CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Wednesday, February 24, 2010

JINSI YAKUPIKA KEKI YA ZABIBU KAVU



Tengeneza keki ya zabibu kavu kisha ongezea ladha mbali mbali kutokana na upendavyo fata maelekezo hapo chini


Mahitaji:


240gram zabibu kavu

240garm maziwa ya maji

240garm siagi (butter)

½ chumvi kijiko kidogo cha chai

240gram sukari

240gram korosho au walnuts au karanga chochote ulichonacho

500gram unga wa ngano

1 kijiko kidogo cha chai baking soda (Baking powder)

2 mayai



JINSI YAKUTENGENEZA

Washa oveni yako katika joto 325 degree F (165 degree C) kisha kipake chombo chako siagi utakacho tumia kuokea keki yako.

Chukua bakuli changanya unga wa ngano, zabibu na baking soda kasha weka pembeni.

Chukua bakuli nyingine weka siagi na sukari ndani kisha piga mapaka ichanyanyike vizuri na kua laini kabisa kisha vunjia mayai ndani piga paka mchanganyiko wako uwe laini kabisa.

Kisha chukka mchanganyiko wa unga mimina kwenye mchanganyiko wa mayai changanya pole pole mpaka upate mchanganyiko mzito wa wastani kama itakua nzito sana ongeza maziwa kama itakua nyepesi sana ongeza unga.

Kwa kuongeza ladha unaweza kuongezea vitu hiyo hapo chini.

½ kijiko kidogo cha chai kungu manga ya unga (nutmeg)

½ kijiko kidogo cha chai Mdalasini ya unga (cinnamon)

1 kijiko kidogo cha chai vanilla ya maji

Kisha mimina mchanganyiko wako wa keki kwenye chombo utakachotumia kuokea na oka kwa dakika 40 hadi 45 kwa moto ule ulioelekezwa pale juu kama oven yako inamoto mkali zaidi unaweza choma kwa dakika 30 ila hatari ya kuunguza na keki isiive kati kati ni kubwa sana.

Baada ya dakika 40 chukua toothpick choma keki yako katikati toa angalia kama itakua kavu basi keki yako imeiva kama itakua na maji maji keki yaki bado haijaiva hivyo iache katika oven kwa muda kidogo kisha angalia tena.

Toa keki yako iache ipoe tayari kwa kuliwa.



 

5 comments:

Anonymous said...

Heheheh tupe vitu kaka.
Yani kina sisi wa mahanjumati umetufikisha. Kila la kheri.


disminder

shamim a.k.a Zeze said...

Shukran saaana chef Issa

nitakuletea picha soon

Anonymous said...

Thanks Chef! Siagi ni 2400 gram au 240 gram?

test said...

chef issa!,

natumai mzima wa afya, mimi ni mfuatliaji mnzuri sana wa blog yako kwa sbb napenda kupika sana tu bu profesional ni adminstrative, naomba nipe tofauti kati ya baking soda na baking powder kwanu huku tanzania tumezoea sana baking powder

Anonymous said...

haya ndo mambo yangu aswaaa,naenda pika na nitakuja apa na majibu

mbona asanteeee?