena na acha ipoe juu ya wire rack. Kitafunwa hiki ni maarufu san kwa upande wa nchi ya marekani.