CHOMA MBUZI AU KONDOO KISHA KULA NA SALAD YA SPINACH NA VIAZI VYA KUOKA MHHHH YAM YAM!!!!!!!!!!!!!!!!
MAHITAJI
1 Nyama ya mbuzi mguu wa mbele au wa nyuma
2 kilo viazi ulaya ( viazi mbatata)
1 kilo nyanya
1 kilo spinach
1 kopo tomato pest
1 chupa ndogo tomato sauce
200 gram soya sauce
50 gram curry powder
50 gram kitunguu swaumu
50 gram tangawizi
100 gram mafuta ya kupikia
50 gram chumvi
100 gram maji ya limao
50 gram masala spice
JINSI YA KUANDAA
Changanya vitu vyote hapo juu kwa wakati mmoja na kisha paka nyama yako ya mbuzi au ya kondoo kisha iweke kweneye friji kwa masaa 3 hadi 4
Huu ni muonekano wa mguu wa kondoo mbichi
Huu ni muonekano wa nyma hii baada ya kuwekewa marination ( Viungo au vikorombwezo) iweke kweye chombo utakachotumia kuokea kweney oven. kisha funika chombo hicho kwa kutumia aluminium foil. choma katika oven kwa masaa 2 kwa mto wa juu. kisha toa nyama itakua imeiva safi na laini.
Hapa ni baada ya kutoka kwenye oven ina waka waka imeshaita tayari kwa kuliwa. Kama unawageni unaweza kuwashangaza kwa kuwasha jiko la mkaa na ukaiweka juu yake kila mgenia anapita unamkatia kama ndafu vile hahahahahahahaaaaaa!!!
Hapa ni baada ua kukatwasasa muonekano ilivyoiva kwa ndani nyama hii inakua laini sana na tamu hasa si mchezo!!!!
Huu ni muonekano wa viazi vya kuoka, kuviandaa unamenya kama kawaida kisha una vipaka mafuta ya kula na chumvi kisha unaviweka kwenye oven una bake mpaka uone vimebadilika rangi na vimekua laini.
Huu ni muonekano wa spinach ya kukaanga na nyanya za kuoka kwajili ya salad
JINSI YA KUANDAA SALAD HII
Kaanga spinach kwenye kikaanga kwa kutumia mafuta ya kula na chumvi kisha iweke pembeni ipoe.
kisha kata nyanya katika vipande viwili kisha iweke kweney oven oka kwa mto mdogo sana kwa muda wa saa 1 inyauke yu isirojeke.
kisha chukau mchanganyiko wa spinach, tango na nyanya kata vipande vidogo na changanya pamoja na goat cheese ay fettah cheese. Nyunyizia kidogo olive oil, chumvi pamoja na vinegar iweke kwenye friji ipoe tayari kwa kuliwa.
Huu ndio muonekano wa salad yetu safi kabisa yenye cheese ya mbuzi ( goat cheese) na mchanganyiko wa mboga majani
BADILISHA MLO WA WEEKEND HII KWA RECIPE HII SAFI KABISA
2 comments:
duuuuuuh nakufagilia mbaya...we ndo unanipa idea ya nini nipike kwangu weekend baada ya kula mchana kazini wiki nzima......kazi nzuri...kaza buti wangu
hello mr chef,
my name is chef gerard, from bagamoyo cost region tanzania,am big up coming chef, am real happy & enjoying your recipe its helping me to my job and home.
thanks & god bless you at all.
Post a Comment