CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Wednesday, January 25, 2012

JIFUNZE KUPIKA PANCAKE YA MBOGA MAJANI


RECIPE YA PANCAKE NA MBOGA MAJANI

MAHITAJI

480 gram unga wa ngano
120 gram maziwa ya maji
5 gram chumvi
50 gram sukari
2 mayai ya kuku
50 gram mafuta ya maji

1 kitunguu kikubwa katakata vipande vidogo
1 nyanya kubwa katakata vipande vidogo toa mbegu za ndani2 pili pili mbichi kata kata vipande vidogo (sio lazima)


majani ya gili gilani kwajili ya kupambia


JINSI YA KUANDAA FATILIA MAFUNZO NA PICHA HAPO CHINI

Muda wa kuandaa : Dakika 15

Muda wa kupika : Dakika 15
Idadi ya walaji : Watu 2
Idadi ya pancake : Kiasi cha 4 mpaka 6



Chukua unga, sukari, chumvi, maziwa, na mafuta ya maji pamoja na mayai changanya kwa pamoja kwa kutumia mchapo kisha weka pembeni unga wako, Kisha katakata pilipili, nyanya na kitunguu kama uonavyo katika picha.



Chukua kikaango kisha weka mafuta kiasi na sambaza vizuri kisha pata moto mimina kati kati ya kikaango unga wako na usambaze uenee kwenye kikaango chote.



Hakikisha unga ni wakutosha katika kikaango ili pancake yako iweze kua nene na mboga majani ziweze kutosha iache iive kwa dakika 3 kwa moto wa wastani, Ikishaanza tu kutoa kama mapovu kwa juu kuonyesha dalili ya kua itakua imeiva chini na inaendelea kuchemka kwa juu basi tupia vipande vya nyanya, korienda na kitunguu kisha geuza chini kuwe juu.



Baada ya kuigeuza utaona rangi ya kahawia upande ule uliokua chini inamaa imeshaiva upande wa kwanza pia upande wa pili ambao unamboga pika kwa dakika 3 na kisha toa itakua imeiva pia unaweza mwagia mafuta kiasi kw apembeni ili yaingie chini ya pancake yako na isiweze kuungua na kushika katika kikaango.



Baada ya dakika 3 itoe itakua imeiva na itakua na harufu safi sana ya kuvutia hakikisha unamapatia mlaji ikiwa yamoto.



Pancake hii unaweza kunywa na chai asubuhi au jioni saa 10 kama kitafunwa tu cha kawaida. Pia unaweza kula kama mlo kamili kwa mchana au usiku pamoja na chuzi wa nyama samaki au hata maharage ya nazi na familia ikafurahia sana sana.

No comments: