CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Tuesday, March 30, 2010

UTAIPENDA SANA COMFY CHICKEN

CHICKEN COMFY NI CHAKULA SAFI SANA PIA KINASAIDIA SANA KATIKA UCHUMI WA NYUMBANI KUMBUKA FAMILIA ZETU ZA KIAFRIKA NI KUBWA KUKU MMOJA UNALISHA WATU 10 HADI 12 NA KILA MTU ANAFURAHIA NA KURIDHIKA.

MAHITAJI

500gram karoti
300gram kitunguu
500 gram pili pili hoho
150 gram mafuta ya kupikia
1/2 kijiko kidogo cha chai chumvi
25 gram kitunguu swaumu
1.5 kilo kuku


JINSI YA KUANDAA FATA MAELEZO KATIKA PICHA



Chukua kuku mmoja mzima mwenye kilo moja na nusu kisha mchemshe katika maji na chumvi aive kabisa nyam iwe laini.


Kisha inyofoe nyofoe hiyo nyama kakitka kuku mifupa weka pembeni kumbuka kutoa mifiupa yote kwa umakini zaidi ni hatari kwa mlaji. Baada ya kuinyofoa nyama na kuitenganisha na mifupa utabakia na gram 800 au 700 gram.



Huu ni ni muonekano wa jisi ya kuzikata mboga kisha zichanganye zote kwa pamoja katika kikaango zikaange ziive tu kiasi. kisha weka kitunguu swaumu na changanya ile kuku ulionyofoa na kua na mfano wa mikato kama ya kuku pika kwa dakia 2 au 3 katika kikaango ni kiasi cha mboga na kuku kuchanganyika na ile kuku ipate tu moto.




Kisha weka katika sahani inaweza kuliwa na wali, ugali, viazi au chapati. Chakula hiki ni salama hata mtoto anaweza kula maana hakina mfupa na mchanganyiko huu wa mboga unaleta ladha safi sana.

Chakula hiki unaweza kulisha watu 10 na kila mmoja anakua amekula wastani wa gram 200 za mchanganyiko wa mboga na kuku inatosha kabisa iwe ni hotelini au nyumbani. Pia kumbuka kula na mchuzi wa nyanya au mchuzi wowote ule upendao.


MWANAO ANAUZITO MDOGO NA ANASUMBUA KULA?? MSAIDIE APENDE KULA!!!

MATATIZO YA MTOTO KUTOPENDA KULA YANASABABISHWA NA VITU VINGI SANA MOJA WAPO IKIWA NA KUKOSA HAMU YA KULA HII PIA INAWEZA KUSABABISHWA NA KINYWA KUTOKUA SAFI NA KUKOSA LADHA KWA CHAKULA PIA IKAMPELEKEA KUTOPENDA KABISA KULA.

MFANO MTOTO UNAPOMSAFISHA KINYWA TAFADHALI KUMBUKA KUBRASH POLE POLE SANA ULIMI ILI KUONDOA ULE UTANDO WA MAZIWA KATIKA ULIMI ANGALIA SANA UZIMUUMIZE MTOTO.

HATA MTU MZIMA KAMA HUNA HAMU YA KULA HUWEZI KULA KABISA TIBA HII NI KWA MTU WA LIKAYEYOTE ASIYE NA HAMU YA KULA TUMIA TANGAWIZI KATIKA JUICE NA CHAKULA WEKA KIASI KIDOGO TU SI MPAKA IWASHE LA HASHA! ITAKUONGEZEA SANA HAMU YA KULA.

HAPA CHINI NI USHAHIDI WA MAMA ANAYEMPENDA NA KUMJALI MWANAE ALIFATA MAFUNZO HAYA NA HIZI NI SHUKURANI ZAKE BAADA YA KUONA MAENDEKEO NA MAFANIKO YA MWANAE.

Hi Chef Issa
Mie naomba nikushuru kwa recipe yako ilee kuhusiana nawatoto wasikula maana imemsaida saana mwanangu, amefanikiwa kuongezeka ka kilo wakati miezi miwili iliyofuatana clinic alikuwa anashuka kgs
nilichokuwa nafanya ni kumchanganyia tangawizi katika kila mlo wake ukiwepo kumchemshia Samaki /supu pamoja na tangawizi na kisha kuja tumbukiza kama ni ndizi nk.

na kumsaigia juice yenye tangawizi, japo nilishindwa ile kutumia ile kumcheshia kwenye maziwa sababu anatumia mawaziwa ya kopo nilichokuwa nafanya kuchemsha maji na tangawizi ndo hayo namkorogea nayo maziwa
Ahsante endelea kutupa darasa zaidi...na ikiwezekana tupe recipe zingine za watoto tofauti tofauti
Mama Iqrah!!

