CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Saturday, December 29, 2012

JIFUNZE KUTENGENEZA KEKI HII NDOGO YA MCHANGANYIKO WA CREAM NA MATUNDA FERSH

 
KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA YA KEKI HII NGUMU NA MCHANGANYIKO WA MATUNDA NA CREAM
 
MAHITAJI
  MAHITAJI YA KUPAMBIA
2 kg matunda ya Strawberries
6 Kijiko kikubwa cha chakula Sukari
500 gram Whipped Cream
  MAHITAJI KWAJILI YA KEKI
  500gr Unga wa ngano
  5 Kijiko kikubwa cha chakula Sukari
  1 Kijiko kikubwa cha chakula Baking Powder
  1/2 Kijiko kidogo cha chai Salt
  8 Kijiko kikubwa cha chakula unsalted Butter ya baridi
  1 Yai kubwa, Piga piga
  1 Kijiko kikubwa cha chakula maziwa ya maji
  1 yai ute mweupe, piga piga
                           JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi : 30 dakika mpaka saa 1
Muda wa mapishi Dakika 15
Idadi ya walaji : Watu 6
Idadi ya keki : Utapat 6 mpaka 8  Shortcakes

 
Toa vikonyo katika matunda ya strawberries.

 
Chukua robo tatu ya matunda ya strawberries weka katika bakuli safi kisha ponda ponda kwa kutumia potato masher.

 
Ponda ponda mapaka upate mchanganyiko laini na safi kabisa. Hii itasaidia kuunganisha shortcakes pamoja.

 
Kisha katakata nusu kwa nusu matunda yaliyobakia.

 
Kisha tupia matunda katika mchanganyiko ulioponda ponda pia changanya na sukari. Kisha changanya pole pole na uiache ipoe kwa dakika 30.

 
Wakati unaendelea, Chukua oven rackiweke mstari wa chini kabisa na uwashe oven kwa joto la nyuzi  425 F. Katika bakuli changanya, unga, 3 Kijiko kikubwa cha chakula sukari, baking powder na chumvi.

 
Kisha kwangua butter kwenye unga. mimi na kwangua hii siagi kwakua natumia mikono kukandai lakini kama unatumia food processor, basi kata vipande vidogo vidogo, Kama unatumia mikono kanda mapaka ichanganyike na kama unatumia mashine basi washa ichanganye mpaka ichanganyike vizuri.


Mimi pia natumia njia nyepesi ya whisk kwajili ya kuchanganya butter na unga

 
Huu ni muonekano baada ya kuchanganyika vizuri.

 
Kwenye bakuli nyingine tumia measuring cup, Changanya mayani yaliopigwa pigwa na maziwa.

 
Kisha changanya unga na maziwa pamoja .

 
Tumia rubber spatula endelea kuchanganya vizuri.

 
Kisha  hamishia mchanganyiko wa unga wako kwenye meza na . KANDA KWA DAKIKA 3 TU USIZIDISHE.

 
Tumia mikono yako kukandamiza mpaka iwe flat kabisa. Kisha tumia biscuit cutter and kisha kata vipande 6 dough rounds.

 
Kisha weka kwenye baking tray, brush tena kwa juu ya biscuti na ute mweupe wa yai

 
Mwagia sukari kwajuu na kisha weka kwenye friji ipoe kwa masaa 2 hours kabla ya kuoka

 
Kisha oka kwenye oven na iwe na rangi ya golden brown, chonma kwa dakika 12 hadi 15. Tumia wire rack weka keki zako na poza kwa dakika 10.

 
Sasa andaa whipped cream. Tumia mashine kwa kupiga na mchapo au mashine.

 
Sasa unaanza kuziunganisha, kata keki katika vipande viwili. Ukishakata tumia kipande cha chini kwa kupanga matunda.

 
Kipande cha chini weka matunda na kisha weka cream kisha funika kipande cha juu.
 
 
 Kisha unaweza kupanba kwa vipande viwili vya strawberries kwajuu ya keki yako na pamba jani la mint kwa kuboresha rangi.
 


No comments: