CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Friday, September 24, 2010

TAARIFA RASMI KWA WAPENZI WOTE WA BLOG

KWA WALE WAPENZI WA DONUT SAMAHANI SANA NILIKOSEA VIPIMO NA NIMESHAREKEBISHA SASA MNAWEZA KUANGALIA UPYA RECIPE NA KUTENGENEZA KWA KUTUMIA RECIPE HIYO KWANI KIPIMO CHA MAZIWA KILIZIDI HII ITAKUA NZURI NA MTAFURAHIA NAOMBA MATOKEO BAADA YA KUTENGENEZA. KWA WASOMI WAPYA WA BLOG HII FUNGUA UPANDE WA KULIA SEHEMU ILIYOANDIKWA MAFUNZO YALIYOPITA UTAIONA.

POLENI SANA WAPENZI WA BLOG HII MLIOTUMA EMAIL KWANGU ILI NIWEZE KUWATUMIA RATIBA NA JINSI YA KUANDAA TAKE AWAY YA WATOTO!

NILIAGIZA BEI ZA VYAKULA DAR ES SALAAM ZIMECHELEWA KUFIKA NATARAJIA KESHO NITAPATA ILI NIFANYIE MAHESABU ILI NIWAONYESHE KILA CHAKULA UTAKACHOTENGENEZA KITAGHARIMU KIASI GANI.

 KISHA NITAWATUMIA SIKU YA JUMA TATU TAR 27.

 NAONA BEI ZA VYAKULA HAZIPISHANI SANA DUNIANA\I KAMA UKIONA MCHELE DOLA1 ULAYA BASI UNAKUA UNAUZWA SH 1300 HADI 1500 TANZANIA.

PILI WALE WOTE MNAOPATA SHIDA KATIKA VIPIMO PIA MTANIANDIKIA EMAIL JUMATATU NIWEZE KUWATUMIA KARATASI  INAYO ONYESHA VIPIMO VYOTE ITAKUA KAZI KWENU MCHAGUE KUTUMIA VIPIMO GANI KIKOMBE, KIJIKO, GRAM AU LITER.
KARATASI HII INATAFSIRI VIPIMO VYOTE TOKA KIMOJA KWENDA KINGINE.

PIA BADO NASUBIRI SANA PICHA ZA VYAKULA MNAVYOTENGENEZA NAHAMU SANA KUONA MAENDELEO YETU TAFADHALI AU KAMA UNA RECIPE YEYOTE ILE UNGEPENDA WATU WAJIFUNZE TOKA KWAKO WE NITUMIE TU KATIKA EMAIL YANGU NI issakesu@gmail.com.

NAWATAKIA KAZI NA SIKU NJEMA

CHEF ISSA



4 comments:

Majoy said...

Asante sana Chef u r so kind be blessed!

Anonymous said...

Asante Kaka Issa, mie nilishajaribu kupika kuku wa Ufuta, Kuku wa nazi, Nyama ya mbuzi. My family really enjoyed it. Unfortunately sikupiga picha. Next time I do it, nitafanya hivyo.
Otherwise Mungu akubariki for the recipes, u know life is too short..so we have to make sure we enjoy every minute of it..that includes the meals we take
God Bless

Anonymous said...

m mungu akuzidishie wala si mchoyo unatuelekeza vizuri na unataka kujua tunachofanya umekamia kweli tuwe wapishi wazuri. basi tutapica picha tukukeltee halahala usicheke tu napenda kujaribu kupika.

ila saa zengine mbona hujibu mawali jamani
nilijaribu kupiga ile keki ya kukunja na kuweka jam na castard katikati haikukubali ikavunjika nilikusea nini

Anonymous said...

Aic kaka issa we ni mkali,mi nilijaribu kupika maandazi,yalikuwa mazuri sana,mana mwanzo nilikuwa najipikia tuuuuu,ubarikiwe sana...tufundishe jinsi ya kutumia oven za majiko ya mkaa ili nasi tusokuwa na uwezo tupate kuenjoy keki siku mojamoja kaka,athanteeeeeeeeeeee...inshort,familia yako lazima inaenjoy sana kuwa na baba kama wewe...