KWA MASOMO ZAIDI JINSI YA UTUMIAJI TEMBELEA SEHEMU ILIYOANDIKWA BLOG ACHIVE CLICK KISHA NENDA KATIKA MAFUNZO YA MWEZI WA 2 ANGALIA TAR 3/2/2010 UTAONA MAFUNZO YA KUMSAIDIA MTOTO AU MTU MZIMA ASIEPENDA KULA KISHA ANGALIA MAFUNZO YA TAR 4/2/2010 UTAONA MAFUNZO YA DAWA YA MAFUA SAFI KABISA.

Monday, March 29, 2010

SEASON GREETINGS

TAR 2/4/2010 NI IJUMAA KUU NA TAR 4/4/2010 NI PASAKA JE UNAJUA VYAKULA MAALUMU KWAJILI YA PASAKA? KAA TAYARI KUPATA DONDOO ZA VYAKULA VYA JADI KWAJILI YA SHEREHE YA PASAKA.



Kwa wale wapenzi wapya wa blog hii ya chakua safi na salama, Blog hii ilianza rasmi tar 1/1/2010 kwahiyo kuna mafunzo mengi sana yameshapita angalia upande wa kulia wa blog katikati kuna neo limeandikwa Blog Archive bonyeza hapo kisha utaona tarehe za kila mwezi na aina ya chakula kilichofundishwa bonyeza jina la chakula kisha utapata mafunzo jinsi ya kutengeneza.

Mfano mafunzo ya mwezi wa kwanza kuna jinsi ya kutengeneza chapati na maandazi na mwezi wa pili kuan jinsi ya kutengeneza biriyani safi kabisa, croissant na vyakula vingi tu. Na mwei wa tatu kunamaelezo ya kutengeneza aina za vitafunwa, BBQ paryt na keki mabali mbali.

Kwa wale wote wenye matatizo ya uzito mkubwa muda si mrefu nitakua nimeshamaliza kuandaa somo la jinsi ya kutumia ratiba na aina ya chakula kitakacho kusaidia kupunguza uzitio iwe ni mwanamke au mwanaume inategemea kuna vyakula vyakupunguza uzitio na kuna vyaklula vya kupunguza kitambi pia.

Kumbuka hakuan cha rahisi duniani kikubwa ni kukazana na kufatilia mafunzo bila kuacha pia imenichukua muda sana kuandaa maana lengo ni kusaidia jamii nzima na kila mmoja afaidike kwahiyo vyakula hivi vitakua ni nafuu na upatikanaji wake ni rahisi kokote duniani.



POACHED SPIRAL FISH FILLET WITH TUMERIC SAUCE

CHAKULA HIKI NI SAFI NA SALAMA KWA WATU WASIOPENDA MAFUTA KABISA NA WASIOPENDA VITAMBI NA WANOTAKA KUDUMISHA UZITO WALIONAO USIENDELEE LADHA NA MUONEKANO NI SAFI SANA!


MAHITAJI

1 kilo Samaki fillet aina yeyote
400 gram karoti
400 gram spinach 
200 gram kitunguu

Kata kata mboga zote hizi kisha zichemshe katika maji yaliyochemka kwa dakika 5 kisha toa weka mafuta ya kupikia kidogo na chumvi ili kuweka ladha katika mboga na kufanya mboga yako ing'ae.


Kisha chukua chombeo cha duara kiwe cha chuma au plastiki yote sawa ili uweze kuishape mboga katika sahani.




Kisha pakua wali ulio katika umbo la duara tumia kikombe weka wali wako uliokwisha iva na kikombe kisiwe kikubwa sana kiwe na umbo la duara uswa na mduara wa mboga tayari uliokwisha tengeneza.





Baada ya kuweka wali mwisho unaweka samaki wako aliyechemshwa jinsi kuchemsha samaki.

chukua fillet ya samaki kisha ikate upana wa kidole gumba kwa urefu kisha izungushe iwe na umbo la duara na ichome na toothpick ili isfunguke kisha itumbukize kwenye maji yaliyochemka na kuchanganywa na mboga mboga kama kariti na kitungu na pili pili hoho pamoja na maji ya limao ili kuongeza ladha kwa samaki huyu chemsha kwa dakika 10 hadi 15 atakua ameiva.

Mtoe samaki na weka juu ya wali kama picha inavyoonyesha.


