CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Tuesday, April 13, 2010

PATA RATIBA SAFI YA CHAKULA CHA WATOTO KWA WIKI NZIMA

BABA NA MWANA WANAKULETEA RATIBA SAFI KABISA YA CHAKULA NA VITAFUNWA KWA WATOTO WENYE UMRI WA MIEZI 9.5 MPAKA MIAKA 6






ANAWASALIMU WATOTO WOTE ANASEMA WAZAZI  JITAIDINI MUWATENGNEZEE WATOTO CHAKULA KIZURI WAWE NA AFYA NA WAFURAHI





Kama umeipenda ratiba hii ya chakula kwajili ya mwanao tuma email kwa issakesu@gmail.com ili nikutumie ratiba maalumu ikiwa kweye ms word uweze kuprint pia nikutumie na maelekezo jinsi ya kuandaa vyakula vyote hivyo kwa urahisi zaidi maelekezo ni mengi hayatatosha hapa katika blog yatachukua ukurasa wote.

Naimani mtaipenda sana na familia zenu watafurahia.



Friday, April 9, 2010

BELGIAN WAFFLE

ASILI YA CHAKULA HIKI NI UBELGIJI NA HULIWA KWA CHAI ASUBUHI AU KAMA KIKATA HAKU YA KULA MCHANA AU USIKU KWA KUONGEZEWA LADHA NA NAKSHI YA MATUNDA AINA TOFAUTI INAPENDEZA SANA.

MAHITAJI
2 mayai
480 gram unga wa ngano 
120 gram mafuta ya mahindi au siagi (butter)
420gram maziwa ya maji
1 sukari kijiko kikubwa cha chakula  
1 kijiko kikubwa cha chakula baking powder
1/4 chumvi kijiko kidogo cha chai

JINSI YA KUANDAA

Washa mashine ya waffle ipate moto

Chukua mayai piga kwa kutumia mchapo mpaka ya lainike na kuweka povu

kisha weka katika mayai mchanganyiko wa vitu vyote vilivyobakia  piga kwa mchapo mpka vichanganyike vizuri kabisa kama mchanganyiko wako ni mwepesi sana jitaidi kuonegza unga kidogo ili uwe mzito.
Weka mafuta ya mahindi au siagi iliyoyeyushwa kati kati ya mashine ya waffle wafuta yatasambaa yenyewe kuzunguka mashine yote ope pole.

kisha mimina katika mashine mchanganyiko wa waffle na choma kwa dakika 5 tu itakua imeiva na kuweka rangi nzuri ya kahawia ila mashine nyingi za siku hizi zinapika kwa dakika 3 tu na ukiiwasha ikawana moto safi inawaka taa nyekundu waffle yako ikiiva ile taa inazima ujue tayari na uitoe.

kumbuka mashine hii inafutwa tu na kitambaa haisafishi kwa maji wala stell wire maana utaharibu ule utando mweusi wa mashine unaosaidia isigandie na iive safi kabisa.




Huu ni muonekano wa waffle mashine na mchanganyiko wa waffle pembeni


Mimina mchanganyiko wa waffle katiakti ya mashine kisha utasambaa wenyewe mashine nzima kumbuka usijaze kabisa maana ina baking powder kumbuka itaingezeka wakati wa kuiva. ukimaliza funika mashine acha waffle yako iive pole pole.



Huu ndi muonekano wa waffle ikiwa imeiva na inarangi safi kabisa ya kahawia
WATENGENEZEE FAMILIA YAKO WAFURAHIE KILA SIKU KWA KUBADILISHA LADHA YA KITAFUNWA BADALA YA CHAPATI NA MAANDAZI KILA SIKU AU MKATE MASHINE HII NI NAFUU SANA MADUKA YA VYOMBO INAUZWA SH 15,000/= TU. NA MNAOSHI UGAIBUNI NENDA DUKA LOLOTE LILE LA VYOMBO VYA NYUMBANI UTAZIPATA KWA URAHISI SANA GHARAMA NI ILE ILE DOLA 15- 20 TU.

