CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Thursday, March 17, 2011

WAPENZI WA PASTA NA NOODLES HIKI HASA NDIO CHAKULA CHENU

WAPENZI WA KUPIKA BIRIYANI ANGALIA MWISHO KABISA CHINI YA BLOG UTAONA RECIPE SAFI YA BIRIYANI

 PIA KAA TAYARI KW AMAFUNZO YA KUPIKA NOODLES HIZI KWA KUTUMIA MBOGA MAJANI

MAHITAJI

1 paketi ya noodles au spaghetti

1 kitunguu maji kata slice
360 gram ya mushrooms ( uyoga) kata slice
2 Tangawizi mbichi kata slice nyembamba sana
 5 gram kitunguu swaumu
1 fungu la spinach
150 gram njegere zilizochemshwa
1 pili pili hoho kata vipande vidogo
2 kijiko kikubwa cha chakula Oyster sauce
5 kijiko kikubwa cha chakula soy sauce
2 kikiko kikubwa cha chakula sesame oil ( mafuta ya ufuta)



JINSI YA KUPIKA FATILIA PICHA NA MAFUNZO HAPO CHINI


Andaa noodles kama maelezo yanavyosema katika paketi. Kawaida huwa nachemsha pamoja na chumvi kisha nachuja maji ya moto na ninazipoza katika maji baridi baada ya kuiva. Kisha nazichuja tena na kuzikausha kisha naweka mafuta ya ufuta kijiko kimoja ili kufanya zisishikane.




Hakikisha wakati umemaliza kuchemsha noodles au spagheti mboga majani zote uweme umeshaanda na kuzilkata kwani tunaanza kupika kwa moto mkali sana na kwa haraka. Katika kikaango weka kijiko kimoja cha mafuta ya ufuta kisha weka moto mkali sana yapate moto kisha ongeza kitunguu swaumu, tangawizi na kitunguu maji.




Vitunguu vikishaiva ongeza pilipili hoho na mushrooms




Hakikisha pilipili hoho zinaiva kiasi tu na kutoa harufu nzuri zisipondeke kisha weka majani ya spinach na endelea kukaanga.




Majani ya spinach yakishapata moto na kuanza kulainika weka noodles pamoja na njegere.


Kisha weka soy sauce na oyster sauce haraka haraka hakikisha unachanganya noodles zako zichanganyike pamoja na sauce na mboga majani.




Kisha toa chakula chako katika moto na muhudumie mlaji haraka. Kuongeza ladha zaidi unaweza weka chilli sauce au tomato ketchup.



CHAKULA HIKI NI RAHISI KUPIKA PIA NI NAFUU KWA GHARAMA YA MANUNUZI PIKA CHAKULA HIKI FAMILIA YAKO IFURAHIE TOFAUTI YA MAPISHI.



3 comments:

Anonymous said...

How come, hakuna maelekezo ya kupika na pia hakuna maelezo ya vitu vya kupikia. Dont cut corner bro, tunahitaji maelezo

Anonymous said...

Hapo sawa kaka, nashukuru.. sasa? kitabu chako cha mapishi kinatoka lini? kiwe kwa lugha hii tafadhali? ahsante.

emu-three said...

Shukurani kwa utaalamu huu wa mapishi!