CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Thursday, August 22, 2013

NAOMBA KURA ZENU KATIKA SHINDANO LA BLOG BORA YA CHAKULA TANZANIA 2013

WAPENZI WA BLOG HII NAOMBA KURA ZENU NDUGU ZANGU MAELEZO ZAIDI YAPO HAPO CHINI NA YANAELEWEKA VIZURI


Jinsi ya kupiga kura

1. Itafunguka ukurasa na kuonyesha website husika ya kwanza kabisa inasema vote for Tanzania best food blog hiyo hiyo fungua . 

2. Kisha utafunguka ukurasa mwingine ukisema PIGA KURA YAKO KUCHAGUA BEST FOOD BLOG bonyeza tena hapo

3. Kisha itafunguka ukurasa wenye majina ya blog zote zinazoshindana blog yetu ya active chef ni yakwanza kabisa bonyeza kiduara cheusi upande wa kushoto ilikuichangua na kisha piga kura yako tukufu tushinde mtu wangu.
 
 
 

NAWASHUKURU SANA WAPENZI WOTE WA BLOG HII YA CHAKULA BORA NA SALAMA

JIFUNZE KUTENGENEZA WALI WA MCHANGANYIKO WA NYAMA YA KUKU NA CHEESE

 
JIFUNZE KUTENGENEZA WALI WA MCHANGANYIKO WA NYAMA YA KUKU NA CHEESE
 
MAHITAJI
4 vifua vyakuku (kata kata vipande vidogo)
 360 gram ya maji
5 gram kitunguu swaumu
1 kijiko kikubwa cha chakula graham masala
1 nyanya ya kopo
500gram sawa na nusu kilo ya mchle
240 gram shredded cheddar cheese
1 kopo la mtindi halisi usio na ladha
1 parachichi au avocado safi lilioiva
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAEEZO HAPOCHINI
 
 
 
Weka kikaango katika jiko kasha pata moto wa kutosha mwagia vipande vya kifua cha kuku na kasha weka kitunguu swaumu, chumvi, pili pili manga na kama unamajani ya giligilani au parsley mwagia kuongeza ladha zaidi ila sio lazima na mafuta ya kukaangia.

 
Endelea geuza geuza isishike chini na kuungulia ndani ya dakika 5 tu itakua imeshaiva kabisa

 
Kisha mimina maji kwenye kikaango ay sufuria, weka graham masala kasha weka nyanya ya kopo na mwisho miminamchele na koroga vizuri funikia chakula kiendelee kuiva.

 
Hakikisha umefunika vizuri chakula kiendelee kuiva pole pole nivizuri kabla maji hayajakauka ukaonja chumvi na kuongezea

 
Hapa maji yote yameshakauka na wali wetu na mchanganyiko wa kuku umeshaiva safi kabisa

 
Wali bado ukiwa wamoto mwagia cheese kwa juu itayeyuka mara moja na kutengeneza mvuto kwa macho na harufu safi sana na ladha ya kipekee mdomoni

 
Ukichota wali kwa chini huu ndio muonekano wake

 
 Baada ya kupakua unaweza mwagia juu mtindi pamoja na parachichi na ukaendelea kufaidi zaidi na family yako.
 


Monday, August 19, 2013

JIFUNZE KUTENGENEZA KUKU WA KUKAANGA PAMOJA NA CHEESE NA SAUCE SAFI

 
KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA YA KUKU HUYU WA KUAANGA PAMOJA NA CHEESE NA UNGA WA MIKATE
 
MAHITAJI
 
240 gram shredded Parmesan cheese
3 vifua vya kuku
480 gram unga wa mkate wa kahawia au bread crumbs
300 gram mtindi uliochanganywa na 100gram vitunguu swaumu vingi, limao, pili pili mbuzi, asali na soya sauce kidogo
1 lita ya mafuta kwa kukaangia
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
 
JINSI YA KUANDAA FATILI APICHA NA MAELEZO HAPO CHINI 
 
 
Jinsi ya kukaausha unga wa mikate unatakiwa kuweka katika oven au kwenye jiko la mkaa na unatakiwa kua makini isiungue iwe ya kahawia tu kish saga katika blenda na  chekecha upate unga safi na laini.

 
Katik picha kushoto ni mchanganyiko wa mtindi ya kitunguu swaumu cha kutosha na kulia ni unga wa mikate kumbuka kuchanganya humo chumvi na pili pili manga.


 
Hatua za maandalizi kwanza chukua kifua cha kuku na kasha kata vipande vya wastani mfano katika picha hapo juu. Chukua vipande hivyo na chovya katika mtindi halafu chovya katika unga wa mkate hakikisha unga wa mkate unapakaza kote safi kabisa.
 

 
Weka mafuta katika kikaango yapate moto wa wastani ikiwa ya moto sana itaungua.

 
Tupia vipande vyakuku katika kikaango na enelea kukaanga

 
Hakikisha unakua makini kugeuza ili isiungulie  hii itatokana na ubora wa kikaango chako au moto ulioweka kwajili ya kukaangia.

 
Hakikisha rangi iwe safi y kahawia ili kukuwako abaki na ladha safi asiungue. Chakula hiki unaweza kula kama mlo kamili nyumbani au unaweza wafungashia watoto wakiwa wanakwenda shule wakala hata ikiwa imepoa badoinakua na ladha safi sana hasa ukila na salad.