Tuesday, January 19, 2010
WAPENZI WA BLOG YETU YA CHAKULA
NIMEKUA KIMYA KWA MUDA NILIKUA NAJIBU MAIL NYINGI SANA ZA MASWALI NA NYINGINE ZA MAOMBI YA RECIPE BINAFSI KWAJILI YA MAPISHI YA NYUMBANI KWAHIYO ILIKUA NI NGUMU KWELI KUANDAA NA KUWEKA RECIPE KATIKA BLOG YETU NAIMANI WOTE WALIONITUMIA MAIL WAMEPATA RECIPE HIZO NA WAMEZIFANYIA KAZI SASA TUNAENDELEA NA MAFUNZO
Saturday, January 9, 2010
BISKUTI SAAFI ZA KARANGA
Namna ya kutengeneza biskuti safi za karanga na jam pia zinadumu kwa miezi 3 mpaka 6 zikiwa katika ubora safi wa kuliwa inategemea na usafi na utunzaji wako. Unaweza tumia aina yeyote ile ya karanga mfano almonds, ground nuts, wholenuts au pistacchio. pia ukiweza kuzichanganya hizi zote itapendeza zaidi.
Kina mama kwa chai ya saa 10 jioni mpatie mwanao au mzee biskuti hii na chai au kahawa utakua umefanya jambo la maana sana. Kwenye migahwa mnapowahudumia wageni walioagiza kahawa au chai tupu unaweza mpatie kipande hiki cha biskuti bila ya kumchaji kama motisha ili kuongeza hamasa na kumfanya mteja ajisikie kua yeye kweli ni mafalme na thamani ya pesa yake inatumika kihalali.
Biscuti hii sio gahli na ni rahisi sana kutengeneza na inakaa kwa muda mrefu sana.
Vitu vyakuandaa
Unga wa ngano gr 600
Sukari gr 240
Kijiki kidogo cha chai robo chumvi
Karanga gr 200
Butter ( siagi) gr 240
Vijiki 2 vya chai vanilla ya maji
Mayai 2
Ganda la machungwa 2 lililokwaruzwa ( lemon zest)
Hatua za kutengeneza
Chukua sukari na siagi changanya pamoja
Baada ya kuchanganyika safi weka maganda ya limao, vanilla, chumvi, karanga na mayai.
Kisha weka unga wa ngano changanya uchanganyike safi kabisa toa weka katika friji kwa muda mchanganyiko wako upoe na uwe mgumu zaidi kwajili ya kutengeneza shape nzuri ya biskuti.
Unga wa ngano gr 600
Sukari gr 240
Kijiki kidogo cha chai robo chumvi
Karanga gr 200
Butter ( siagi) gr 240
Vijiki 2 vya chai vanilla ya maji
Mayai 2
Ganda la machungwa 2 lililokwaruzwa ( lemon zest)
Hatua za kutengeneza
Chukua sukari na siagi changanya pamoja
Baada ya kuchanganyika safi weka maganda ya limao, vanilla, chumvi, karanga na mayai.
Kisha weka unga wa ngano changanya uchanganyike safi kabisa toa weka katika friji kwa muda mchanganyiko wako upoe na uwe mgumu zaidi kwajili ya kutengeneza shape nzuri ya biskuti.
Baada ya mchanganyiko waku kukamilika na kua katika umbo gumu, chukua baking sheet au karatasi ya kuokea kama hauna basi tumia karatasi nyeupe ipake mafuta ya siagi yote ilowane utatumia kuokea na haita ungua kwenye oven yako. Kisha kata kipande kiasi na zungusha kwa mikono yakua miwili utengeneze umbo la duara kama mpira kisha ingiza kidole cha mwisho kidogo kati kati ya umbo hilo la duara utapata shimo dogo kisha panga biskuti hiyo kwenye tray ukisubiri hatua inayofuata.
Chukua kiini cha njano cha yai changanya na maji kidogo tu ili upate ute mwepesi kisha chukua brush na pakaza ute huo juu ya biskuti zako zote saafi kabisa.
Katika picha hapo juu ni mfuko wa nailoni ukiwa na mchanganyiko saafi wa matunda aina ya redcourant pia pembeni unaweza ona tunda hilo halisi mchanganyiko huo wa tunda utauweka katika lile shimo kwenye biskuti ilikuongezea ladha zaidi.
