CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Sunday, April 15, 2012

JIFUNZE KUPIKA WALI WA SAUSAGE NA MBOGA MAJANI MCHANGANYIKO


JIFUNZE KUPIKA MBOGA MAJANI NA MCHANGAKO WA WALI NA SAUSAGE
MAHITAJI

3 vipande vya sausage
1 fungu la majani ya vitunguu
1 kitunguu kikubwa
100 gram njegere
500 gram chele basmati
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
JINSI YA KUANDAA FATIKLIA PICHA NA MAELEZO

Muda wa mapishi dakika 45
Muda wa maandalizii dakika 15

 

Huu ndio muonekano wa majani machanga ya vitunguu


Kaanga vitunguu maji katika kikaango kwa kuweka mafuta ya kupikia kiasi


Kisha ongezea majani mabichi ya vitunguu kama inavyoonekana katika picha


Baada ya kukaanga kwa dakika mbili vitunguu pamoja na majani vitoe tu harufu na sio kuungua kubadilika rangi kisha weka mchele na endelea kukaanga


Kaanga mchele kwa dakika 3 mpaka 4 kisha weka maji ya wastani yazidi mchele wako kiasi na uendelee kukoroga ili maji yachanganyike na mchele wako


Kisha funikia na weka moto wa wastani ili wali wako uive taratibu


Kisha chukua sausage zako na kata kata vipande vidogo


Huu ndio muonekano wa vipande vya sausage baada ya kukata


Kisha tupia juu ya wali wako njegere zilizochemshwa pamoja na vipande vyoote vya sausage


Kumbuka kuendelea kukoroga ili kila kitu kichanganyike, pia kama mpenzi wa blue band au samli unaweza weka kiasi ili kuongeza ladha na harufu safiu sana katika wali wako


Safi sana hapa kila kitu kimechanganyika na ninaimani baada ya dakika 45 wakli wako utakua umiva kama haujaiva basi ongezea maji kidogo na endelea kupika katika moto mdogo


Ukimaliza pakua na mpatie mlaji chakula hiki kikiwa chamoto



waandalie famili au hotelini kila atakae kula atafurahia sana

9 comments:

Anonymous said...

sasa ndugu yangu hujatoa maelekezo kuhusu upishi huo,mi naona vitu kwenye sahani lakini vingine hata sielewe nadhani ungekuwa unaelezea kidogo

Anonymous said...

kaka habari?

mapishi yako yote unasema "FUATILIA PICHA NA MAELEZO"

Ila maelezo hakuna yaani hatuyaoni,
ina maana yanapeperuka au hutaki kuyaweka????



mdau wako mwanza

Anonymous said...

hongera sana kaka kwa kazi nzuri kweli wewe si mchoyo wa elimu. Nina mradi nataka kufanya hapa nyumbani tanzania ni mdogo tu nilipenda sana tuwasiliane kwa e-mail unishauri. asante

Anonymous said...

hello chef, pliz rusha na recipe ya mapishi mbali mbali ya nyama, kuku, utumbo na mbuzi. thanx

Anonymous said...

kaka weka maelezo tunapenda nasi kujua kila hatua,,,asante mdau Morogoro

Anonymous said...

jamani hakuna maelezo?au baada ya muda ndo utaweka?

Anonymous said...

Picha zinaeleweka lakini maelezo kushney sasa wengine bila maneno hakuna kinachoeleweka.

Jiang said...

Sijaja jamvini siku nyingi sana Chef, na hii imenivutia, wikend hii ndefu naenda kuijaribu. Ntakupa majibu, thankx.

Anonymous said...

jiang uko adi uku?safi sana mwanamke pishi mwezangu,chef ananifurahisha sana sana hajui tu jinsi alivotuboreshea mapishi yetu majumbani mwetu walahi