CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Saturday, March 30, 2013

JIFUNZE JINSI YA KUPIKA MKATE HUU MWEUPE

JIFUNZE KUTENGENEZA MKATE HUU MWEUPE NI RAHISI NA NAFUU KUANDAA ONYESHA UJUZI WAKO KATIKA FAMILIA
 
MAHITAJI
 
1 kg unga wa ngano
2 kijiko kidogo cha chai chumvi
240 gram maziwa ya maji ya vugu vungu
60 gram maji ya vugu vugu
2 kijiko kikubwa cha chakula siagi, iyeyushe
3 kijiko kikubwa cha chakula asali
2 kijiko kidogo cha chai amira ya chenga

JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
 
Muda wa maandalizi : Masaa 2 hadi 4
Muda wa mapishi : Dakika 30 hadi saa 1
Idadi ya walaji : Watu 4
Ujazo : Unapata mkate wenye 9-inch
 
 
Chukua robo tatu ya unga pamoja na chumvi kisha chukua mchapo na uchanganye. 

 
 Chukua bakuli safi kavu kisha changanya maziwa, majina, siagi, chumvi pamoja na amira. Hakikisha joto la maziwa na maji liwe 110 degrees.

 
 Mimina mchanganiko wako wenye maziwa katika unga.

 
Anza kukanda pole pole 

 
Hapa mchanganyiko wako umeshaanza kushikana. 

 
Chukua mchanganyiko wako kisha weka juu ya meza hakikisha umemwagia unga kwa juu endelea kukanda vizuri kwa dakika 10.

 
Kama unafikiri mchanganyiko bado una maji maji, basi chukua robo ya unga iliobakia tumia kijiko kikubwa cha chakula ongeza kimoja kimoja epuka kuweka unga wote ukazidisha.

 
Chukua bakuli safi na kavu, kisha lipake mafuta na weka mchanganyiko wako katika hiyo bakuli. 

 
KIsha tumia plastic na funika weka sehemu yenye joto, jikoni kuna joto.

 
Hakikisha mchanganyiko wako umeongezeka mara 2, ndani ya dakika 40 mpaka 50. 

 
Kisha chukua mchanganyiko wako ukande vizuri na weka katika chombo chako cha kuokea kiwe cha chuma au cha kioo kama changu chenye ukubwa wa  8.5 X 4.5 X 2.5 (1.5 Lita).

 
 Kisha funika tena kwa plastic

 
 Weka pembeni kwa dakika 20 mpaka 30 itakua imeshaumuka vizuri kama unavyoona katika picha weka katika oven.

 
 Kumbuka oven yako unatakiwa uiwashe kabla katika joto la 350 degrees, ukishaweka unga katika oven unaweza rushia maji kidogo ili kuweka mvuke utakao saidia kuweka rangi nzuri ya brown na kua na gamba gumu. Oka kwa dakika 40 mpaka 50 mkate wako utakua umeiva.

 
Toa mkate wako katika pan, hamishia katika wire rack, ili mkate uweze kupoa.

 
Kata kata vipande na wapatie walaji, unaona mkate ulivyochambuka. 

 
Unaweza ukavuta picha huu mkate ni mtamu kiasi gani ukishapaka siagi kwajuu? au ukipaka jam pia? Ni mtamu sana sana.
 


Thursday, March 21, 2013

JIFUNZE KUTENGENEZA YAI JICHO LA NG'OMBE NA KIPANDE CHA MKATE

 
RECIPE SAFI KABISA YA KUTENGENEZA KITAFUNWA HIKI KWA WAKATI WA MAPUMZIKO YAHA MAREFU.
 
MAHITAJI
 
1 Yai
1 kipande cha mkate
1/2 kijiko kidogo cha chai siagi
5 gram chumvi
2 gram pili pili manga
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
 
 
Chukua kipande cha mkate kunja nusu kisha kata mduara kati kati.

 
Huu ndio muonekano wa mduara baada ya kukata

 
Chukua brush na kisha paka pande zote mbili siagi.

 
Chukua kipande cha mkate kisha weka katika kikaango chenye moto wa wastani ili isiungue.

 
Kisha pasua yai na mimina kati kati ya mkate

 
Kisha nyunyizia chumvi na pili pili manga kwa juu ya yai nali mkate.

 
Baada ya dakika 3 hadi 4, upande mmoja uta.kua umeiva geuza upande wa pili

 
Upande wa pili pika kwa dakika 2 tu utakua umeiva pia.


HUU NI MUONEKANO WA MKATE JICHO LA NG'OMBE UKIWA UMEIVA WAANDALIE FAMILIA WAFURAHIE.
 
UKITAKA KUENJOY ZAIDI FUNGUA FACEBOOK PAGE KWA KU CLICK HII LINK http://www.facebook.com/pages/Active-chef/509561519067534 KISHA CLICK LIKE NA UTAKUA MWANACHAMA UTAWEZA PATA HABARI ZOTE ZINAZOHUSU MAPISHI NA PIA MAPISHI MAPYA KILA SIKU.