Tumia mfuko wa nailoni kuweka mchanganyiko huo wa ladha ya tunda unaweza weka ladha yeyote ile ya tunda ulipendalo au jam uwezo wako tu na bado biskuti itapendeza sana. kisha weka kwenye oven amabayo tayari inamoto wa watani choma kwa muda wa kisha toa weka pembeni zipoe.
Biskuti zetu zipo pembeni na zimeshapoa tayari kwa matumizi ya kula zikiwa na rangi safi ya kahawia na nyekundu ya redcorant.
muonekano huo hapo juu ni maumbo mbali mbali ya biskuti lakini zikiwa zinatumia njia na vipimo sawa vya uandaaji, tofauti yake ni jinsi yakukata kenye maumbile.
Hiyo yenye rangi nyeusi ni baada ya kuiva na kupoa unachovya kwenye chocolate iliyoyeyushwa kisha unaiweka biskuti yako pembeni tena ili ipoe na chocolate ishikevizuri.
Hiyo yenye rangi nyeupe, chukua ute mweupe wa yai piga na sukari nyeupe kiasi kidogo sana kisha utapata povu chukua na pakaza juu katika biskuti mbichi kisha choma itakapo iva itatoka na muonekano huo
Utapunguza gharama ya kuwanunulia watoto biskuti madukani kwani utengenezaji wake ni nafuu sana na unatengeneza nyingi zitakazo kaa kwa muda mrefu sana bila kuharibika wala kupoteza ubora.
Friday, January 8, 2010
UTENGENEZAJI WA ICE CREAM BILA YA KUTUMIA MASHINE
Ice cream ni kifunga hamu ya kula ( Dessert ) moja wapo nzuri sana na inaweza kuliwa na watu wa lika zote pia unaweza kula ice cream muda wowote ule utakaojisikia na ukafurahia hasa ukiangalia hali ya joto inayopatikana nchini kwetu. Fata maelezo hapochini jinsi ya kutengeneza pamoja na mahitaji ili ufanikishe uandaaji wako.
Vitu vya kuandaa.
Maziwa ml 240
Sukari ml 240
Chumvi kijiko kidogo cha chai robo (1/4)
Vanilla ya maji kijiko kikubwa cha chakula 1/2
Vanilla ya mti ml 120
Low fat maziwa ml 120
low fat cream ml 120
Whipping cream yenye ubaridi wa wastan ml 480
Biskuti zilizochovywa Chocolate cream ml 480
Badala ya biskuti zilizochovywa na chocolate cream unaweza weka vipande vya chocolate, unaweza weka mchanganyiko wa ladha mabalimabli mfano matunda kama strawbery, cherry, Embe kwa kuchanganya kiasi cha ml 480 kama inavyoonyehs hapo juu katika mtiririko wa vitu vya kuandaa.
Vunja vunja vipande vya biscuti vilivyochovywa na chocolate weka pembeni safi ukisubiri baadae kidogo kuzitumia.
Weka maziwa katika sufuria nzito kwenye jiko lenye moto wa wastan acha yachemke pole pole mpaka yatakapotoa mapovu pemebi ya sufuria yatoe na weka pembeni yapoe.
Baada ya kutoa maziwa katika moto na kuyaweka pembeni yapoe changanya sukari na chumvi ndani yake
Koroga vizuri maziwa hayo mpaka sukari na chumvi viyeyuke vizuri
Changanya tena whiping cream na vanillah kwenye maziwa yale pole pole kisha changanya maziwa na ile cream vilivybaki ambavyo vyote vinamafuta kiasi ( low fat ) mpaka ichanganyike vizuri.
Kisha mimina mchanganyiko wako wote kwenye bakuli safi la kioo ili uweze kupoa na kuganda
Baada ya kumimina katika bakuli chukua bakuli jingine kubwa kiasi ya lile lenye mchanganyiko wako kwajili ya kugandisha kua ice cream. Weka barafu katika bakuli hilo kisha weka juu yake bakuli lenye mchanganyiko wako. Baada ya mchanganyiko wako kupoa kabisa chukua plastic wrap funika bakuli lako vizuri na weka katika friji kwa masaa 4 au hata masaa 24 kwa kuweka mchanganyijo wako ndani ya friji itasaidia sana kubadilisha mchanganyiko kua rojo rojo au mzito na inakua rahisi kukoroga tena ili upate umbile halisi la ice cream na laini kwa mlaji.