BISKUTI BISKUTI


BISKUTI ZA LADHA YA COCOAMACHUNGWA, TANGAWIZI NA VANILLA


Picha hii inaonyesha mahitaji kwajili ya biskuti

3 Mayai
250 gram sukari ya unga / Icing sugar 
750 gram unga wa ngano
1 kijiko kidogo cha chai baking powder
250 gram siagi /  margarine
70 gram cocoa powder
1 Chungwa au limao
1 kijiko kidogo cha chai Tangawizi 




Changanya unga wa ngano, baking powder, sukari ya unga pamoja na siagi



Kisha iponde ponde ichanganyike vizuri kabisa




Baada ya hapo tengeneza shimo katikati kisha vynjia mayani na endlea kuchanganya mpaka upate mchanganyiko safi kabisa



Huu ni muonekano safi wa mchanganyiko safi wa unga wa biskuti ukielekea kukamilika




Kwaruza chungwa mpaka upate vichenga chenga vya ganda la chungwa au unaweza tumia limao



Gawanyisha unga wako uliokwisha kandwa katika pande mbili sawa weka cocoa powder kwenye moja ya unga uliotenga




Kisha uchanganye vizuri kabisa ili ili kokoa yote iingie safi kabisa kwenye mchanganyiko huo wa unga wa biskuit



Huu ni uonekano wa mchangayiko wa unga wa biskuti kila moja lina ladha na muonekano tofauti kwasasa



Anza kusukuma kwanza ulemchanganyiko mweupe kwa upana wa wastaniisiye nyembamba sana biskuti zako zitakakamaa sana 




kisha sukuma ule mchanganyiko wa pili uliobaki wa cocoa uwe na upana sawa na ule mchanganyko mweupe


Kisha zungushia kwenye mpini wa kusukumila ule mchanganyiko wa cocoa ili iwe rahisi kubeba kisha beba weka juu wa mchanganyiko mweupe na kisha zungusha mpini pole pole ili mchanganyiko wako uachie pole pole mpaka mwisho



Kisha sukuma kwa juu ya mchanganyiko mweupe upate usawa mzuri na michanganyiko hiyo miwili ishikane safi kabisa




ukimaliza anzia mwanzo kuja kiasi kisha endelea kuzungusha mpaka umalize mduara wote




Baada ya hapo chukua aluminium foilzungushia kwa juu ifunike safi kabisa kisha weka kwenye freezer kwa masaa 2 itakua imepoa vizuri na imeshikana safi kabisa tayari kwa kukatwa na kuchomwa kwenye oven



Toa mduara wako wa biskuti katika freezer kisha anza kukata upana wowote unaopenda wewe kisha weka kwenye tray na choma kwa dakika 15 - 20 kikubwa angalia biskuti zimekua ngumu na rangi nzuri ya kahawia angalia zisiungue.



HUU NI MUONEKANO SAFI NA THABITI WA BISKUTI YAKO YENYE LADHA ASFI SANA UNAWEZA KUTUMIA KWA CHAI YA JIONI SAA 10 AU SAA 4 ASUBUHI IWE OFISINI NYUMBANI AU HOTELINI.



CHICKEN PYRAMID WITH COCONUT GREEN PEAS

KAA TAYARI KWA MAPISHI HUYU KUKU MTAMU KULIKO KUKU WOTE ANALIWA NA PILAU NA NJEGERE ZA NAZI MHHH YAM YAM!!!



Thursday, April 8, 2010

EGG AND POTATO GNOCCHI

Classic Italian Egg and potato Gnocchi


MAHITAJI

800 gram viazi ulaya
1 yai bichi
200 gram unga wa ngano



Kiazi hiki aina ya desiree ndio bora hasa kwa utengenezaji wa gnocchi il ukikosa unaweza tumia kiazi ulaya chochote ukinunua kiazi kiweke angalau siku 2 ili maji maji yapungue maana kikiwa fresha sana kinakua na maji na yanasababisha gnocchi iwe ngumu na nzito sana pia unaweza ukomba muuzaji sokoni akuuzie viazi ambayo sio fresha san vilivyokaa angalau siku 2 visiwe vya kuoza hahaaahahah!

