FAMILIA YAKO KAMA HAWAPENDI KULA DAWA NI KUWAFANYA WAPENDE KULA NA NI RAHISI SANA JUISI HII AINA YA LEMONADE NI KIBOKO KWA ASIYEPENDA KULA LAZIMA APATE HAMU NA ATAKULA TU.
TEGENEZA JUISI YA LADHA TOFAUTI KWA RECIPE YA LEMONADE NA MATOKEO UTAYAONA HARAKA SASA JIANDAE TU KUONGEZA BAJETI YA CHAKULA MAANA WASIO NA HAMU ITAKUJA.......!!
FUATILIA MAFUNZO HAPO CHINI KAMA PICHA NA RECIPE ZINAVYOONYESHA.
KWA NYUMBANI TANZANIA SASA JOTO LINAANZA NA HASA MWEZI UJAO MAPAKA JANUARY JOTO HUWA LIKO JUU KATA KIU KWA VINYWAJI HIVI.
KWA NYUMBANI TANZANIA SASA JOTO LINAANZA NA HASA MWEZI UJAO MAPAKA JANUARY JOTO HUWA LIKO JUU KATA KIU KWA VINYWAJI HIVI.
SIO KILA JUISI INAMANUFAA NA MWILI WAKO UISJI HIZI ZINAMANUFAA NA FAIDA SANA NA MWILI WAKO KIAFYA KUTOKANA NA MAFUNZO YA NJIA BORA YA UTENGENEZAJI.
WATERMELON LEMONADE JUICE ( juisi ya tikiti maji na limao )
MAHITAJI
120gram sukari nyeupe
120gram maji baridi
1 kilo ya watermelon katkata vipande vipande
480 maji baridi
60 gram jisi ya limao
480 gram ice cubes
JINSI YA KUANDAA
Weka vipande vya watermelon kwenye blender funika na saga mpaka iwe rojo rojo kisha chuja kweney chujio la chai iwe safi kabisa.
Chukua maji 120 gram na sukari 120 grama chamsha katika kikaango mpaka iyeyuke vizuri kwa dakika 5 kisha itoe kwenye moto. Katika mchanganyiko huo wa sukari na maji changanya maji tena 480 gram na jisi ya limao.
Chukua glasi 10 kisha weka ice cubes (barafu) na mimina mchanganyiko wa sukari limao na maji kwenye hizo glasi, Baada ya hapo chota vijiko vitatu vya chakula ile rojo la watermelon iliyosagwa weka kwenye kila glasi moja yenye mchanganyiko wa lemonade.
Kumbuka kuikoroga vizuri kabla hujampatia mnywaji.
Kumbuka kuikoroga vizuri kabla hujampatia mnywaji.
PINE APPLE LEMONADE JUICE ( Juisi ya nanasi na limao )
MAHITAJI
720 gram juisi ya nanasi
3 limao kubwa, yakamue juisi
240 gram sukari nyeupe
120 gram asali mbichi
6 slices za limao
2 lita ya soda water
3 limao kubwa, yakamue juisi
240 gram sukari nyeupe
120 gram asali mbichi
6 slices za limao
2 lita ya soda water
JINSI YA KUANDAA
Chukua sufuria safi weka kwenye moto wa wastani kisha weka juisi ya nanasi, juisi ya limao, sukari na sukari. Acha ipate moto ianze kuchemka kwa dakika 10. Kisha iweke pembeni ipoe baada ya hapo iweke kwenye friji usiku kucha.
Weka glasi 6 viapnde vya barafu. Kisha weka kipande 1 limao kila galsi kwa hizo glasi zote 6 . Kisha mimina mchanganyiko wa ile juisi ya nanasi nusu glasi . Baada ya hapo jaza glasi nusu uliyobakia kwa soda water na ukoroge kabla ya kumpatia mnywaji.
STRAWBERY LEMONADE JUICE ( Juisi ya tunda strawberry na limao )
MAHITAJI
I lita ya maji iliyochemshwa na 200 gram ya juisi ya limao kwa dakika 10, 200 gram sukari vyote chemsha pamoja sukari iyeyuke.
200 gram vipande vya barafu.
1 kilo ya strawberry zilizokatwa nusu
200 gram vipande vya barafu.
1 kilo ya strawberry zilizokatwa nusu
JINSI YA KUANDAA
Katika bakuli kubwa changanya ule mchanganyiko wa maji na limao pampja na barafu. Kisha mimina katika glasi nusu ya mchanganyiko wako wa maji na limao, mwisho weka viapnde vya strawberries.
Koroga na mpatie mnywaji.
Koroga na mpatie mnywaji.
PASSION LEMONADE JUICE ( Juisi ya tunda passion na limao )
MAHITAJI
300gr sukari
500gr maji ya baridi
400gr juisi ya limao
400gr juisi ya limao
500gr juisi ya tunda passion
1 lita ya maji baridi
1 kilo ya ice cubes ( Vipande vya barafu )
JINSI YA KUANDAA
JINSI YA KUANDAA
Chukua sukari 300gr changanya na maji 500gr weka katika sufuria chemsha mpaka sukari iyeyuke kisha toa weka pembeni maji hayo yapoe.
Katika bakuli kubwa weka hayo maji yenye sukari, 400gr juisi ya limao, 500gr juisi ya tunda passion, lita moja ya maji baridi na kilo moja ya barafu ( ice cubes ). Kisha koroga vizuri ichanganyike na kisha iweke kwenye friji ipoe kwa saa 1 hadi masaa 4.
Kumbuka baaa ya kuichanganya hapa itakua kali kweli mchangayiko wa limao na passion lakini inavyozidi kukaa barafu inayeyuka na ladha itakua imebalance na kupata ladha safi kabisa uchachu wote utaisha na kubaki ladha safi.