MAHITAJI YA KUTENGENEZA WHITE SAUCE



150 gram Unga wa ngano
200gram Blue band au butter
1/2 kijiko cha chai unga wa binzali au safron
1 lita maziwa
1 maji ya limao
1/4 kijiko cha chai kungu manga
2 mbegu za karafuu kavu
1 kikubwa kitunguu chop chop

JINSI YA KUTENGENEZA



weka blue band au butter katika kikaango au sufuria acha iyeyuke kiasi kisha weka kitunguu chop chop kaanga kilainike.
Kisha weka unga wa ngano koroga uchanganyike vizuri na mafuta kisha chukua mchapo wa chuma (Whisker) ili utumie kukorogea wakati unaweka maziwa.

Anza kumimina pole pole mziwa huku ukikoroga na mchapo mapaka upate rojo zito kabisa endelea kumimina maziwa mapaka upate rojo laini kabisa kama maziwa yamekuishia basi ongezea hata maji kiasi. kisha weka kungu manga, unga wa binzali kwa rangi nzuri au safron ya njao au ya orange  na karafuu kuongeza ladha safi kabisa.





Huyu ndie samaki alie kamilka sauce yake inawekwa mwisho kabisa baa ya samaki kupangwa unaweka katika umbo la duara kuzunguka chakua hicho mwisho kabisa juu unaweka kipande cha limao.

Furahia siku na familai yako.

Saturday, March 27, 2010

REDWINE CABBAGE, BBQ FISH NA PUMPKIN

WAJUA BOGA LINAPENDEZA SANA UKILA NA KABECHI ILIYOPIKWA NA MVINYO MWEKUNDU PAMOJA NA MSHIKAKI WA SAMAKI?




Menya vizuri boga na ulikate katika muonekano wa umbo zuri kama inavyoonekana katika picha. Lichemshe mapak liive ila lisibondeke kumbuka libaki na umbo lake zuri ili lipendeze katika sahani




Kisha weka kabechi yako katika sahani nyuma ya hilo boga.

Jinsi ya kuipika hiyo kabechi kwanza kata kata kabechi katika mkato mdogo mdogo kisha iweke kwenye maji na mvinyo mwekundu ( red wine) iwe ya kutosha ichemshe kwa masaa 4 mapak kabechi yote ibadilike rangi iwe nyekundu kumbuka pombe yote huyeyuka wakati unapika kitakachobaki ni harufu nzuri ya zabibu zilizosindikwa.



kisha panga mboga ziliizochomwa pembeni ya boga na kabechi




Unaweza pia kuipamba kwa stail hii weka kabechi chini kisha weka boga kwa juu kisha unafata mshikaki kumbuka maji yale yanayobakia wakati unachemsha kabechi yatumia kama sauce pembeni ya kulia boga na mshikaki wako safi wa samaki.


Kumbuka wakati unachemsha pombe yote inayeyuka hakuna kilevi chochiote kinachobakia chakula hiki ni salama hata mtoto anawezakula na akafurahia kabisa.

Jinsi ya kutengeneza mshikaki wa samaki angalia katika blog achieve utaona jinsi ya kuandaa BBQ party kisha fungua angalia jinsi ya kutengeneza aina tofauti za mishikaki.





Friday, March 26, 2010

CRUNCH FISH DIPPER

HAPA MWANAO AU MUMEO LAZIMWA AKUOMBE UIPIKE KILA BAADA YA SIKU MBILI NI NZURI SANA UNAKULA NA BBQ SAUCE NA TARTARE SAUCE PAMOJA NA POTATO BLOCKS HAINA MAFUTA UNAPIKA KATIKA OVEN KILA KITU NI SAFI NA SALAAMA KWA MLAJI MHHHH YAM YAM YAM!!!




Hivi ni vizi vya kawaida kabisa kata mikato mikubwa kupita kidogo said ta kidole iwe katika umboa la pembe nne kama tofali ( Block) kisha vipake mafuta ya kula kidogo na chumvi kisha viweke kwenye oven mafuta yanasaidia viive na rangi nzuri pia visishike kwenye tay uliyobekia.


 Huu ni muonekano wa fillet ya samaki ikate nayo katika muonekano kama kwenye picha umbo la urefu wa kidole na upana pia. Kumbuka kuiwekea viungo samaki yako maji ya limao au vinega pamoja na tangawizi na kitunguu swaumu kilichosagwa na chumvi.