Baada ya masaa 4 au masaa 24 toa mchanganyiko wako kwenye friji kisha koroga vizuri na mwikosafi wa mbao au kijiko kikubwa.
Kisha funika tena na plastic wrap au foil kitu chochote kitakachozui hewa kuingia katika bakuli lako tayari kwa kugandisha kwenye freezer. Baada ya hapo weka bakuli lako katika freezer na ruhusu mchanganyiko wako ukae kwa masaa 2 kwenye freezer kisha utoe.
Baada ya kutoa mchanganyiko wako katika freezer tumia mashine ya kuchapia au unaweza tumia mchapo wa chuma au unaweza tumia uma ya kulia chakula na kukoroga vizuri mchanganyiko amabao utakua tayari umeshaanza kuganda lengo ni kuvunjavunja mapande ambayo yameshaanza kuganda. Kisha funika na plastic wraptena na rudisha katika freezer kwa masaa 2.
Baada ya masaa 2 toa mchanganyiko wako na koroga kwa kutumia mashine au uma yakulia chakula. Ice cream yako itakua nzito safi lakini bado kwa kuweza kuchota na kuliwa, kama mchanganyiko bado haujaganda vizuri kutokana na nguvu ya freezer rudisha kwenye freezer igande tena kwa muda kiasi.
Baada ya ice cream yako kua imeganda vizuri chukua zile bisckuti zenye chocolate tupia katika mchanganyiko wako wa ice cream na uchanganye vizuri sana kwa umakini, aidha inaweza kua ni matunda ya ladha yeyote badala ya biskuti bado itapendeza na utakua umebadilisha ladha.
Kisha chukua chombo cha plastic kisafi na kikavu, weka mchanganyiko wako ndani yake na hakikisha unaacha nafasi ya inchi 1 au 1/2 inchi kwajili ya kutanuka.
Kisha funika vizuri plastic yako na mfuniko safi na uirudishe katika freezer iweze kuganda kabisa mpaka itakapokua ngumu.
Baada ya ice cream kua ngumu toa kwenye freezer fungua chombo chako cha plastik na tumia chombo maalumu cha kuchotea ice cream vipo vingi sana hapa nyumbani tanzania vinauzwa kwenye supermaket. Chota maumbo mazuri sana ya mviringo kisha weka kwenye bakuli au glasi ya udongo na ufurahie ice cream yako!!
NATUMAI MPAKA HAPO MTAKUA MMEELEWA VIZURI SANA SOMO HILI LA LEO NA KUWEZA KUTENGENEZA ICE CREAM SAFI KABISA WATOTO, BABA AU MGENI AKAFURAIA SANA CHAKULA HIKI CHEPESI.
NAOMBA MTENGENEZE KWAKUFATA MAELEKEZO VIZURI HALAFU MNIPATIE MATOKEA KISHA TUENDELEE NA SOMO BAADA YA KUTENGENEZA ICE CREAM HIYO UTAIPAMBA VIPI TUTAFANYA UPAMBAJI WA AINA TOFAUTI ZENYE LADHA MBALIMBALI YA ICE CREAM AINA 10 HADI 20.
Thursday, January 7, 2010
SAMAHANI SANA WAPENZI WA BLOG HII
Naomba radhi kwa wapenzi wote wa blog hii kwani nimeshindwa kuweka mafunzo yeyote kuanzia tar 4/1/2010. Nimebanwa na majukumu ya siku 4 tu kwasasa nipo katika chuo uholanzi nimealikwa kama mwalimu mgeni kubadilishana utaalamu na wanafunzi wa chuo cha Horeca en Toerisme kesho kutwa na maliza na naahidi j mosi tar 9/1/2010 nitaendelea na mafunzo na mtegemee mambo mazuri zaidi. nitaleta mafunzo jinsi yakutengeneza ice cream za ladha mbali mbali nyumbani bila kutumia mashine ukiwa na friza tu unaweza tengeneza nyumbani na ni rahisi kabisa na familia wakafurahia sana.
Katika picha hapo juu ni chef Issa na huyo pembeni yangu ndio mkuu wa chuo cha Horeca en Toerisme Uholanzi ndio alienialika kwenda chuoni kwake kufundisha kwa siku 2 lengo ni kubadilishana utaalamu nikiwa kama mwalimu mgeni.
Monday, January 4, 2010
NAKARIBISHA MASWALI NA MAONI MUDA WOTE.