Tuesday, March 5, 2013

JIFUNZE KUTENGENEZA KEKI HII YA MCHANGANYIKO WA KOKOA BILA YA KTUMIA MAYAI

 UTENGENZAJI WA KEKI HII YA MCHANGANYIKO WA KOKOA BILA YA KUTUMIA MAYAI
 
MAHITAJI
250 gms unga wa ngano
250 gms sukari
250 gms siagi
50 gms unga wa cocoa
1 kijiko kidogo cha chai baking soda
1/2 kijiko kidogo cha chai baking powder
1/2 kijiko kidogo cha chai chumvi
1 kijiko kidogo cha chai vanilla essence
250 gram pureed Mori Nu silken Tofu (Badala ya mayai 4)

JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAFUNZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi : Dakika 30 mpaka saa 1
Muda wa kupika 30 mpaka saa 1
Idadi ya walaji: Watu 4
 
Hii ni picha ya Tofu inauzwa madukani.
 
 
Washa oven katika moto wa 180 deg C (350 deg F). Paka siagi au mafuta pia nyunyizia unga kwa mbali kwenye pan  ya ukubwa huu (8″x8″), Fungua box lenye mchanganyiko wa tofu na upoige kama wewe hutumii mayai nakama unatumia mayai basi piga mayai 4 piga kwa mkono au mashine mpaka uone mapovu.

 
Weka katika chujio la chuma unga wa ngano, cocoa powder, baking powder, baking soda pamoja na chumvi.

 
Hakikisha umechekecha vizuri na kisha weka pembeni.

 
Chukua siagi na sukari pia piga kwa mashine au mchapo changanya na vanilla essence.

 
Chukua mchanganyiko wa tofu au mayai weka katika mchanganyiko wa siagi na sukari. 
 
 
Tumia mchapo au mashine chapa mpaka uchanganyike safi kabisa mchanganyiko wako.
 
 
Sasa mimina mchanganyiko wa unga pole pole katika mchanganyiko wa siagi na mayai au tofu

 
Kisha endelea kupiga kwa mchapo au mashine mpaka mchanganyiko wako uchanganyike vizuri.

 
Kama mchanganyiko wako umekua mzito basi unaweza mimina pole pole maziwa huku ukiendelea kuchanganya.

 
Kisha mimina mchanganyiko wako mzito katika pan,

 
Hakikisha unasambaza vizuri kwa juu iwe na muonekano mzuri kabisa.
 
 
Kisha choma kwa dakika 45 mpaka 5 itakua imeiva. ( oven yangu inachoma kwa dakika 32 tu )

 
Huu ndio muonekano wa keki baada ya kuiva, hapa nimeiweka ili ipoe.
 
 
 
Weka keki yako katika tray yake kisha mwagia sukari ya unga au icing sugar kwa juu kuongeza mvuto. Unaona muonekano safi kabisa. Pika kwa biashara au kitafunwa nyumbani.
 
 


JIFUNZE KUTENGENEZA HOT CHOCOLATE YA MCHANGANYIKO NAZI

 
KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA MUDA SI MREFU
 
MAHITAJI
 
500gram low fat Milk yanapatikana duka lolote la chakula
200gram tui la nazi
60 gram maziwa ya kawaida yaliyochemshwa yakapoa
1 kijiko kikubwa cha chakula Cocoa powder
1/4 kijiko kidogo cha chai Vanilla
50 gram fresh whipped cream (sio lazima)
vipande vya Chocolate (sio lazima)
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi Dakika 15
Muda wa kutengeneza: Dakika 15
Idadi ya walaji: Watu 3
Ujazo baada ya kuandaa : 600 ml

 
Katika kikaango mimina maziwa aina zote pamoja na tui la nazi.

 
Chemsha mchanganyiko huu kwa moto mdogo, hakikisha unakoroga pole pole.

 
Kisha mimina unga wa cocoa  na uendelee kukoroga

 
Hakikisha unaendelea kukoroga ichanganyike vizuri.

 
Toa katika moto kisha mimina vanilla katika mchanganyiko wako.

 
Mchanganyiko wako utakua mziko kiasi mpatie mnywaji  ikiwa ya moto juu yake unaweza pamba na whipped cream pamoja na unga wa chocolate. Hutaweza kusikia ladha kali ya nazi ila kama wewe ni mpenzi sana wa nazi punguza idadi ya maziwa kisha weka nazi zaidi kwa ladha unayotaka. Muandalie mgeni nyumbani au watoto kinywaji hiki rahisi na cha haraka kuandaa.

 


JIFUNZE KUTENGENEZA KITAFUNWA CHA DENGU


KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA MUDA SI MREFU

MAHITAJI

250 gram dengu kavu au Chickpeas,
1 kijiko kidogo cha chai mafuta ya kupikia
1 Bay Leaf sio lazima ni kwajili ya harufu
1/2 kijiko kidogo cha chai mchanganyiko wa unga wa Cumin na Coriander
1/2 kijiko kidogo cha chai Pili pili nyekundu ya unga
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
 
Muda wa maandalizi : Masaa 4 hadi 8
Muda wa mapishi : Dakika 30 hadi saa 1
Idadi ya walaji : Watu 4
Baada ya kuiva ujazo : 500 gram