CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Monday, January 25, 2010

NAMNA YA KUTENGENEZA MAANDAZI



Chukua Amira ya chenga gram 11




Chumvi nusu kijiko kidogo cha chai



Sukari gram 250



Unga wa ngano kilo moja


Maji ya uvugu vugu nusu lita




Mafuta ya kupikia lita 2 na nusu


Weka pakiti ndogo ya amira yenye ujazo wa gramu 11 yoote kwenye unga wako wa kilo moja





Kisha weka chumvi nusu kijiko kidogo cha chai chumvi hii husaidia kupunguza mafuta ndai yaa andazi baada ya kuiva andazi lako litakua halina mafuta safi na salama kwa mlaji


Weka sukari gram 250 katika unga wako



Baada ya hapo weka mafuta ya moto ujazo wa kikombe kidogo cha chai au gr 250
 changanya vizuri mafuta bado yakiwa yamoto




Kisha weka maji ya uvuguvugu ili kuuwa ngano nakufanya amira kuweza kumuka haraka





Kanda mchanganyiko wako safi kwa kutumia nguvu na umakini mpaka mchanganyiko wako uwe laini



Mchangyanyiko wako kama uko bado ni teketeke na ulizidisha maji kidogo weka unga kiasi kisha endelea kukanda mpakja uwe mkavu na laini


Hapa safi sasa



 Shepu vizuri tayari kwa maandalizi ya kusukuma na kukata






Sukuma unga wako mpaka saizi ya unmene halisi wa andazi lako utakavyopenda liwe


Kisha tumia kitu chechote kile kukatia kwa umbo lolote lile utakalo lipenda





Yaache kwa muda wa dakika 10 baada ya kuyakata yaumuke kisha itakua tayari kwa kuyachoma



Baada ya kukata maumbo mazuri ya duara unga unaobakia unaweza viringisha maumbo tofauti kama uonavyo katika picha pia unaweza tengeneza hata herufi


 Pasaha mafuta yako katika moto wa wastani yasiwe na moto mkali utapelekea maandazi yako kuungua kisha yaweke katika moto na geuza kila mara ili yasivimbe upande mmoja na ikawa vigumu kuyageuza






Hili ni anfazi lako safi limeshaiva na halina mafuta ndani na safi kabisa


11 comments:

Anonymous said...

Du yamy yamyiii, am going to do it for Kids over this weekend, Mungu akubariki kwa kushare nasi kipaji chako kaka. tupe ushauri juu ya watoto wasiopenda kula

Mdau
Lim2217

Anonymous said...

Mbona maandazi hayana iliki? Sie watu wa pwani maandazi yanatiwa iliki, yaani zile mbegu zake unatoa unazisaga kidogo unachanganya kwenye unga kabla hujaweka maji. Mimi maandazi kwa ajili ya watoto huweka mayai na maziwa au tui la nazi badala ya maji ili kuongeza virutubisho.

Mswahili

Anonymous said...

mswahilki sie hatutaki mapishi ya kiswahili,kaka hapa ye anatufundisha ya kwake hivyo hajakosea.we na iliki kivyako vyako.Wapishi wengii...........???

Anonymous said...

chef hongera kwa kazi nzuri,endelea kutuelimisha na kutunufaisha kwa kipaji ulichopewa na Mola.
kila la kheri Chef
mama Roxxie.

Anonymous said...

asante kaka sana kwa recipe yako nzuri sana ya maandazi, hata mie sipendi vikorombenzo naipenda style yako hiyo, ukiweka iliki sipendi kabisa hiyo arufu yake kwenye maandazi asante naenda kupika saa hii ,

Anonymous said...

nakukubali sana kaka angu...mara nyingi nikitaka kupika hua nachungulia humu ndani nipate maujanja mara moja namsuprise husband

Anonymous said...

kila nikikaanga maandazi au kalimati yanakuwa na done ndani yani halichambuki kama sponji, nakosea nini??

Anonymous said...

Asante kwa maelekezo. Nataka kupika maandazi lakini natumia dough mixer kukandia je nafuata utaratibu huo

Anonymous said...

Chef katika siku zote nilizowahi kupika maandazi haya kiboko! Malaini na mazuri mno na ndani hayana mafuta. Ubarikiwe sana. Asante!

Anonymous said...

Chief nimeyapenda sana haya maandazi, maana hayana viungo ving me hua sipend maandazi yenye ilik na viungo viingii.

Unknown said...

Chief hakika nakupongeza sana kwa elimu ya ujasiliamali uliyoitoa bure tena kwa kueleweka. Tushindwe wenyewe maana maandishi pamoja na picha vinajieleza wazi kabisa