KWA YEYOTE ANAEPENDA KUCHANGIA AU HAJAELEWA VIZURI SEHEMU YEYOTE ILE TAFADHALI TOA MAONI AU ULIZA MASWALI ILI UPATE UFAFANUZI ZAIDI NASHUKURU SANA WOTE MNAOCHANGIA NA MUDA SIO MREFU DARASA LITAANZA RASMI KWA KUZINGATIA MAONI YA WASOMAJI.
DARASA LITAKAU KWA MTINDO WA KUANDAA CHAKUALA KUTOKA KWENYE STARTER HADI DESSERT TUTAANZA NA MILO MITATU HADI MILO SABA INAKUAJE.
WAKATI HUO HUO TUTAKUA TUNAJIFUNZA KUCHONGA NA KUREMBA MBOGA MABLI MBALI.
Thank you so much for all those who buy their time to give very productive comments on my blog, I real appreciate thank you once again. If you find any difficulties to understand recipes in kiswahili and you like the dish picture please just email me on issakesu@gmail.com Soon I will send you the recipe in English.
Chef Issa
DARASA LITAKAU KWA MTINDO WA KUANDAA CHAKUALA KUTOKA KWENYE STARTER HADI DESSERT TUTAANZA NA MILO MITATU HADI MILO SABA INAKUAJE.
WAKATI HUO HUO TUTAKUA TUNAJIFUNZA KUCHONGA NA KUREMBA MBOGA MABLI MBALI.
Thank you so much for all those who buy their time to give very productive comments on my blog, I real appreciate thank you once again. If you find any difficulties to understand recipes in kiswahili and you like the dish picture please just email me on issakesu@gmail.com Soon I will send you the recipe in English.
Chef Issa
JINSI YA KUPIKA MGUU AU KIFUA CHA BATA
Kila mmoja wetu anatambua ulaini na utamu wa nyama ya bata endapo utampika vizuri. Fatilia hapo chini maelezo jinsi ya kukata vipande hivyo vya nyama ya bata na jinsi ya kuitengeneza kwa mtindo safi kabisa, kama ni kwenye mgahawa basi wateja wakula mlo huo watajitokeza kwa wingi na kwa walaji wa nyumbani basi utakua umeongeza chaguo jingine katika ratiba yako ya chakula, pika kifua cha bata acha watu wale kisha muulize kila aliekula hii ni nyama gani utapata majibu mengi sana kuliko utavyotegemea kwa sifa na ubora wa nyama hii.
Huyo ndio bata mzima akiwa ameshachinjwa na kusafishwa vizuri kabisa
Hivyo ni vifua vya bata kwa muonekano wa pande mbili mbele upande wa ngozi na nyuma sehemu yenye nyama tupu bila mfupa.
Huu ni mguu wa bata ukiwa na mfupa na haujatolewa ngozi kwa upande wa pili.
Vitu vta kuandaa ni
Kitunguu swaunu 1 kisage vizuri
Kitunguu maji 1 kata vidogodogo sana
Chumvi na pilipili manga
Maji 100gr
Juisi ya chungwa 1
Asali ya nyuki vijiko 4 vikubwa vya chakula
Bay leaf 1
Oregano kijiko nusu kidogo
Rosemary kijiko nusu kidogo
Mafuta ya maji yakupikia 150ml
Zabibu kavu 150 gr
Kama inavyoonysha katika mtiririko wa kuandaa vitu vya kupika pamoja na bata wako nimesema mafuta ya maji ya kupikia tumia yeyote kulingana na uwezo wako
Chukua vitu vyote ulivyoandaa hapo juu weka katika bakuli kama unavyoona katika picha changanya kwa pamoja vyote.
Kisha weka nyama kwenye chocmbo kitakachotosha vizuri halafu mwagia juu ya nyama ya bata mbichi ule mchanganyiko wako safi usambaze kote.
Weka nyama yako ndani ya friji lenye nyuzi joto 4 hadi 5 kwa masaa mawili kuruhusu ule mchanganyiko wako uingie vizuri katika nyama.
kama hauna friji usiweke kwenye friza acha nje sehemu yenye hewa safi na sio joto kwa muda wa saa 1 ukiwa umefunika ili wadudu wasiingie.
Baada ya muda huo kupita chukua nyama yako ya bata weka katika kikaango chenye mafuta kiasi na moto wa wastani kaanga pande zote mbili pole pole na nyama itaiva vizuri sana ikiwa na ladha safi.
