CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Tuesday, March 23, 2010

FISH FILO PASTRY WRAP

HII NI BITE NZURI SANA NA UNAWEZA KULA KAMA MLO KAMILI PIA NA WALI UGALI AU VIAZI VYA KUKAANGA AU UKALA YENYEWE TU KWA JUISI AU SODA.

MAHITAJI

1 Yai
150 gram Kitunguu
100gram Pili pili hoho
100gram Caroti
5 matone ya Tabasco sauce
1 kilo Fillet ya samaki
1 Limao
1/2 kijiko kidogo cha chai chumvi
1 kijiko kidogo cha chai Unga wa binzali
Filo pastry/ manda ( inategemea na wingi wa mchanganyiko wa samaki na ukubwa wa bite yenyewe)
100 gram Unga wa ngano




Kata kata kitunguu, pili pili hoho, caroti kama inavyoonysha katika picha kisha changanya pamoja na chumvi na unga wa binzali hii husaidia kupunguza shombo ya samaki na kuongeza rangi nzuri ya chakula


Kisha chemsha kwa dakika 10 tu fillet ya samaki aina yeyote ile ya samaki uipendayo.


Kisha chukua samaki iliyokwisha chemshwa kwa wastani itakua haijaiva vizuri incharange charange mpaka isagike kabisa kisha iweke ndani ya mchanganyiko wako.



Kisha weka yai moja ndani ya mchanganyiko huo


Kisha weka unga wa ngano ndani ya mchanganyiko huo



 kisha changanya na ule mchanganyiko wa mboga mboga safi kabisa mpaka uchanganyike vizuri na kubadilika rangi kisha kamulia limao ili kuongeza ladha safi 




Kata filo pastry yako kwa umbo lolote lile upendalo



Kisha ongezea matone 5 ya tabasco sauce kuongeza kali ya pili pili hii huchangamsha sana mdomoni kama wanakula watoto jaribu kupunguza.



Kisha tumia kijiko kuchota mchanganyiko wako na kuuweka kati kati ya filo pastry ili uweze kukunja na kuufunika mchanganyiko wa samaki na mboga



Baada ya kuchota mchanganyiko wa samaki huu ndio muonekano



Anza kukunja kama picha inavyooonyesha



Endelea kukunja kama picha inavyoonyesha



Hapa sasa unaelekea kunjo la mwisho kama picha inavyoonyesha ukimaliza geuza chini iwe juu na juu iwe chini ili hii mikunjo yako ikandamizwe kwa chini kitafunwa chako kisije kikafunguka

Kisha chukua mafuta na brusha kipake hicho kitafunwa chako chote ili kulaini na kusaidia iwe laini pindi utakapo pika katika oven isiwe kau kau na iwe na rangi nzuri itakapo iva.

Choma kwenye oven kwa muda wa dakika 30 hadi 40 kulingana na moto wa oven yako.



Ukitaka kujia imeshaiva inakua ngumu na nzito zaidi na rangi ya kahawia, huu ndio muonekano baada ya kuva na unaipanga vizuri tu katika sahani na wali na mcuhi pembeni.



Usisahau ukiipamba vizuri kumbuka kuweka na limao pembeni au juu yake mlaji atakapo itaji kuongeza ladha zaidi katika kitafunwa hiki kizuri cha samaki

UFAFANUZI ZAIDI

Filo pastry inatengeneza kutokana na unga wa ngano na inatengenezwa kiwandani na ni laini kweli kumbuka kutumia leya 4 au nne ili iwe ngumu na nzito wakati wa kukunja ili isi vunjike au kuchanika na ni bei rahisi tu ukienda katika maduka ya chakula utaipata kwa urahisi kabisa

Kama hukubahatika kabisa kuipata madukani bado unananfasi kubwa sana tu ya kufurahia kitafunwa hiki kwa kutumia manda ya kutengenezea sambusa na usione utofauti na ikapendeza kabisa.

WAFURAHISHE WATOTO NYUMBANI KWA KUWAANDALIA SAMAKI HUYU MTAMU KABISA KUMBUKA WATOTO WENGI HUPENDA VYAKULA VIKAVU KULIKO VYA MCHUZI



Sunday, March 21, 2010

WAPENZI WA SUPU FAIDIKENI SASA KAZI IMEANZA

JINSI YA KUTENGENEZA SUPU YA SPINACHI

MAHATIJI

2 kilo Spinach
1/2 kilo Karoti
300 gram Kitunguu
500gram Kiazi ulaya
250 gram siagi
200 gram fresh cream kwa kupambia
250 gram maziwa ya maji/ fresh cream


FATA MAELEZO JINSI YA KUTENGENEZA SUPU YA SPINACH KAMA PICHA NA MAELEZO YANAVYOELEKEZA.