Kisha chovya kwenye unga wa ngano kipande hicho cha samaki kung'uta unga huo kisha chovya kwenye mayai yaliopigwa



ukishatoa katika mayai weka kwenye unga mkavu wa mikate hakikisha samaki wako ameenea unga wa mikate pande zote safi kabisa. ( jinsi ya kuandaa unga wa mikate chukua vipande vya mikate kisha weka kwenye oven mapaka mikate yote iwe ya kahawi isiungue kisha itoe tumia kwaruzo au greater kwaruza na utapata unga huo safi kabisa na utaweza kutumia kupikia vyakula vingi tu)



Huu ni muonekano safi kabisa wa samaki wako baada ya kuwatia unga wa mikate safi kabisa wachukue na kuwaweka katika oven kwa dakika 15 - 20 inategemea na moto wa oven yako



Kisha watoe na chukua brush wapake mafuta ya kula kidogo sana ili kusaida kuleta rangi nzuri na harufu nzuri na kulainisha samaki yenyewe pia. kisha rudisha kweney oven kwa dakika 3 - 5  kisha toa tayari kwa kuliwa.



Huu ni muonekano wa viazi vyako tayari vikiwa vimeisha iva  baada ya kuviweka katika ovena pia kwa dakika 15 - 20 vitoe tayari kwa kuliwa.



Panga katika sahani yako kwa staili hii kama huna kile kibakuli kidogo cha kuongezea utanashati maana kumbuka watoto wanapenda sana kula vitu vilivyonakshiwa huu ni mtego tosha wa kumnasa mwano asie penda kula vyakula vikavu watoto wanapenda sana sana.



Unaweza kula samaki huyu akiwa na BBQ sauce zinauzwa madukani ni nafuu sana, pia na tartare sauce



Furahia chakua hiki na familai yako weekend hii





Thursday, March 25, 2010

WASHANGAZE FAMILIA KWA KIPAPATIO CHA KUKU NA NYAMA YA NG'OMBE

CHAKULA HIKINI KIZURI SANA KWANI UNAPATA LADHA YA NYAMA MBILI KWA WAKATI MMOJA NA NIRAHISI SANA KUANDAA.





Kata kipapatio cha kuku kama inavyoonekana kwenye picha



Hiki ndio kipapatio cha kuku




Kikate tena nusu kama kinayooneka katika picha





Kisha kata mwisho kabisa wa ncha ya mfupa ili uweze kuimenya nyama iachane na mfupa



Hiki ni kipapatio kikiwa tayari kwa kuokwa katika oven kipake kitunguu swaumu na tangawizi,chumvi na mafuta ya kupikia kidogo kisha kiweke kwenye oven kiive



Katika sahani weka viazi vya kusagwa ( mush potato) jinsi ya kutengeneza chemsha viazi ulaya katika maji na chumvi mpaka viive kabisa viwe laini kisha viponde kwa mchapo wa chuma weka kungu managa kidogo na maziwa ya maji na siagi kidogo.



Katika picha huo ni muonekano wa sahani tayari ikiwa na viazi vya kusagwa na mboga zilizochomwa na nyama ya ngombe iliyokatwa vipande vidogo ikaangwa mapka ikaiva kisha ikawekewa mchuzi mzito wa nyanya unakaanga tena mpaka ukauke kabisa katika nyama.




Kisha toa vipapatio katika oven na uviweke juu ya nyama iliyokwisha kaangwa



Huu ni muonekano safi wa mchanganyiko wa kipapatio cha kuku na nyama ya ngombe ya kukaanga pamoja na viazi ulaya vya kusaga.



Wednesday, March 24, 2010

JINSI YA KUPIKA MACARONI, PEENE PASTA AU SPAGHETI

CHAKULA HIKI NI KIZURI SANA NA NIRAHISI SANA KUPIKA HUTUMIA MUDA KIDOGO SANA WA MAANDALIZI NA GHARAMA NAFUU. SIO WATU WAZIMA TU HATA WATOTO HUPENDA SANA KULA CHAKULA KITAMU NA CHENYE MUONEKANO WA TOFAUTI UNAWEZA PIKA KWA MTINDO HUU AINA YEYOTE ILE YA PASTA.




Hii ni white sauce mahitaji na jinsi ya kutengeneza angalia chini mwisho wa picha.


Hii ni penne pasta ichemshe katika maji yaliyo chemka weka chumvi na mafuta ya kupikia kidogo yasaidie zisishikane wakati unachemsha pia kumbuka kuzikorogo koroga wakati unachemsha.


Ukisha chemsha kwa dakika 7 hadi 10 zitoe katika maji zisiendelee kuiva lazima uwe umeshaanda white sauce yako safi kabisa ziweke kwenye sahani



Kaanga kitunguu kasi kilainike vizuri kumbuka kuweka na chumvi kidogo



Kisha mwagia juu ya pasta hiyo white sauce mhhhh inapendeza safi sana


Kisha juu yake weka vitunguu vya kukaanga mhhh inaharufiu safi sana na ni tamu kweli kweli unaweza fanya mchanganyiko wa mboga kama karoti na pilipili hoho na kitunguu au ikabaki kitunguu peke yake yote sawa.




