CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Monday, January 9, 2012

JIFUNZE KUTENGENEZA CHAKULA HIKI CHA MCHANGANYIKO WA MABOGA, KAROTI, KITUNGUU NA PANEEL CHEESE


 RECIPE HII SAFI KABISA YA CHAKULA HIKI CHA MCHANGANYIKO WA MBOGA

MAHITAJI

120 gram mbegu za alizeti au unaweza tumia mbegu za ufuta

1 Boga dogo, menya, toa mbegu na katakata vipande
1 kitunguu kikubwa, chop chop
5 gram kitunguu swaumu
1 carrot kubwa, kata kata vipande vya ukubwa kama kwenye picha
240 gram paneel cheese au unaweza tumia ( mushrooms , uyoga )
1 kijiko kikubwa cha chakula korosho za kuoka, chop chop
1 fungu la corriender na parsley kwajili ya kupambia
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga



JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi : Dakika 30

Muda wa kupika : 30 dakika mpaka saa 1
Idadi ya walaji :  Watu 2



Weka maboga katika baking pan, nyunizia kiasi mafuta pamoja na pili pili manga. 



Roast katika oven kwa moto wa 400F kwa muda wa dakika 20 hadi 30 hakikisha inaiva na ukibonyeza inabonyezeka yaani laini wastani.


Kisha weka mafuta katika kikaango na kikishapata moto weka kitunguu, karoti na paneel cheese pampoja na chumvi na kitunguu swaumu endelea kukaanga.

 

Kisha weka maboga yaliookwa kwenye oven pamoja na mbegu za ufuta au mbegu za alizeti pia unaweza tumia hata mbegu za maboga endelea kukaanga na onja kama chumvi au pili pli manga haitoshi ongezea kiasi.


Kisha mwagia kwa juu majani ya korrienda na parsley kuongeza ladha na kuongeza rangi katika muonekano wa chakula chako.

 

Chakula hiki ni safi sana kwa afya ya mlaji kwani hakina mafuta kabisa pia ni tajiri sana kwa nutrition, Kumbuka kumwagia kwajuu zile korosho za kuokwa kwa juu kabla ya kumpatia mlaji.


Chakula hiki unaweza kula kama kilivyo au ukaongeza nyama, samaki au chapati au mkate pia na ukafurahia mlo huu wewe na familia yako.

 



NI RAHISI SANA KUANDAA NA HAKINA GHARAMA KABISA WAANDALIE FAMILIA YAKO CHAKULA BORA WAFURAHI.



 

Friday, January 6, 2012

JIFUNZE KUPIKA WALI AINA YA RISOTTO


RECIPE SAFI KABISA YA KUPIKA WALI AINA YA RISOTTO WALI HUU ASILI YAKE NI ITALIA NA MARA NYINGI UNAPIKWA NA MVINYO MWEUPE NA CHEESE  HAKIKA LADHA YAKE NI SAFI SANA SANA!!!


MAHITAJI

360 gram Arborio Rice ( Risoto rice)

1/2 kijiko kidogo cha chai Saffron strands
2 kijiko kikubwa cha chakula siagi
1 kitunguu maji kikubwa chop chop
1 kijiko kidogo cha chai kitungu swaumu cha kusagwa
1 kwaruza limao maganda yake (zest Lemon)
1.2 lita ya maji
5 gram chumvi
3 vegetable cubes
2 glasi za white wine
5 gram pili pili manga
20 gram Vegetarian Parmesan Cheese shaving
2 kijiko kikubwa cha chakula Extra Virgin Olive Oil (sio lazima)
Parsley kwa kupambia


JINSI YA KUPIKA FATILIA PICHA NA MAFUNZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi: Dakika 15

Muda wa kupika: Dakika 30
Idadi ya walaji: Watu 4


Chukua sufuria kisha chemsha maji lita moja na nusu pia weka vegetable cubea ili uweze pata vegetable stock na hakikisha unafunika ili yachemke mapema.



Weka saffron katika bakuli pamoja na maji yamoto kijiko kimoja mpaka iyeyuke na kubadilisha rangi.



Weka siagi katika sufuria ikishayeyuka weka kitunguu maji na kitungu swaumu endelea kukaanga kwa dakika 3 mpaka iwe laini.



Kisha chukua wali wako mkavu hutakiwi kuuuosha kawaida huwa unakua msafi sana. Weka ndani ya sufuria na endelea kukaanga.


Endelea kukaanga mpaka utaona unabadilika rangi na kunukia harufu nzuri.



Kisha weka glasi moja ya mvinyo mweupe ( white wine) pamoja na safrom acha iendelee kuiva pole pole. Kumbuka safron sio lazima kuweka. 

 

Hakikisha unaendelea kukoroga na chakula chako kisishike kwa chini au kuungulia.



weka gram 600 za vegetable stock katika yale maji uliochemsha mwanzo katika wali wako na koroga kisha acha maji yakaukie kumbuka wakati unasubiri maji ya kauke unatakiwa mara kwa mara unaendelea kukoroga.



Kisha ongeza kikombe kimoja cha white wine endelea kukoroga. Hakikisha kila maji yanapokauka we unaendelea kuongeza kikombe kimoja yakikauka tena unaongeza kikombe kimoja mpaka wali wako uive.


Baada ya wali wako kua creamy sasa weka chumvi na pili pili manga kisha koroga vizuri.



Mwagia kwa juu na Parmesan cheese, parsley. Mimi na familia yangu huwa tunapenda kunyunyiziakwa juu Extra Virgin Olive oil chakula kikiwa tayari kwenye sahani inasaidia kuongeza moistness na richness kwenye  risotto nikiwa pembeni na Crusty bread.




ONYESHA UJUZI WAKO FAMILAI IFURAHIE CHAKULA HIKI KITAMU



Saturday, December 31, 2011

KHERI YA MWAKA MPYA WAPENZI WOTE WA BLOG YA CHAKULA SALAMA NA BORA



HABARI WAPENZI WA BLOG HII SAFI YA CHAKULA BORA NA SALAMA

NASHUKURU SANA KWA USHIRIKIANO WENU NA MCHANGO WA MAWAZO YENU PAMOJA NA KUA WASOMAJI WAZURI SANA WA BLOG HII.

CHANGAMOTO ZIMEKUA NI NYINGI SANA IKIWA MOJA WAPO NI MUDA WA KUKAA CHINI KUWEKA PICHA NA MAELEZO YA MAFUNZO JINSI YAKUNDAA VYAKULA.

TUOMBE UZIMA MOLA AKIPENDA NITIMIZE NDOTO YANGU YA KUANZA KUWEKA VIDEO HII HAITAKUA NA MASWALI MENGI MAANA KILA MMOJA WENU ATAONA NA MNAKIELEWA KISWAHILI KWA UFASAHA KABISA.

PIA WALE WOTE WALIOJIANDIKISHA KUJIUNGA NA CHAMA CHA WAPISHI TANZANIA KAENI TAYARI KABISA KWA MKUTANO MKUU WA CHAMA PIA TUWEZE KUCHAGUA VIONGOZI NA SHUGHULI ZA CHAMA KUANZA RASMI

KWA NIABA YA ACTIVE CHEF ASSOCIATION OF TANZANIA NA CULINARY CHAMBER BLOG NAWATAKIA MWAKA WA MAFANIKIO NA AFYA NJEMA 2012 MOLA ATULINDE SOTE NA ATUSIKILIZE DUA ZETU SOTE AMIIN

WASALAAM

CHEF ISSA


Thursday, December 29, 2011

JIFUNZE KUPIKA KITAFUNWA CHA SPINACH NA DENGU


KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABIS A YA KITAFUNWA HIKI CHA DENGU NA SPINACH

MAHITAJI

240 gram dengu (Whole Black Gram)

2 pili pili mbuzi (green chillies)
5 gram tangawizi ya kusaga
1 kitunguu maji kikubwa chop chop
240 gram spinach mbichi ikate kate (chopped Spinach)
5 gram chumvi
majani ya giligilani ya kuongeza ladha (Cilantro)
majani ya curry kwa kuongeza ladha (Curry leaves)
JINSI YA KUPIKA FATILIA PICHA NA MAFUNZO HAPA CHINI

Muda wa kuandaa : masaa 3 hadi 4

Muda wa kupika: dakika 30
Idadi ya walaji: Watu 4
Idadi wa vitafunwa : Kiasi cha 8-10 inategemea na upana au umbo


Loweka kwenye dengu  kwenye maji kiasi cha lita moja kwa masaa 2 hadi 3 au mpaka utakapo ona zimeshameza maji na kulainika.



Hakikisha unazichuja na kuzikausha vizuri kama picha inavyoonyesha.



Weka dengu zako kwenye blenda ( food processor) pamoja na chumvi, tangawizi na pili pili ila sio lazima kama hutumii pili pili ingawa inaleta ladha ya kuchangamsha. 


Hakikisha unasaga mchanganyiko uwe na muonekano kama huo usiweke kabisa maji ila kama blenda yako unaona haiwezi kusaga sababu ya ukavu basi weka maji kidogo sana ili uweze kusaga na kupata mchanagnyiko mkavu kama huo.



Kisha chukua dengu zilizosagwa weka katika bakuli pamoja na kitunguu maji, majani ya gili gilani, majani ya curry pamoja na spinach pia unaweza nyunyizia ndimu kiasi kuongeza ladha sio lazima.



