KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA YA KUAMSHA LADHA KWENYE WALI ULIOPIKWA KISHA UKALALA ( KIPORO)
MAHITAJI
700 gram za wali uliolala ( Kiporo)
2pc kitunguu maji kikubwa
5 pc nyanya za kuiva
1 kijiko kidogo cha chai dengu
1/4 kijiko kidogo cha chai pili pili manga
1/4 kijiko kidogo cha chai Turmeric powder
1 pili pili moja kavu (siolazima)
2 kijiko kidogo cha chai mafuta ya kupikia
1 kijiko kidogo cha chai siagi
Majani ya Curry kiasi
majani ya giligilani kiasi
KUJIFUNZA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
Chukua vitunguu maji 2 vikubwa kwani mimi napenda sana ladha ya kitunguu hivyo unaweza tumia hata kimoja kasha kata kata fine kabisa.
Weka mafuta katika kikaango yapate moto kasha tupia pili pili
KIsha weka kijiko cha dengu.
Endelea kukoroga hakikisha dengu hazi ungui la zinabadilika rangi kiasi kuwa kahawia.
Kisha weka vitunguu maji na chumvi na uendelee kukoroga kwa dakika 2 mpaka 3.
Wakati kitunguu kinaendela kuiva, Kata kata nyanya katika vipande vidogo vidogo. Mimi pianapenda sna ladha ya nyanya hivyo nilitumia pc 5 wewe unaweza tumia sawa au ukapunguza kua 3 au 2 kutokana na unavyopenda.
Ongeza moto kwenye jiko kisha mwagia nyanya ulizokwisha kata kata na uendelee kukoroga.
Weka turmeric au manjano, endelea kupika kwa moto mwingi mpaka nyanya yako iive iwe soft and mushy.
ongezea maji masafi kikombe kidogo kimoja cha chai , na utupie majni ya curry
kisha weka sambar powder na ukoroge ili ichanganyike.
punguza moto uwe wa wastani kisha pika kwa dakika 5 mpaka 7 ukiwa umefunika mfuniko.
Hatua hii inafanya mchuzi wako uwe safi na wenye ladha. sasa hapo ni ruksa kuonja na ukiona nyanya imeleta ladha ya uchachu kisha ongezea sukari kidogo ili kusawazisha ladha kua ya kawaida. Hakikisha mchuzi wako una ladha safi kwani ndio itabeba ladha yooote ya huo wali.
Kisha weka wali uliopikwa au kiporo. Weka kidogo kidogo hakikisha kuna mchuzi wa kutosha wali usizidi.
Hakikisha unakoroga pole pole mpaka wali unachanganyika na kua safi kabisa ila usiwe kavu sana au kua teke teke.
Funika mfuniko na pika katika moto wa wastani kwa dakika 5 hapawali utakopa ladha toka kwenye mchuzi na kua safi kabisa
Zima jiko kisha weka kijiko kimoja cha samli au siagi.
Unaweza ula wali huu pamoja na mtindi, pia rushi majani ya giligilani kwa juu kuongeza ladha na harufu nzuri pia unaweza kula na kachumbali au salad pamoja na parachichi au ndizi mbivu.
No comments:
Post a Comment