Chukua viazi vyako vikiwa na maganda vioshe vizuri toa mchanga wote kishs vichemshe katika maji kwa dakika 20 hadi 25 hakikaisha vimeiva kwa kuchoma na uma au toothpick kisha  vitoe vimenye maganda vikiwa bado vyamoto kisha viponde ponge viwe tope kabisa.

Kisha weka unga wako na yai changanya vizuri kama unakanda unga wa mkate au maandazi usitumie muda mwingi utaaribu mchanganyiko wako unatakiwa ukande kiasi tukama bado unamaji maji basi ongeza unga kidofo tu ili ubaki laini usiwe mgumu sana mchanganyiko ukizidi una ukawa mkavu sana gnocchi inakua ngumu n nzito pia ukisha changanyika kata maumbo madogo madogo kama picha zinavyoonyesha hapo chini.



Kata umbo dogo la duara kisha kandamiza na uma ya chakula ili upate mistar mistari inayoweka muonekano mzuri


Weka maji katika sufuri chemsha mpaka yachemke kabisha kisha weka gnocchi zako mbichi zikiiva mara moja zitapanda juu ya maji zitoe na ziweke pembeni zipoe





Huu ni muonekano wa gnocchi zikiwa zimeiva na ziko pembeni zipoe





Kisha weka mafuta kidogo tu katika kikaango kilicho chemka sana ili uzikaange gnocchi kuongeza ladha ya kau kau pia zitabadilika na kua na rangi ya kahawia nzuri. kaanga kwa dakika 2 tu.



Weka kwenye kikaango chenye mafuta yaliyopata moto kisha kaanga


Huu ni muonekano wa gnocchi zilizokwisha kaangwa na kua na rangi nzuri ya kahawia



Huu ni mchanganyiko wa mboga za karoti, kitunguu na pili pili hoho kwajili ya kulia gnocchi



Weka mboga kwenye kikaangao chenye mafuta kiasi yaliochemka kisha kaanga kiasi tu kisha weka mchuzi wa nyanya safia kaanga kwa dakika 3 kisha itakua tayari kumbuka kuweka chumvi





Pakua zile gnocchi zilizokaangwa weka kwenye sahani



Kisha juu yake weka mboga mboga zenye mchuzi safi kabisa wa nyanya


Huu ni muonekano wa gnocchi tayari ikiwa na muonekano safi kabisa wa mchuzi wa nyanya na mboga mboga tayrai kwakuliwa kumbuka kumpa mlaji bado ikiw na moto.





Hii ndio GNOCCHI  yenyewe imeshapambwa na nynya ya kuchoma na jani la parsley inapendeza sana machoni na ladha yake ni safi sana.

Chakual hiki kinaweza kuliwa na mtoto na mtu mzima na wote wakafurahia pia ni rahisi sana kutengeneza.

Tunakaanga kuongeza ubora na kubadilisha ladha lakini unaweza zitoa katika maji baada ya kuchemsha na ukaziwekea mchuzi ukala safi kabisa bila kuzikaanga ili kubadilisha ladha.

Unaweza kula na nyama aina yeyote ile na ukafurahia sana sana.

IJALI FAMILIA YAKO KWA CHAKULA BORA NA SALAMA



BEEF TARTARE

BEEF TARTARE

MAHITAJI

1 kilo nyama ya kusaga
200 gram matango machanga ya kopo ( Ghekins)
100 garm kitunguu maji chochop
50 gram tomato pest
50 gram tomato ketchup
100 gram vinegar ( siki)
50 gram soya sauce
50 gram tabasco sauce
30 gram chumvi
40 gram mafuta ya mahindi
100 gram oyster sauce
200 gram red wine / brand

Changanya mchanganyiko wote kwa pamoja kisha weka katika sahani kwa shepu nzuri kama inavyoonekana kwenye picha  kisha mpatie mlaji ale ilkiwa ya baridi pamoja na mkate wa aina yeyote ule.

Nyama hii uliwa ikiwa mbichi na huambatana na redwine ili isaidie kuipika tumboni ni nzuri sana ila inataka moyo kama hujawahi kuila.


