CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Friday, August 26, 2011

JIFUNZE KUTENGENEZA KEKI HII SAFI KABISA YA MCHANGANYIKO WA NAFAKA


KAA TAYARI KWA KUJIFUNZA KUTENGENEZA KEKI HII SAFI KABISA NA RAHISI PIA HATUA KWA HATUA JINSI YA KUPAMBA KEKI

MAHITAJI

Mchanganyiko kwajili ya Cake

720 gram unga wa ngano
1 kijiko kidogo cha chai Baking powder
1 kijiko kidogo cha chai chumvi
360 gram sukari
1 kijiko kidogo cha chai  unga wa Cinnamon
4 mayai vunja na ubakize ute mweupe tu
180 gram ndizi ya kuiva iponde ponde
120 gram Vegetable Oil
480 gram ndzi mbivu kata kata vipande
1 kijiko kidogo cha chai Vanilla Essence
120 gram kata kata vipande vya nanasi
240 gram vunja vunja koroshon za kuokwa

Mchanganyiko kwajili ya Cream Cheese

1 lita ya light Cream Cheese isiyo na mafuta
120 gram  Butter au margarine
1 kilo Icing Sugar
1 kijiko kidogo cha chai Vanilla Essence
120 gram chopped koroso za kuokwa katika oven

JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAEELEZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi : saa 1 mpaka 2

Muda wa kupika : dakika 30 mpaka saa 1
Idadi ya walaji : 8 na zaidi
Katika bakuli changanya unga wa ngano, chumvi, sukari, baking powder na unga wa mdalasini ( cinamon)Changanya vizuri mpaka vichanganyike kabisa

 

Chukua bakuli kisha piga ute mweupe wa yai na uchanganye na mafuta, vanilla pamoja na ndizi ya kuiva ulio iponda ponda kisha mimina mchanganyiko huu katika unga wako.Tumia mwiko kuchanganya mchanganyiko huu pole pole mpaka uchanganyike.Huu ni muonekano safi kabisa unga wako umechanganyika vizuri kwa kutumia mwiko.Baada ya hapo weka vipande vya nanasi ulivyo kata kata, 240 gram ya korosho zilizookwa pamoja na vipande vya ndizi mbivu.Endelea kuchanganya kwa kutumia mwiko mpaka upate mchanganyiko safi kabisa.Chukua vyombo vya kuokea keki vyenye vya mduara na kina cha 9-inch  kisha mimina mchanganyiko wako sawa kwa sawa katika vyombo vyote vitatu.Coma keki yako katika moto wa 350° kwadakika 25 mpaka 30 inategemea na oven yako pia unaweza choma mpaka ukiweka katika keki tooth pick na inatoka kavu. Poza keki zako katika wire racks kwadakika 10; kisha toka katika pans ilizo chomea, na kisha ziache zipoe moja kwa moja katika wire racks.Kwajili ya kupambia: Piga cream cheese pamoja na  butter kwa speed ndogo kwama unatumia mashine ya umeme mpaka ilainike kabisa.Pole pole na kidogo kidogo mimina icing sugar,endelea kupiga kwa speed ndogo mpaka iwe nyepesi na inapandaKisha ongezea vanilla.Paka mchanganyiko wako wa Cream Cheese katika kila keki yako kwa upande wa juu tuKisha zipandanishe na juu kabisa paka tena kama ionekanavyo katika pichaKisha paka na pembeni ya keki pia kama picha inavyoonyesha iwe rafu rafu tuKisha mwagia juu ya keki yako 120 gram cup za korosho zilizookwa na ukazikata kata.


Kisha iweke keki yako katika friji. Ladha ya ndizi mbivu na nanasi pamoja na korosho inafanya keki hii iwe na ladha ya kipekee na ukiila mara moja utatamani kula kila siku!Huu ni muonekano wa keki ikikatwa kwa ndani unaona mpangiliona muonekano wake  ulivyosafi?KEKI HII NI SAFI, RAHISI KUANDAA NA TAMU SANA WAFURAHISHE FAMILIA YAKO NA MAPISHI SAFI YA KEKI HII.

8 comments:

Anonymous said...

KAKA ASANTE KWA KUTUONYESHA JINSI YA KUTENGENEZA HIYO KEKI ILA NN?
MAELEZO HAKUNA YAAN IMEKUA ZIRO MKALI. KM HATUJAKUSOMA HV.

Anonymous said...

kaka Issa tupe na recipe basi! tuandikie mahitaji yote tafadhali

Anonymous said...

Habari,
naomba tafazali uandike recipe ya hii keki-imenitamanisha ningependa kuijaribu. .
Asante

Anonymous said...

jamani weka recipe basi

Colleta said...

Chef, yaaani keki imenvutia saaana, ttzo ni hujaeka maelezo. Pliiiiz, work on iiiiit!

Anonymous said...

Can't wait for this recipe please post the ingredients and procedures, thanks

Anonymous said...

maelezo kaka etu

Anonymous said...

its a very nice cake, but wud u plse write recipe as well to all ur pictures, bse its really hard to understand.