Ule mchanganyiko wako wa mwanzo wa viungo uliomuunga bata wako kabla ya kupika usitupe hifadhi pembeni kwajili ya kutengeneza mchuzi wa kula pamoja na nyama hiyo ya bata.
Kwa wale wasio penda mafuta unaweza choma nyama hiyo katika jiko la mkaa lenye moto wa wastani ili nyama hii iive taratibu isibabuke kama unavyoona hapo chini katika picha.
Hapo chini ni muonekano wa nyama ya bata ikiwa imeshaiva na kukatwa slice za wastani bila kuachanisha kifua hicho ili kisipoteze muonekano wake halisi.
Hapo chini ni muonekano wa ule mchanganyiko uliotumia kumuunga bata akiwa mbichi kabla ya kumpika.
Chukua mchanganyiko huo wote weka katika sufuria au kikaango, washia jiko moto wa wastani ili mchuzi huo uive pole pole pia ongezea na glass moja ya mvinyo mwekundu au ( Redwine).
Hapo chini ni chupa na kipimo ambacho ni glasi halisi ya wine
Red wine italeta harufu na ladha nzuri sana kwa wale wasiotumia pombe wawe na amani kwani pombe yote inabadilika kua mvuke na kuisha kabisa kinachobaki ni harufu nzuri na ladha ya zabibu iliyovundikwa.
Ikishakua nzito tafadhali toa katika jiko tayari kwa kusave sauce hii unamwagia juu ya bata au unaweka katika chombo kidogo unasave pamoja na nyama hiyo ya bata mlaji atajipimia kiasi cha sauce anachopenda.
Muonekano wa upangaji sahani hapo chini hii yote ni kumvutia zaidi mlaji na kukifanya chakula chako kionekane safi na salama.
Nyama hii ya bata unaweza savu na ugali, wali, viazi hata mihogo ya kuchemsha vyovyote upendavyo na utafurahia zaidi ikiwa umefata maelezo vizuri ya uandaaji.
Naimani mtakua mmefurahia sana mapishi haya ya nyama ya Bata. Ukifatilia toka mwanzo nimekua nagusia vyakula ambavyo watu wengi hawapendi sana kula aidha kwakukosa umaarufu au kwa kutokufahamu njia mbada ya kukipika ili kipendeze na kiweze kulika.
Tengeneza bata huyu na usimueleze mlaji kisha baada ya mlaji kula muulize anahisi nyama hii ni nyama gani? kuanzia hapo yule asiye mpenzi wa kula bata atakua mwanachama mzuri sana mama nyumbani unakua umeongeza idadi ya mabadiliko ya chakula nyumbani.
Kuna mdau alieuliza oregano ni nini? hapo chini ni picha ya spice inayoitwa oregano zinapatikana sana kila duka la chakula hapo nyumbani Tanzania na uliza kwa jina hilo hilo supermaket yeyote ile utapata natumai utakua umeifahamu na kwenda kuinunua na ni nafuu bei yake.

Mdau ulie uliza mbadala wa Redwine kwaruza ganda la limao au chungwa upate zile chenga chenga kijiko kimoja cha chai then weka katika mchanganyiko wako utapata harufu safi na ladha nzuri sana.
Sunday, January 3, 2010
APPETIZER OR FINGER FOOD
FISH TERRINE
Mshangaze mgeni wako nyumbani siku utakapomualika kwa chakula cha mchana au usiku kwa kumpatia terrine hii safi kabisa ya samaki wakati akisubiri mlo kamili.
Chukua fileti ya samaki weka katika ubao iponde vizuri pole pole mpaka iwe bapa kama inavyoonekana katika picha.
Chukua fileti kiasi ya samaki kata vipande vidogo vidogo na ichemshe na limao kidogo kwenye maji ya wastani iive kisha chuja acha samaki peke yake weka pembeni ipoe na ule mchuzi weka pembeni upoe pia.
Kisha chukua zucchin ikate kwa urefu slice nyembamba sana kata nyingi zakutosha inategemea na ukubwa wa chombo utakachotumia kutengenezea terrine yako.
Chukua chombo ambacho ungependa kutengenezea terrine yako chenye mtindo wowote ule kama ni cha mviringo au mraba au pembe tatu kama hicho hapo juu, Kinaweza kua cha chuma au plastik inayostahimili moto.
Tanguliza clinfilm kwenye chombo chako, kisha panga slice za zucchin kwa kuzipandanisha kiasi usiache nafasi.