Kata mboga zako kama inavyoonekana katika picha kumbuka kuziosha vizuri sana na kausha maji



Kisha weka siagi katika sufuria acha iyeyuke vizuri



Kisha weka vitunguu ndani ya sufuria kaanga kidogo vilainike



Kisha weka mchanganyiko wa mboga zote zilizobaki changanya vizuri zichznganyike



Kisha weka maji baridi katika sufuria yenye mchanganyiko wa mboga na uiache ichemke



huu ni muonekano wa kuiva kwa mboga na maji yamebadilika rangi tayari kwa kusagwa na kua supu tamu kabisa



Chukua mchanganyiko wako safi kabisa wa mboga na maji kisha weka katika blender na saga mpaka upate rojo safi kabisa na laini




Baada ya kublend mchanganyiko wote huo rudisha supu yako katika jiko na ichemshe tena kwa uongeza ladha weka frsh cream au maziwa ya maji acha ichemke vizuri kisha weka chumvi kulingana na ladha yako ila supu haipendezi kua na chumvi nyingi kua makini



Kisha chota supu yako safi na mimina kwenye chombo maalumu cha kuhudumia mnywaji wa supu yako



Huu ndio muonekano wa supu yako katika bakuli maalumu la kunywea



Hii ni chupa maalumu kwajili ya kupambia supu yako, unachotakiwa kufanya ni kuweka fresh cream ndani yake.



Kisha tumia chombo hiki kumimina katika bakuli maalumu na uzungushe miduara eneo lote la bakuli kama picha inavyelekeza.




Pole pole zungusha mduara mapaka mwisho





Kisha tumia toothpik kuchorea michirizi mizuri amabyo itafanya muonekano tofauti katika supu yako na kumfanya mnywaji ashangae kabla ya kunywa supu hii anzia katikati kata mpaka mwisho wa bakuli.



Hivyo hivyo kata kuanzia kati kati mpaka mwisho huu ndio muonekano wako halisi wa supu kumbuka kufanya zoezi hili kwa haraka sana na mpatie mnywaji wa supu ikiwa ya moto.




WAJUA MAPISHI MBALI MBALI YATOKANAYO NA WALI WA MAJI ???


WALI WA MAJI UNAWEZA UKAUBADILISHA KATIKA MAPISHI MENGI SANA MFANO UMEPIKA WALI WA MAJI GHAFLA UKAVAMIWA NA WAGENI  JUMAPILI YA LEO BILA TAARIFA NYUMBANI NA NI WAHESHIMA NA WAKATI WAKULA UMEKARIBIA WASHANGAZE KWA MAPISHI TOFAUTI MOJA WAPO NI HAYA MAWILI.

1- PILAU SAFI LA ZABIBU KAVU
2- WALI WA CAROTI 

NI RAHISI SANA KAMA NI HOTELINI AU NYUMBANI MLAJI AKAFURAHIA SANA SANA KWA LADHA SUPA!!!!!!!!

PILAU LA ZABIBU KAVU

Mahitaji

30 gram Unga wa binzali
50 gram Kitunguu swaumu kilichosagwa
10gram mbegu za Karafuu kavu
20 gram Mdalasini ya unga
20 gram Hiriki ya unga au mbegu
100 gram Kitunguu maji
150 gram Zabibu kavu
15 gram Pili pili manga
15 gram Jira ya unga




Huu ni muonekano wa wali wa maji uliokwisha pikwa ukaiva



Weka mafuta yapete moto kisha weka kitunguu maji kilicho katwa katwa safi pamoja na kitunguu swaumu kaanga kwa dakika 2 tu kilainike




Kisha weka mchanganyiko wa viungo vyako vyote vilivyobakia katika kikaango au sufuri kisha kumbuka kukoroga ili visishike na kuungua chini ya chombo unachopikia.



pili pili manga, mdalasini ya unga, zabibu kavu, unga wa binzali, jira ya unga, mbegu za hiriki na mbegu za karafuu kisha kaanga mapaka viungo hivi viungue kiasi kama dakika 3 - 4 zinatosha



Baada ya kuiva viungo vyako weka wali wako uliokwisha iva ndani ya viungo hivyo changanya haraka na kwa umakini zaidi mpaka wali wote uchanganyike vizuri na viungo vyote na kubadilika rangi safi kabisa.




Huu ndio muonekano safi kabisa wa wali wako ukiwa tayari kwa kuliwa na kinachoonekana hapa ni zabibu kavu tu mhhh wali huu ni mtamu sana sana.




Baada ya pilau lako kuiva tafadhali kumbuka kulipamba katika sahani usipakue kwenye hot pot pilau yako safi imalizie kwa muonekano safi kabisa na unaovutia.


