CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Sunday, March 21, 2010

WAJUA MAPISHI MBALI MBALI YATOKANAYO NA WALI WA MAJI ???


WALI WA MAJI UNAWEZA UKAUBADILISHA KATIKA MAPISHI MENGI SANA MFANO UMEPIKA WALI WA MAJI GHAFLA UKAVAMIWA NA WAGENI  JUMAPILI YA LEO BILA TAARIFA NYUMBANI NA NI WAHESHIMA NA WAKATI WAKULA UMEKARIBIA WASHANGAZE KWA MAPISHI TOFAUTI MOJA WAPO NI HAYA MAWILI.

1- PILAU SAFI LA ZABIBU KAVU
2- WALI WA CAROTI 

NI RAHISI SANA KAMA NI HOTELINI AU NYUMBANI MLAJI AKAFURAHIA SANA SANA KWA LADHA SUPA!!!!!!!!

PILAU LA ZABIBU KAVU

Mahitaji

30 gram Unga wa binzali
50 gram Kitunguu swaumu kilichosagwa
10gram mbegu za Karafuu kavu
20 gram Mdalasini ya unga
20 gram Hiriki ya unga au mbegu
100 gram Kitunguu maji
150 gram Zabibu kavu
15 gram Pili pili manga
15 gram Jira ya unga
Huu ni muonekano wa wali wa maji uliokwisha pikwa ukaivaWeka mafuta yapete moto kisha weka kitunguu maji kilicho katwa katwa safi pamoja na kitunguu swaumu kaanga kwa dakika 2 tu kilainike
Kisha weka mchanganyiko wa viungo vyako vyote vilivyobakia katika kikaango au sufuri kisha kumbuka kukoroga ili visishike na kuungua chini ya chombo unachopikia.pili pili manga, mdalasini ya unga, zabibu kavu, unga wa binzali, jira ya unga, mbegu za hiriki na mbegu za karafuu kisha kaanga mapaka viungo hivi viungue kiasi kama dakika 3 - 4 zinatoshaBaada ya kuiva viungo vyako weka wali wako uliokwisha iva ndani ya viungo hivyo changanya haraka na kwa umakini zaidi mpaka wali wote uchanganyike vizuri na viungo vyote na kubadilika rangi safi kabisa.
Huu ndio muonekano safi kabisa wa wali wako ukiwa tayari kwa kuliwa na kinachoonekana hapa ni zabibu kavu tu mhhh wali huu ni mtamu sana sana.
Baada ya pilau lako kuiva tafadhali kumbuka kulipamba katika sahani usipakue kwenye hot pot pilau yako safi imalizie kwa muonekano safi kabisa na unaovutia.


MAPISHI YA WALI WA KAROTI

Mahitaji

Kitunguu maji
karoti
siagi( Butter) inasaidia kuweka harufu nzuri katika chakula chako
Huo ni muonekano halisi wa kitunguu kilichokatwa na karoti iliyokwaruzwa


Weka siagi yako katika sufuria kisha weka vitunguu kaanga kidogo

Kisha weka karoti pia kaanga ziiive kiasi 
Huu ndio muonekano wa karoti imeshaiva

Kisha weka wali wako ndani ya mchanganyiko wa wali uliokwisha ivaHakikisha unachanganya safi kabisa mapaka karoti na wali vinachanganyika safi
Kisha tengeneza shape nzuri ya wali na weka katika sahaniWali huu unaweza kula na mboga yeyote ile na utakua umewashangaza wageni kwa ubora na ladha ya chakula ulichowaandalia furahia weekend na familia yako hujachelewa.


7 comments:

Anonymous said...

Thank ma bro, leo ntakijaribu kulipika ili wali la carrot. blog yako ni nzuri

Anonymous said...

Kaka Inshallah nitapika mapishi fulani katika birthday ya mtu halafu nitapiga picha nikutumie.disminder.

Anonymous said...

Yaami kaka nashukuru sana kwa elimu hii ambayo ni nadra kuipata kama hivi. Ninaipenda sana blog yako na ni lazima niifungue kila siku kwa kuwa ninapenda sana kupika na kwa kweli haya maujuzi unayotuongezea yanatupa credit sana tu majumbani mwetu. Asante sana na Mungu akubariki!

Anonymous said...

jamani chef eti jira moto ndio nini?

Anonymous said...

we ni mkali,kila unachopika kinavutia!!!ntajaribu pilau na zabibu....

Ruky said...

Thank you

Anonymous said...

Du kaka yangu yaani hapa umenusuru ndoa yangu yaani kumbe nilikua sijui kupika kabisa!!!! Endelea kutuelimisha hivyo hivyo!