Baada ya hapo panga fileti ya samaki mbichi ambayo imeshapondwa ikawa flat kabisa.
Katika picha tunaona samaki iliyochemshwa katika kikaango ute mweupe wa yai na ute wa njao wa yai
Samaki iliyochemshwa imechanganywa na majani aina dill yamekatwa katwa vizuri yakawa madogo kabisa
Baada ya kuweka dill fresh ongezea ute wa yai mweupe ( mayai matatu yanatosha kwa samaki gramu 500) pamoja na cream mililita 200.
Weka chumvi na pili pili manga ilivichanganyike vizuri.
Weka katika mashine ya kusagia saga mchanganyiko wako mpaka uwe mzito kabisa sio kimiminika, kama hua mashine basi unaweza tumia mwiko kuponda mpaka mchanganyiko wako uwe mzito na safi.
Mchanganyiko wako uko safi kabisa kama unavyoonekana hapo katika picha ni mzito na umekamilika.
Kumbuka fileti yetu ya samaki ni rangi nyeupe ili tupendezeshe na kupata mchanganyiko safi wa rangi chukua safron ya njano weka katika mchanganyiko wako wa samaki.
Kisha chukua mchanganyiko wako wa samaki na uweke katika chombo ulichokiandaa kwajili ya terrine yako safi.
Kama unavyoona katika picha slice za zucchin na fileti ya samaki vimezidi katika chombo chetu cha terrine tutaona faida yake hapo chini.
Ukishamaliza weka mchanganyiko wako wa samaki ukatosha vizuri kabisa.
Chukua zile zucchin zilizozidi pamoja na fileti ya samaki funika kwa juu tayari utakua umeshapata umbo kamili la pembe tatu napia usisahau kufunika na ile clingfilm juu ya chombo chako cha kupikia terrine.
Pika kwenye stimer kwa dakika 30 hadi 45 kisaha itoe itakua imeshaiva vizuri na kua ngumu kabisa tayari kwa kuliwa.
Kama hauna stimer basi unaweza tumia sufuria weka chombo chako cha terine kisha weka maji katika sufuria yasizidi kile chombo chako cha kupikia terrine yawe nusu tu kisha chemsha kwa muda huo huo kumbuka kufunika sufuria yako wakati wa kuchemsha.
Baada ya kutoa katika stimmer weka pembeni terrine yako ipoe.
Ikishapoa toa katika chombo na iweke katika ubao wa kukatia muonekano utakua kama hapo juu unavyooona terrine yetu ipo tayari matumizi ya chakula.
Wakati wa kukata posheni unafata mikato ya zucchini ndio posheni moja kwa mlaji mmoja tu. pia unaona muonekano mzuri wa rangi 3 yeupe, kijani na najano.
Terrine hii ikishapoa unaweza ihifadhi katika friji kwenye ubaridi wa nyuzi joto 4 hadi 5 ikisubiri kuliwa pia inaweza kaa mwezi mzima bila kuharibika.
Wakati wa kusevu baada ya kukata posheni yako weka katika kisahani kidogo cha kikombe cha chai ili kiendane na ukubwa wa terrine yako.
Kumbuka mwanzo tuliweka pembeni ule mchuzi wa samaki, uchemshe changanya na cream, safroni ya njano, chumvi na pilipili manga pika kwa moto mdogo mapaka mchuzi huu uwe mzito kabisa.
Mwagia mchuzi huo juu kila unapo save terrine hii na unaweza pamba juu ya terrine hiyo na kitu chochote kile upendacho. Juu ya terrine hiyo nimepamba na vitunguu vya kukaanga vinasaidia kuleta harufu nzuri.
KUMBUKA KUA HUO SIO MLO KAMILI BALI NI KITIA HAMU WAKATI UNASUBIRI MLO KAMILI. RECIPE HIYO HIYO UNAWEZA TUMIA KWA KUTENGENEZA TERRINE YA KUKU AU NG'OMBE NA IKAPENDEZA SANA SANA.

Haya ndio majani aina ya dill,
Mdau alieuliza ule ute wa njano ule hauna kazi tena.
Kutengeneza slice za zucchin pia unaweza tumia kifaa kile cha kumenyea karoti au viazi utapata slice nzuri tu natumai wadau hapa nitakua nimejibu maswali yenu vizuri kabisa.
Subscribe to:
Posts (Atom)


