Hakikisha unachanganya vizuri sana.



Kata kidogo na kisha hakikisha unatengeneza umbo la kama mpira.



Tumia karatasi ya Plastic na uipake mafuta kisha weka ule mviringo wa machanganyiko wa dengu na spinach juu yake kisha tumia vidole vyako viwili na ukandamize.



Tumia kidole chako na choma kati kati upate umbo kama la doughnut. Ni jinsi ya kutengeneza umbo zuri lakini sio lazima!



Chukua sufuria au kikaango weka mafuta kisha pata moto wa wastani chukua ile mchanganyiko kisha weka katika sufuria na endelea kukaanga hakikisha mafuta ni moto wasatani ili isibabuke na matokeo yake haiivi ndani (med-hot).



Kumbuka kugenuza mara kwa mara mpka upate rangi hii nzuri ya kahawia.



Kisha toa na weka katika karatasi ili yapoe na kuchuja mafuta pia. Kama ulifata maelekezo vizuri basi itaiva vizuri na wala hazitakau na mafuta kabisa karatasi haitaloana mafuta kabisa.



Hakikisha unampatia mlaji haraka sana ikiwa bado inamoto kwani ndio inakua na ladha nzuri pia unaweza kula na- Coconut chutney, spicy tomato chutney au tomato ketchup! ni nzito sana ukila unashiba kabisa.


Hazipendezi kukaa kwenye friji zaidi ya siku moja zinapoteza ladha na ubora pia

 



MIMI NA FAMILAI YANGU HUWA NAPENDA KULA NA SPICE TOMATO KETCHUP NA TUNAFURAHIA SANA. NI RAHISI KUTENGENEZA NA FAMILIA ITAFURAHIA SANA KITAFUNA HIKI.

Thursday, November 24, 2011

JIFUNZE KUPIKA DENGU HIZI TAMU SANA


 RECIPE SAFI SANA YA DENGU HIZI ZA AINA YAKE
MAHITAJI


240gram Pigeon Peas ( Dengu)
1/4 tsp Turmeric (manjano)
720 gram maji masafi
3  kijiko kikubwa cha chakula samli (Ghee)
1 kitunguu kikubwa chop chop
1 nyanya ya kuiva kubwa chop chop
1 kijikon kimoja cha chai binzali nyembamba
2 pili pli kavu nyekundu (Dried Red Chilies)
3 mbegu za karafuu
1 tangawizi ya kusaga (grated Ginger)
majani ya Curry na giligilani kwajili ya kupambia
5 gram maji ya limao
5 gram ya chumvi

JINSI YA KUANDAA CHAKULA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa kuandaa : Dakika 15

Muda wa kupika : Dakika 15
Idadi ya walaji : Watu 4




Osha dengu katika maji baridi kisha zichuje vizuri.



Unaweza tumia njia mbili ya kuzipika hizi dengu moja ni kuloweka kwa masaa 2 kisha unazichemsha kwa sufuria ya kawaida au unaweza tumia pressure cooker na ukaweka manjano na kutumia maji gram 720.



Kwa kutumia preasure cooker ni dakika 10 tu zinakua zimeshaiva.



Wakati unachemsha dengu weka kikaango au sufuria ipate moto weka mafuta kisha ongeza samli (Ghee), binzali nyembamba, karafuu, pilipili, tangawizi, kitunguu maji pamoja na chumvi endelea kukaanga.



Vitunguu vinapoanza kuiva ongeza nyanya endelea kukaanga zikiiva weka majani ya curry na majani ya giligilani.



Toa dengu zako katika pressure cooker. dengu zako zitakua zimeiva kabisa na kua na ubora safi kabisa.



Maji yatakua yamekauka katika preasure cooker chemsha maji kikombe kimoja na weka katika preasure cooker na ukoroge.



Kisha chukua ule mchanganyiko wako wa vitunguu na nyanya kisha mimina kwenye dengu zako.



Hakikisha unaendelea kukoroga na ongeza maji ya limao pia kwa kuongezea ladha zaidi.



Hakikisha unampatia mlaji chakula hiki safi kabisa kikiwa chamoto unaweza kula na chapati, mkate, Tortillas, Naan or ugali pia hata wali na familia ikafurahia sana.



Binafsi huwa napenda kula ikiwa pamoja na chapati na wali ili kuongeza ladha na ubora huwa naongeza limao kwakua linasaidia kupunguza madini ya chuma katika dengu.








ANDAA CHAKULA HIKI KIZURI UKIWAPUMZISHA NYUMBANI KULA NYAMA MARA KWA MARA NA WATAFURAHIA KUANZA MWAKA NA CHAKULA SAAFI