CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Wednesday, January 26, 2011

JIFUNZE KUTENGENEZA MKATE HUU AINA YA PUTO


MKATE HUU NI MWEPESI SANA NA UNAVIMBA UNAKUA KAMA PUTO KIASI FLANI UNAPENDEZA KWANI UNAKUA KAMA MKATE WA MAAJABU KAA TAYARI KWA RECIPE SOON.

MAHITAJI

240 gram unga wa ngano
1/4 chumvi kijiko kidogo cha chai
120 gram za maji (Usiweke maji yote inaweza zidi hii hutegemea na kiwango cha unga weka maji kidogo kidogo)




Changanya unga na chumvi katika bakuli


Weka maji katika unga kidogo kidogo endelea kukanda


Kanda pole poel mpaka unga wote uchanganyike. Hakikishs maji unaweka kidogo kidogo mpaka unga wote uchanganyike maana kiasi cha maji kitahitajika kutokana na kiwango cha unga. Pia unaweza ongezea kijiko kimoja cha mafuta moto uliyochemsha kwajili ya kuongeza ladha na ubora na uendelee kukanda na mchanganyiko wako usiwe laini sana wala mkavu sana uwe wastan.


Kanda vizuri kwa mara ya mwisho mchanganyiko wako uwe kama unavyoonekana katika picha.


Kisha kata vipande vidogo na zungusha miduara kama inavyoonyesha katika picha ukubwa wa miduara utategemea na ukubwa wa kikaango chako. Hakikisha hupotezi muda kata na sukuma haraka haraka kisha choma ili mkate wako utoke vizuri.


Sukuma kwa saizi ya wastani kama inavyonekana katika picha. Usisukume nyembamba sana zitakakamaa sana na hazitakua nzuri.


Hakikisha unarudia kwa kila miduara yote iliyobaki. Wakati huo huo hakikisha mafuta yanamoto na uanze kukaanga mkate wako.



Kata kipande kidogo cha unga na tupia katika mafuta kuangalia kama mafuta yamepata moto kama mafuta yanamoto kipande hicho kitachemka na kuja juu haraka. Mafuta yawe yamoto lakini sio moto wa kutoa moshi yataunguza mkate wako. Kama ukiweka kwenye mafuta ambayo hayana moto mkate wako utabaki flat na hautavimba na utameza mafuta hautakua mzuri tena.


Baada ya kuhakikisha mafuta yanamoto sasa tupia mkate katika mafuta.


Wakati mkate unapanda juu, Hakikisha unaendelea kumwagia juu ya huo mkate mafuta inasaidia uweze kuvimba.


Kumwagia mafuta inasaidia sana unaona sasa mkate umeshavimba na kupendeza.


Hakikisha una geuza geuza mpaka upate rangi nzuri unayoipenda wewe kahawia ya kawaida au kahawia ya udhurungi.

Weka katika paper towel ili ichuje mafuta. Kama ulikaanga vizuri haita meza mafuta na utakua mzuri sana sana.


Unaweza mpatia mlaji mkate huu na aina yeyote ya chakula utakachopenda au anachopenda. Unaweza mpatia mlaji mkate huu pamoja na Potato Masala (masala ya viazi ulaya) au njegere za nazi. Pia inapendeza sana kusave na sauce za aina mbili mint sauce na tamarind sauce ( Mchuzi wa ukwaju).



MKATE HUU UNAWEZA KULA KWA CHAKULA NA MCHUZI WA AINA TOFAUTI ANGALIA MUONEKANO MZURI WA MKATE HUU KATIKA PICHA TENGENEZA FAMILIA YAKO IFURAHIE SIO KAZI NGUMU.



8 comments:

Anonymous said...

i love this blog

Mariam.

MILKA said...

Halow tupe hicho kitu mapeme lieo na mapishi ya unga wa mchele tuinjoy kesho week edn Ahsante saaaaaaaaaaana mie najifunza mapishi kutoka katika blog yako BIG UP

Anonymous said...

tuambie mahitaji tukitaka kuupika mkate huo

Anonymous said...

Kaka shida ni muda au hivyo vitu ni vigumu sana kupika ni wiki sasa tunahamu!!!!

Friend

Anonymous said...

kaka Bado umetoa vitu nusu nusu huo mkate wa PUTO hujamaliza tunafanyaje uwe umekamilika

Anonymous said...

Wahindi huita huu mkate PULL.
mama yangu alinifundsha kutumia maji ya dafu kama unataka uzidi kuwa na ladha nzuuuri na pia ukishaukanda unaweza kuufunika kwa plasticfoil hewa isipite, uuuh ukija kusukuma na kuchoma utapenda mwenyewe!!

ni mkate wa rahisi na haraka sana kutengeneza. Asante kaka Issa.

tweety

Anonymous said...

Mee too, looh!

Anonymous said...

kaka naipenda sana blog yako, naomba utufundishe jinsi ya kupika biliani. yaani natamani sana kujua hicho kitu.