MAPISHI YA WALI WA KAROTI

Mahitaji

Kitunguu maji
karoti
siagi( Butter) inasaidia kuweka harufu nzuri katika chakula chako




Huo ni muonekano halisi wa kitunguu kilichokatwa na karoti iliyokwaruzwa


Weka siagi yako katika sufuria kisha weka vitunguu kaanga kidogo





Kisha weka karoti pia kaanga ziiive kiasi 




Huu ndio muonekano wa karoti imeshaiva





Kisha weka wali wako ndani ya mchanganyiko wa wali uliokwisha iva



Hakikisha unachanganya safi kabisa mapaka karoti na wali vinachanganyika safi




Kisha tengeneza shape nzuri ya wali na weka katika sahani



Wali huu unaweza kula na mboga yeyote ile na utakua umewashangaza wageni kwa ubora na ladha ya chakula ulichowaandalia furahia weekend na familia yako hujachelewa.


Tuesday, March 16, 2010

UNATAKA KUFANYA BBQ PARTY SUPER NYUMBANI KWAKO?


JIBU KUBADILISHA UBORA WA CHAKULA NA MTINDO WA MUONEKANO WA SHEREHE UTAYOIFANYA NYUMBANI KWAKO YA AINA YEYOTE ILE IKIWA UMEWAALIKA RAFIKI ZAKO AU NDUGU WA KARIBU WASHANGAZE NA WAFURAHIE IWE HISTORIA FATA MAELEKEZO YA MAANDALIZI KWAUJUMLA HAPO CHINI KAMA PICHA ZINAVYOOELEKEZA.





kata mboga zako aina tano au nne mfano kitunguu, nyanya, bilinganya, zucchini, carroti na pili pili hoho kisha  zipake mafuta na chumvi kisha ziweke kwenye kikaango au kwenye jiko lako la kuchomea nyama na uzichome ziive nusu zisiive sana ziweke pembeni zipoe na zitatumika kama salad wakati wa BBQ lunch au diner.




Hapa ni muonekano wa mpangilio mzima wa salad. Kwakua sherehe yetu ni BBQ basi kila chakula lazima hkiwe na ladha nzuri ya harufu ya moshi wa makaa. Zile mboga ulizochoma zipange vizuri katika sahani na uziweke sehemu moja kama zinavyoonekana katika picha wageni wako watafurahia sana saladi hii.





Katika picha unaona mpangilio wa sauce safi kabisa maalumu kwajili ya kulainisha na kuongeza ladha katika nyama choma zako safi kabisa. Kutoka kushoto katika picha ni Teriyaki sauce, BBQ sauce, vipande vya limao na chilly pickle jinsi ya kutengeneza vyote hivi mwisho kabisa soma recipe yake.




Hizi ni mbavu za nguruwe au (pork spare ribs).

Chukua mbavu za nguruwe kata katika mikato ya wastani ambayo unaweza kushika na kula. kisha chukua kitunguu swaumu na tangawizi iliyosagwa changanya na mafuta ya kupikia kidogo, nyanya ya kopo, soya sauce na chumvi kisha changanya mpaka rojo lote lishike nyama yote kisha weka katika oven iive nusiua narojo lile lishike vizuri kwenye nyama. kisha weka pembeni kwajili ya kuiivisha vizuri kabisa katika jiko lako la mkaa baadae wakati wa sherehe.




Hii ni nyama ya ngombe (Beef fillet)

Kata nyama kwa urefu umbo la kama kidole ili ilingane na iwe rahisi kuiweka katika mti wa mshikaki. Kisha chukua tangawizi na kitunguu swaumu kilichosagwa, chumvi, pili pili manga, mafuta ya kupikia, soya sauce, nyanya ya kopo, tabasco sauce kidogo na Hp sauce kidogo changanya mpaka rojo lote lichanganyike katika nyama yako iweke katika friji kwa muda wa saa nzima au 2 kisha iwe tayari kuchiomwa katika jiko la mkaa wakati wa sherehe mikato ya aina hii inasaidia uivaji na kupunguza gharama maana unatengeneza mishikaki mingi sana kwa nyama kiasi tu.

Mchanganyiko huu unaweza tumia pia unapoandaa kuku wa kuchoma mhhhh!!!!





Hii ni mishikaki ya samaki unaweza tumia fillet ya ( sangara, redsnapper, king fish, barakuda)
Kata fillet ya samaki kwa urefu ilingane kiasia urefu wa mshikaki wako hii inasaidia kuiva haraka na urahisi wa mlaji.
Baada ya kukata chomeka katika miti ya mishikaki. Kisha chukua juice ya limao, unga wa binzali, kitunguu swaumu na tangawizi iliyosagwa, chumvi na pili pili manga pia unaweza weka mtindi changanya mpaka rojolile lichanganyike vizuri kabisa kisha wea katika friji tayari kwa kuchomwa baadae wakati wa sherehe.




Hivi ni viazi mishikaki mhhh safi sana na rahisi kweli kutengeneza.

Chukua kiazi ulaya kimenye kisha kikate nusu, kisha chomeka katika kila nusu mti wa mshikaki kama inavyoonenkana kwenye picha. Kisha chukua sufuria weka maji baridi kisha weka viazi vyako na uchemshe mpaka viive nusu. Ukiweka maji baridi yanasaidia viazi vyako kuchemka pole pole pamoja na viazi hii itasaidia viazi vyako visipoteze umbo lake mongo'nyoka vitaiva na kubaki na umbo lake zuri. weka viazi kwa mtindio wa kusimamisha miti juu viazi chini ndani ya maji.

Tumia mti wa mshikaki kwajili ya kucheki kama viazi mvimeiva ukichoma mti ukaingia kirahisi badi vimeiva kama havijaiva mti hauwezi kuingia. kisha vitoe viazi vyako vikae pembeni visubiri kuchomwa wakati wa sherehe. 







Sasa ndio wakati wenyewe umewadia wageni wameshafika na chakula chako kipo jikoni tayari kwa kuwashangaza wale wote walioudhulia kwa kula chakula chenye ladha safi na kinapikwa live!!

Tenganisha nyama zako kama inavyoonekana katika picha Kiazi kikae mahala pake kisichanganyike na nyama yeyote ile, pia samaki na nguruwe zisiguzane na nyama yeyote ile maana sio kila mtu anakula samaki na ngurue aidha kwa misinghi ya dini au aleji.

Nyama ya ngo'mbe na kuku vianweza kukaa pamoja hakuna neno vyakula vyako vyote katika jiko la mkaa vipake mafuta ving'ae ili vipate rangi nzuri ya kahawia ukiendelea kuvichoma pia mafuta yanapodondokea katika mkaa na ladha ile ya nyama inatoa moshi mzuri wenye harufu ya nyama choma na kuwadondosha mate na kuwazidishia hamu wageni si mchezo wakati bado hawajaruhusiwa kuvamia sehemu ya maakuli yanayopikwa live.




Huu ni mpangilo safi kabisa wa nyama pamoja na viazi katika jiko lako la nyama choma kumbuka miti ya mishikaki iangalie nje ya jiko hii ni kwajili ya usalama wa miti isiungue na wewe mchomaji iwe rahisi kugeuza na wakati mlaji anahitaji ni rahisi kuchukua katika jiko. Huitaji madishi ya kuhifadhia chakula maa chakula chote unapika live katika jiko moja yaani we acha tu ni rahisi na ninafuu sana na itapendeza sana sana. 



Yaani kila kitu kime kaa ki BBQ tu baada ya kupata mlo safi kabisa mwisho ni kikata hamu cha chakula chukua matunda yako ya aina 3 hadi 5 au 6 kulingana na uwezo wako. katika picha huo ni mshikaki wa matunda ya aina 3 tu. chukua nanasi, embe na water melon kata mtindo wa box kisha tunga katika mti wa mshikaki na weka katika sahani yako safi na uweke kwenye friji yapoe kwajili ya kuliwa katika sherehe.




Hahaha samahani jamani huu ndio muonekano wa chakula katika sahani baada ya kujipakulia ni rahisi kula ni rahisi kuandaa na gharama ni nafuu sana na wageni wako hawata chafuka na michuzi kila mtu anaweza kuaanda hivi nyumbani kwa gharama nafuu sana ukiniambia idadi ya watu unaotaka kuwaalika nitakupa kiasi cha mahitaji anaukafanya BBQ party yako iwe safi kabisa.


JINSI YA KUANDAA VIKOLOMBWEZO VYA KULIA NYAMA

Jinsi ya kutengeneza pili pili angalia mafunzo ya mwezi wa pili katika blog archive

BBQ sauce zipo madukani nyingi san tu zinauzwa na ninafuu kununua kuliko kutengeneza

Malimao unakata kama picha inavyoonyesha

Jinsi ya kuandaa teriyaki sauce

400gram Chukua soya sauce
200gram maji
50gram kitunguu swaumu kilichosagwa
50gram tangawizi iliyosagwa

Chemsha kwa pamoja mpaka ipungue na kua nzito kiasi kisha weka ipoe tyari kwa kuliwa na nyama choma

MAHITAJI YA BBQ KAMA UNAWATU 100 HADI 150

17 Kuku ( kuku mmoja kata vipande 10)
5 kilo Fillet ya ng'ombe
5 kilo Mbavu za nguruwe
5 kilo Fillet ya samaki
20 kilo Viazi ulaya

BBQ SALAD
3 kilo Nyanya
3 kilo Kitunguu
3 kilo karoti
2 kilo Bilinganya
2 kilo Zucchini