CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Monday, November 12, 2012

JIFUNZE KUTENGENEZA JUISI YA KAROTI NANASI NA TANGAWIZI

 
JIFUNZE KUTENGENEZA JUISI SAFI KABISA YA NANASI TANGAWIZI NA KAROTI NI RAHISI SANA NA PIA INAONGEZA SANA HAMU YA KULA KWA MTOTO AU MTU MZIMA AKIWA AMEPOTEZA HAMU YA KULA.
 
MAHITAJI
 

1 450 grams au nanasi 1 kubwa
50 gramsTangawizi osha na menya
1 Carrot ya wastani osha menya katakata vipande vidogo
5pc Ice cubes 
 
FATILIA MAFUNZO NA JINSI YA KUANDAA KATIKA PICHA HAPO CHINI

Muda wa maandalizi : Dakika 15
Muda wa mapishi : Dakika 15
Idadi ya walaji : Watu 2
 
 
Huu ni muonekano wa vyakula vyako

 
Menya nanasi kisha toa ile sehemu ngumu ya kati kisha kata kata vipande vidogo.

 
Baada ya kukata kata nanasi vipande vidogo kisha kata karoti na tangawizi na weka katka bleda au  (or juicer).

 

Saga vizuri ilainike na kisha chuja kwa chujio.

 
Chuka vipande vya barafu na weka katika bakuli safi ulilochuja ili ipoe na uweze mpatia mnywaji.

 
WATENGENEZEE FAMILIA WAFURAHIE KINYWAJI HIKI SAFI WAKATI HUU WA JOTO KALI SANA NA HASA KWA WALE WAVIVU WA KUNYWA MAJI HII NI NJIA MOJA WAPO YA KUZOEA NA KUJIFUNZA KUNYWA MAJI
 


2 comments:

Anonymous said...

ASANTE SANA CHEF UMENIPA NAMNA YA KULIPENDA NANASI KWA JINSI HII YA JUICE,ME SIPENDI KABISA NANASI KULILA MENGI YANAKUA MACHACHU SANA

Anonymous said...

Aisee very simple, gonna try it tonight, thanks Issa.