Saturday, April 3, 2010

HIVI NDIO VYAKULA KWAJILI YA PASAKA

PATA MAELEKEZO JINSI YA KUANDAA KUANZIA SUPU, SALAD, MAIN COURSE MAPAKA DESSERT KWAJILI YA PASAKA



Salad ya viazi ulaya, maharage mabichi, kipande cha nyanya, tunda la olive na vipande vya cheddah cheese

Chemsha viazi ulaya visiive sana na maharage mabichi pia chemsha yasiive sana kisha acha yapoe.
chukua viazi na maharage changanya na chumvi kidogo na mafuta ya mahindi kisha weka katika sahani kama inavyoonekana mwagia kidogo balsamic vinega chora mistari miwili kama inavyoonekana katika picha. Mwisho weka juu vipande vya chizi na tunda la olive.



Hii ni classic Italian minestrone soup

100 gram Njegere
1/4 paketi spagheti au noodles
100gram grcarrot
100 gram kitunguu
100 gram leeks
100 gram grzucchini
100 gram cabbage
200 gram Nyanya ya kopo
pili pili manga na chumvi

chukua mafuta ya siagi 150 gram weka katika jiko kisha kaanga mchanganiko wote wa mboga hizo kwa dakika 3 tu kisha nyanya ya kopo kaanga kiasi kisha weka maji wastani mpaka mboga zote zizame katika amji kisha weka spagheti au noodles na chemsha mpaka ziive zikishaiva weka chumvi na pili pilimanga kwa mbali kisha hudumia supu yako ikiw aya moto pia unawez hifadhi katika friji kwa siku 7 hadi mwezi katika freezer kwa matumizi ya baadae.



Hii ni nyama ya sungura na mint sauce

Chukua mguu wa sungura chemsha katika maji na chumvi, kitunguu swaumu na pilipili manga kwa muda wa saa 2nyama itaiva vizuri na kua laini sana.

Toa nyama hiyo kata kata weka katikasahani na kisha chukua mint sauce inauzwa madukani weka lile rojo zito kwenye maji chemsha kwa dakika 5 sauce hiyo itakua safi sana weka juu ya nyama ya sungura au nyama ya kondoo kula na wali na ugali pia.



hii ni chicke pyramid ohhh ni ngumu kiasi kutengeneza soon nitaweka picha 10 zinazoonyesha mtiririko jinsi ya kuiandaa ila ni tamu sana na inaliwa na njegre za nazi na pilau kama unavyoona katika picha.




Hii ni honey grazed ham

Kwanza kabisa chukua roll nzima ya ham ichemshe kwa masaa 2 kisha kata slice ya honey grazed ham kisha weka slice ya nanasi, kisha weka slice za bacon ya nguruwe na juu yake weka slice za nyanya na mwisho kabisa weka slice za cheddah cheese. mwisho chemsha kiasi red wine katika kikaango kwa dakika 2 tu halafu mwagia pembeni ya chakula hiki.

Unakula na potato wheels na grilled vegetable kama inavyoonyesha katika picha kumbuka kuhudumia ikiwa yamoto.



Hii ni oven backed apple with cinamon sugar and vanila sauce

chukua apple kisha likate slice halafu chukua unga wa ngano na mayai piga pamoja kisha chukua slice za apple weka katika lile rojo la unga chova kisha toa panga hizo apple katika bakinga tray mwagia mafuta kiasi kisha zichome kwa moto wa watani zikisha badilika rangi zitoe.

kumbuka unatakiwa uwe umeshaandaa cinamona sugar( sukari ya mdarasini) ukitoa tu yale ma apple kwenye oven chovya katika hiyo sukari na kumbuka kuhudimia mlaji apple zikiwa bado zamoto.




Hii ni Calamerized cream na ladies finger biscuit, cherry na zabibu

Chukua sukari yeyote ile weka katika kikaango mpaka iungue iwe ya kahawia kisha weka maziwa changanya haraka haraka mpka upate rojo zito kisaha iache ipoe.

