CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Friday, June 18, 2010

JITAIDI KUA MBUNIFU KATIKA KUPAMBA CHAKULA CHAKO



UBUNIFU WA KUPAMBA CHAKULA KATIKA MUONEKANO WA KIPEKEE INASAIDIA SANA KUONGEZA HAMASA KWA MLAJI HATA KAMA CHAKULA HAKIKUA NA LADHA SAFI MLAJI ANARIDHIKA KWANZA KABLA YA KUKIONJA



Huu ni muonekano wa bata wa kuchonga kwa kutumia tunda nanasi safi sana pamba mezani na mwisho wa chakula unaweza kula kama kikata hamu na familia yako


Ni rahisi sana jinsi ya kuchonga katika muonekano huu


Hii ni keki nzuri kabisa ya vanilla cream na karanga


Pamba vizuri sahani zako hata kama unawageni 100 uhuru wa kila mtu kula kwa sahani yake ikiwa imepambwa inapendeza sana sana


Kata matunda na panga sahani kubwa kwa mtindo huu ikiwa unafamilia kubwa au unawageni nyumbani kila mmoja atachukua aina ya tunda analopenda kutokana na mvuto wa mpangilio


Si kazi ngumu kukata na kupamba sahani ya matunda hakuna kizuri kisicho na juhudi kikubwa ni wewe kupenda kuhudumia chakula chenye muonekano thabiti.

WASANGAZE FAMILIA YAKO KWA KUPAMBA SAFI CHAKULA CHAKO NAWATAKIA WEEKEND NJEMA




4 comments:

Disminder orig baby said...

KWA UREMBO HUO? NTANG'ATWA MIMI KABLA YA CHAKULA.

INAPENDEZA SANA KAKA

Anonymous said...

uko juu kaka!

Anonymous said...

hongera kaka kwa uhodari wa ubunifu kipaji unacho. safi sana!!!!!

Anonymous said...

wee kiboko

nakuombea dua ufike mbali sana kimataifa kwa ujuzi wako ktk mapishi