KAA TAYARI KWA KUJIFUNZA KUTENGENEZA KEKI HII YENYE LADHA YA MAEMBE NA MTINDI HALISI.
MAHITAJI
360 gram unga wa ngano
1 kijiko kidogo cha chai Baking Powder
1/2 kijiko kidogo cha chai chumvi
1 kijiko kidogo cha chai tangawizi ya unga
60 gram siagi isiyo na chumvi (Unsalted Butter) au blue band
60 gram Vegetable Oil (mafuta ya mahindi au ya olive )
240 gram sukari
4 ute mweupe wa mayai
100 ml Mtindi halisi (Natural Yogurt)
1 kijiko kidogo cha chai vanilla essence
60 gram juisi nzito ya maembe
1 limao kwaruza upate chenga chenga ( Zest)
360 gram unga wa ngano
1 kijiko kidogo cha chai Baking Powder
1/2 kijiko kidogo cha chai chumvi
1 kijiko kidogo cha chai tangawizi ya unga
60 gram siagi isiyo na chumvi (Unsalted Butter) au blue band
60 gram Vegetable Oil (mafuta ya mahindi au ya olive )
240 gram sukari
4 ute mweupe wa mayai
100 ml Mtindi halisi (Natural Yogurt)
1 kijiko kidogo cha chai vanilla essence
60 gram juisi nzito ya maembe
1 limao kwaruza upate chenga chenga ( Zest)
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
Muda wa kuandaa : Dakika 30
Muda wa mapishi : dakika 30 mpaka saa 1
Idadi ya walaji : Watu 3
Washa oven iwe na joto la170C (350F). Paka siagi tray yako ya kuokea keki. Weka unga wa ngani kwenye bakuli pamoja na baking powder, chumvi na Tangawizi ya unga kisha weka pembeni.
Changanya zest za limao pamoja na sukari
Kanda kwa mikono ili iweze kuchanganyika.
Kisha chukua bakuli lenye sukari, siagi na mafuta ya olive au ya mahindi.
Kisha chukua bakuli nyingine weka ute mweupe wa mayai piga pamoja na vanilla mpaka itoe povu.
Kisha chukua mchanganyiko wa mayai piga pamoja na mchanganyiko wa sukari na siagi.
Baada ya kuchanganya vizuri kisha chukua yogurt na mwiko koroga pole pole mpaka ichanganyike vizuri
Kisha mimina unga pole pole na changanya kwa kutumia mwiko
Koroga mpaka uchanganyike vizuri kabisa endelea kuongeza mtindi mpaka upate mchanganyiko mlaini na mzito kwa ajili ya keki
Kisha ongezea mchanganyiko wa maembe na endelea kuchanganya vizuri.
Kisha mimina mchanganyiko wako kwenye tray ya kuokea na choma kwa dakika 50 mpaka 60.
Baada ya hapo hakikisha unachoma inakua na rangi safi ya kahawia. Kuiva kwa keki yako itategemea na aina ya kikaango ulichotumia na aina ya oven ukliookea mimi huwa nachoma kwa dakika 35 tu na inaiva.
Acha keki ipoe katika kikaango kwa dakika 5 mpaka 10 kisha toa na weka katika sahani tayari kwa kuliwa.
Ukiikata kwa ndani inakua laini safi kabisa na muonekano kama huo.
Unaona keki hii ilivyochambuka?
Ubora wa keki unategemea mchanganyiko mzuri, na muonekano wa keki inategemea na aina ya kikaango unachotumia.
NI NAFUU NA RAHISI KUTENGENZA WAANDALIE FAMILIA WAFURAHIE
2 comments:
CAKE INAVUTIA HADI RAHA, NATAMANI NINGEIPATA MDA WA KUFTURU.
SASA KAKA ISSA UNAONAJE KAMA UNGETUPA RECIPE ZA FUTARI, INGAWA NIMECHELEWA KUULIZA, ILA INGEKUA BOMBA SANA, UNGEKUA NA HOTELI HAPA BONGO VILE AMBAVYO SIWEZI KUPIKA NINGEKUJA KU ORDER HOTELINI KWAKO, MANA VYAKULA VYAKO VINAVUTIA SANA
FUNGUA FOOD PLACE AISEE, uko juu sana. keep up the good work
Yakhe, uki-google 'mapishi ya futari' utapa post nyingi tu, kutoka website nyingi tu.
Post a Comment