Chukua cream fresh tumia mchapo chapa mpaka iwe nzito kabisa iwe kama povu kama unamashine tumia kuchapa kwa urahisi zaidi kisha chukua lile rojo la sukari iliyopoa tumia kijiko kuchnagnaya cream iliyokma povu na lile rojo la sukari ya kahawia kisha weka katika chombo kizuri au bakuli dogo pamba na bikuti kama hapo juu na zabibu au strawberry.

FURAHIA PASAKA NA FAMILIA YAKO KWA CHAKULA NAFUU NA RAHISI KUTENGENEZA.


Thursday, April 1, 2010

BEEF SATAY MHHH YAM YAM YAM !!!

SATAY SAUCE UNAWEZA KUTUMIA KATIKA AINA YEYOTE YA NYAMA NA INALADHA KUBWA YA KARANGA

MAHIAJI
70 gram mafuta ya kupikia
150 gram kitunguu maji chop chop
1kilo Nyama ya ngombe au mbuzi au samaki au kuku
200 gram Soya sauce
500 gram karanga iliyosagwa ya kopo
pili pili ya unga au tabasco au pilipili fresh ( weka kulingana na ladha unayoweza kula)
500 gram maziwa ya maji
1 kijiko kidogo cha chai unga wa mdalasini
300 gram Nyanya ya kopo
1/2 kijiko kidogo cha chai pili pili manga
1/2 kijiko kidogo cha chai unga wa kayene
1 kijiko kidogo cha chai kitunguu swaumu kilichosagwa
1 kijiko kidogo cha tangawizi iliyosagwa
300 gram maji
100 gram vinega au maji ya limao.

JINSI YA KUANDAA

Weka mafuta katika sufuria kisha weka kitunguu maji, kitunguu swaumu, tangawizi, unga wa cayene, unga wa mdalasini, pili pili manga kaanga vichanganyike vizuri kwa dakika 2 -3

Kisha weka  nyanya ya kopo changanya vizuri, kisha weka karanga ya kusagwa changanya mpaka ichanganyike vizuri. kisha weka maziwa ya maji pamoja na maji koroga mpaka upate mchanganyiko safi kabisa mziti kama haijakorogeka vizuri tumia mchapo wa chuma.

kisha weka pili pili fresh au pili pili ya unga na juice ya limao. acha ichemke kama ni nzito sana ongeza maji au maziwa mpaka upate mchanganyiko mzito wastani na kama imekua maji sana basi ongeza karanga ili iwe nzito.


Kata nyama vizuri iwe katika umbo jembamba kama muonekano katika picha na iweke kwenye miti ya mishikaki ichome kwenye griller au jiko la mkaa yote sawa mpaka iive kabisa.



Hii ndio muonekano safi kabisa wa sauce nzito ya karanga ni tamu sana na unaweza kuitunza kwa miezi 2 - 3 katika freezer bila kuharibika ukawa unatumia kidogo kidogo kumbuka kuigawa katika kiasi kidogo utachokua unatumia ili kila unapohitaji usiyeyushe yote unapoyeyusha na kugandisha tena unaruhusu wadudu kuingiua na sauce yako itaharibika.



Kama kawaida weka wali au ugali au chips katika sahani kwa muonekano thabiti na mzuri ili kumvutia mlaji. Kwa mtummoja mpatie mishikaki mitatu ya nyama hahahahahahaaaaaa ikiwezekana muongeze maana ni mitamu sana sana.



Mwagia sauce juu ya nyama pole pole saafi kabisa. Kumbuka sauce yako isiwe maji iwe nzito ili iweze kushika katika nyama na ndio inabeba ladha nzima ya chakula.



Huu ni muonekano safi kabisa wa chakula hiki kizuri naimani familia yako itakipenda sana na watakusifia mama kila unapoingia jikoni basi watoto watakua wanakuja kukusumbua kwa harufu nzuri wanaona kama chakula kinachelewa.

KAMA HAUNA KARANGA YA KUSAGWA BASI KAANGA KARANGA KISHA ZIPIKE HIVYOHIVYO KWA KUFUATA UTARATIBU KAMA ILIVYOELEKEZWA BAADA YA KUIVA CHUKUA BLENDER SAGA UTAPATA SAUCE SAFI NA LADHA NZURI SANA.