CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Sunday, December 5, 2010

JIFUNZE KUTENGENEZA SALAD HALISI AINA YA KACHUMBARI


UHALISIA WA SALAD HII UNATOKEA INDIA IKIWA INAJULIKANA KWA JINA MAARUFU LA Kachumber HAPO ZAMANI ILIKUA INATENGENEZWA KWA MCHANGANYIKO WA KITUNGUU TU NA MAGANGO KWA LUNGHA YA KIHINDI NENO Kachar ni mbichi au haijapikwa RECIPE RAHISI NA SAFI KABISA


MAHITAJI

1 kitunguu kikubwa kata slice nyembamba sana
1 Tango kubwa, menya na katakata
1 au 2 pili pili mbichi (Sio lazima ingawa inaongeza ladha safi sana)
2 Nyanya kubwa za kuiva, Kata kata
1/2-kijiko kidogo cha chai cumin powder (sio lazima)
2 limao kamua kisha hifadhi maji yake
5 gram Pili  pili manga
5 gram chumvi
1 fungu la gili gilani kwa kupambia na kuongeza ladha


JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAFUNZO HAPA CHINI



Kata kata mboga mboga zote weka katika bakuli moja kisha kamuli maji ya limao.



Kisha weka unga wa cumin,chumvi na pili pili manga.
 


Kisha chuku mwiko wa mbao au kijiko cha chakula na koroga vizuri ichanganyike.  Onja uone kama viungo vimekolea. Kisha funika salad yako na weka katika friji. Kuweka katika friji inasaidia salad yako ipoe na viungovyote viingie vizuri na kukolea katika salad.



Mpatie mlaji ikiwa yabaridi. Unaweza kula na chakula chochote wengi hupendeea kula na nyama choma.




HUU NI MUONEKANOSAFI KABISA WA KACHUMBARI YETU RAHISI NA TAMU KWA LADHA HALISI.



3 comments:

Anonymous said...

Issa siku hizi umekuwa mvivu wa kutuandikiarecipe unaniudhi

Anonymous said...

Jamani maelezo ya wapi Issa wewe? au ni tatizo la kiufundi..???

Anonymous said...

nataka kutengeneza cake ya bday tar 20 feb unaweza kunitengenezea? my email is pendo_ptr@yahoo.com nijulishe na unipe bei pls