MAHITAJI YA KUTENGENEZA WHITE SAUCE

150 gram Unga wa ngano
200gram Blue band au butter
1 lita maziwa
1/4 kijiko cha chai kungu manga
2 mbegu za karafuu kavu
1 kikubwa kitunguu chop chop

JINSI YA KUTENGENEZA
weka blue band au butter katika kikaango au sufuria acha iyeyuke kiasi kisha weka kitunguu chop chop kaanga kilainike.



Kisha weka unga wa ngano koroga uchanganyike vizuri na mafuta kisha chukua mchapo wa chuma (Whisker) ili utumie kukorogea wakati unaweka maziwa.



Anza kumimina pole pole mziwa huku ukikoroga na mchapo mapaka upate rojo zito kabisa endelea kumimina maziwa mapaka upate rojo laini kabisa kama maziwa yamekuishia basi ongezea hata maji kiasi. kisha weka kungu manga na karafuu kuongeza ladha safi kabisa.



WAJUA KUTENGENEZA SUPU YA MAHINDI MABICHI YA NJANO??

MUMEO AU MTOTO ANASUMBUA KULA?? HAHAAAA HAPA NDIO PA KUMKAMATA USIMLAZIMISHE MTOTO UJI MTENGENEZEE SUPU HII OHHHH ATAIPENDA NA ATAKULA SANA SANA.

MUMEO MTENGENEZEE ANYWE KABLA YA CHAKULA OHHH LAZIMA AKUSIFIE SANA NA HATAKUA NA KISINGIZIO TENA KWANINI ASILE NYUMBANI NA ATAWAHI KURUDI NYUMBANI AKIJUA MLO SASA UKO MAHALA PAKE

KWA HOTELINI SUPU HII ITAKUA NI GUMZO KWA WATEJA WAKO NA TEGEMEA MGAHAWA WAKO KUA MAARUFU KWAJILI YA SUPU HII

MAHITAJI

1 kopo mahindi mabichi ya njano
200 gram karoti
100 gram kitunguu
150 gram leeks
1 lita maziwa
150 unga wa ngano
100 gram blueband au butter( siagi)




Hii ndio picha leeks inavyoonekana sokololote lile ukienda mjini utazipata kwa urahisi sana na kwajina hili hili



Mchanganyiko wa mboga zikate katika umbo dogo sana karoti, kitunguu na leeks.


Haya ni maindi mabichi ya njano ndani ya kopo kama umelima mahindi haya sio vibaya ukitumia fresh ila sio makavu.



Maziwa katika bakuli ukiwa umeshaanda na mchapo kwajili ya kukorogea


Weka mafuta na mchanganyiko wako wote wa mboga kweny sufuria



Hapa tayari mboga zimeisha iva na hazijaungua kumbuka wala hazina rangi ya kahawia



kisha weka unga wa ngano ndani ya sufuria yenye mchanganyiko wa mboga





koroga vizuri unga ushikame na mboga zote


kisha mimina maziwa kidogo kidogo kumbuka kukoroga kwa kutumia mchapo koroga kwa kasi bila kuachia ili mchanganyiko wako uwe sawa na usiweke madonge madonge ya unga



Baada ya kukoroga maziwa yote na kupata mchanganyko safi na mzito weka aromati ( inapatikana kwa urahisi sana duka lolote liel la chakula na nirahisi sana) inaladha safi sana na huna haja ya kuweka chumvi ukitumia kiungo hiki mhhhh!!!



Mwisho kabisa mimina mahindi yote na kopo libaki tupu acha ichemke vizuri kwa dakika 5 hadi 7 kisha itakua tayari kwa kunywewa ikiwa yamoto.


Huu ni muonekano wa supu ikiwa imepambwa vizuri katika bakuli na jani la minti na vipande viwilivya nyanya muonekano tu ni kigezo cha kumvutia mnywaji ukiacha ladha safi sana ya supu hii.

Kwa mtu mzima au mtoto aliepoteza uzito atarudisha uzito wake haraka sana, na kwa mtoto ambaye hajaanza kula vyakula vigumu baada ya supu hii kuiva iweke kwenye blenda na msagie mwanoa ohhhhh jamani atakunywa na yeye ndio atakua anakukumbusha mama ile supu tamu bado haijaiva tu ????

FURAHIA NA FAMILIA YAKO PAMOJA NA WATEJA WAKO.