RECIPE SAFI KABISA YA KITAFUNWA HIKI CHENYE MCHANGANYIKO WA UNGA WA MAHINDI NA MAJANI YA KITUNGUU
MAHITAJI
120 gram unga wa ngano
120 gram unga wa mahindi wa njano
1/4 kijiko kidogo cha chai Baking Soda
1 pc yai
120 gram maziwa
60 gram majani ya vitunguu maji
1 pili pili hoho
5 gram chumvi
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
Pasha mafuta katika kikaango kwajili ya kukaangia. Kisha changanya unga wa ngano, unga wa mahindi, chumvi na baking soda.
Chukua bakuli safi, Changanya vizuri maziwa na mayai mpaka ichanganyike vizuri kabisa.
Kisha mwagia mchanganyiko wako wa maziwa kwenye mchanganyiko wa unga na changanya vizuri kabisa.
Mimi huwa natumia icecream scoop wewe unaweza tumia pia ua ukatumia kijiko
Kisha chota tupia katika mafuta yamoto na uendelee kukaanga.
Kumbuka kugeuza geuza wakati zinaendelea kuiva.
Kumbuka kuweka moto wa kati ili mafuta yasiwe yamoto sana zitababuka na zisiive vizuri au mafuta yakiwa sio yamoto safi itasababisha zisiive na ziwe chini ya kiwango.
Ukitoa katika mafuta zikaushe katika towel zichuje mafuta.
Enjoy zikiwa zamoto na ndio zinakua bado hazijapoa na fresh.
Pata kitafunwa hiki kwa chai ya saa 4 asubuhi au chai ya saa 10 jioni safi sana.
3 comments:
kaka issa nimependa kitafunwa ila sasa naona kama umeweka na mayai pia,utuelekeze jinsi ya kuandaa kaka issa
asante sana kwa kutulahisishia mapishi ya vitu vidogo km ivi yet ni muhimu sana katika familia.
so unga wa mahindi wa njano tutaupata super-market??
aza
Dear nashukuru kwa masomo yako mazuri,umeweza kutusaidia kupata ujuzi wa kupika mapishi mbalimbali mpaka familia zinafurahi, Ila nakuomba ukiweza tupe somo la kuandaa meza kwa ajili ya mlo na matumizi ya wine kabla na baada ya mlo, na matumizi ya glass za wine, ninapata changamoto pale unapokuta umewekewa glass 3 na chupa zenye wine 2 na maji ya kunywa issue glass ipi itumike kwa wine kabla ya kuanza kula na ipi ya maji na ipi ya wine baada ya kula, na labda nisaidie aina au majina ya wine kwa ajili ya appetite na zile za kusaidia mmeng'enyo wa chakula
Post a Comment