UMECHELEWA KUTOKA KAZINI NA UMETAMANI KUPIKA BAMIA JIFUNZE NJIA HII RAHISI NA NYEPESI YA KUPIKA KWA UBORA NA LADHA SAFI KABISA
MAHITAJI
500 gms bamia mbichi (Ladiesfinger)
2 vitunguu vikubwa kata slice
1 kijiko kidogo cha chai tangawizi iliyosagwa
1 kijiko kidogo cha chai kitunguu swaumu kilichosagwa
1 kijiko kidogo cha chacumin binzali nyembamba
1/2 kijiko kidogo cha chai unga wa manjani (turmeric)
1 kijiko kidogo cha chai unga wa giligilani -(coriander powder)
1 kijiko kidogo cha chai unga wa pili pili (chilli powder)
1/2 kijiko kidogo cha chai juisi ya limao (lemon juice)
1/21 kijiko kidogo cha chai Garam Masala
5 gram chumvi
MUDA WA MAANDALIZI
Muda wa kuandaa : Dakika 30
Muda wa kupika : Dakika 30
Idadi ya walaji : Watu 2
JINSI YA KUANDAA FATILIA MAFUNZO HAPA CHINI
Osha, safisha kisha kausha bamia zako. Kisha kata ncha za mwisho na ukate tena kugawanyisha mara 2 kama uonavyo katika picha.
Katika kikaango cha moto weka 1/2 kijiko kidogoc ha chai mafuta ya kupikia, kisha ongezea binzali nyembamba. ikishakua ya brown, ongezea kitunguu maji kilichokatwa, pamoja na tangawizi na kitunguu swawumu cha kusagwa pamoja na chumvi. Endelea kukaanga mpaka vitainike.
Kisha weka bamia, hakikaisha hapa unaongeza moto uwe mkali kabisa na kaanga haraka ili bamia ichanganyike na viungo na kitunguu. Kisha punguza moto na acha bamia ichemke kwa dakika 5.
Chakula hiki kinakua tayari tu pale bamia zinapokua laini baada ya kupikwa kwa dakia 15 hadi 20..
HAzitakua rojo rojo zitakua na ugumu wa wastani (crunchy) na ni laini kwa mlaji. Just the right bite to it. Kabla ya kutoa unaweza ongeza moto na ukamalizia kiungo cha mwisho juisi ya limao na garam masala, koroga vizuri na kisha mpatie mlaji na Chapati pamoja na wali.
CHAP CHAP UNAANDAA
CHAP CHAP IMEIVA
CHAP CHAP UNAKULA
8 comments:
Ahsante maana nilikuwa juzi tu nimekutana na bamia dukani nikanunua nitajaribu mpiko huu.
No idea what you say on the blog, but love your dishes, I am just cooking off the photos!!!Keep it up, great blog
ndugu yangu mbona naona imekuwa kavu sana je nikiongeza nyanya na roiko mchuzi mix yaweza kuwa nzuri nikalia ugali?
Rose
duh bamia nimezipika zimenogaje asante sana chef.halafu please soma emails zako chef
huwa sipendi bamia lakini leo nimezikung`yata hatariiiii.shurani sana chef
MHH HIYO KWELI NI CHAP CHAP, BIG UP BROZ
asante kwa kunifundisha mapishi ya bamia unanikumbusha sanga mwalugesha
duh umentamanisha,leo naenda pika hii chakula yani na ugali wa udaga+mahindi
kweli waafrika tuna vyakula
Post a Comment