Kabla ya kumuhudumia mywaji kumbuka kukoroga, pia unaweza kuweka kwenye friji kwa siku 3 - 4 bila kuharibika.
HII NI ORANGE LEMONADE JUICE ( Juisi ya chungwa na limao)
MAHITAJI
240gr sukari
240gr maji ya moto
1 kijiko kikubwa cha chakula kwaruza maganda ya limao upate chenga chenga
2 kijiko kidogo cha chai kwaruza maganda ya chungwa upate chenga chenga
720gr maji baridi
720gr maji baridi
480gr jusi ya chungwa
60gr jusi ya limao
JINSI YA KUANDAA
Chukua sufuri kisha weka chenga chenga za limao na chungwa pamoja na maji moto na sukari ichemke mpka sukari yote iyeyuke kwa dakika 8 - 10 pia itakua nzito.
Kisha itoe jikoni na ichuje ili kutoa yale maganda. Kisha weka maji hayo yenye sukari yaliyopoa katika bakuli kubwa na uchanganye na jusi ya chungwa pamoja na juisi ya limao na maji baridi .
weka katika friji kwa saa 1 na mpatie mnywaji pamoja na barafu.

HII NI CARROT LEMONADE JUICE ( Juisi ya karoti na limao )
MAHITAJI
240gr sukari
240gr maji ya moto
1 kijiko kikubwa cha chakula kwaruza maganda ya limao upate chenga chenga
2 kijiko kidogo cha chai kwaruza maganda ya chungwa upate chenga chenga
720gr maji baridi
480gr jusi ya karoti
60gr jusi ya limao
JINSI YA KUTENGENEZA JUISI YA KAROTI
Chukua karoti 700 gr kisha tumia grater kwaruda karoti sehemu yenye matundu madogo kabisa ya mwisho kisha chukua 200gr ya maji safi baridi changanya na uanze kukamua na kuchuja kisha utapata 480gr za juisi ya karoti.
kama unamashine ya kukamualia juisi basi rahisi sana osha vizuri na uzimenye karoti zako kisha weka kwenye mashine na washa ikamue yenyewe.
240gr maji ya moto
1 kijiko kikubwa cha chakula kwaruza maganda ya limao upate chenga chenga
2 kijiko kidogo cha chai kwaruza maganda ya chungwa upate chenga chenga
720gr maji baridi
480gr jusi ya karoti
60gr jusi ya limao
JINSI YA KUTENGENEZA JUISI YA KAROTI
Chukua karoti 700 gr kisha tumia grater kwaruda karoti sehemu yenye matundu madogo kabisa ya mwisho kisha chukua 200gr ya maji safi baridi changanya na uanze kukamua na kuchuja kisha utapata 480gr za juisi ya karoti.
kama unamashine ya kukamualia juisi basi rahisi sana osha vizuri na uzimenye karoti zako kisha weka kwenye mashine na washa ikamue yenyewe.
JINSI YA KUANDAA
Chukua sufuri kisha weka chenga chenga za limao na chungwa pamoja na maji moto na sukari ichemke mpka sukari yote iyeyuke kwa dakika 8 - 10 pia itakua nzito.
Kisha itoe jikoni na ichuje ili kutoa yale maganda. Kisha weka maji hayo yenye sukari yaliyopoa katika bakuli kubwa na uchanganye na jusi ya karoti pamoja na juisi ya limao na maji baridi .
weka katika friji kwa saa 1 na mpatie mnywaji pamoja na barafu. Juisi hii inaweza kukaa kwa siku 2- 3 katika friji.

RED APPLE LEMONADE JUICE ( Juisi ya tunda apple jekundu na limao )
MAHITAJI
3 nyekundu apples, menya na toa kokwa ka kati kati
2 limao kamua Juisi
1 kijiko kikubwa cha chakula sukari
240gr maji safi baridi sana
JINSI YA KUANDAA
Tumia mashine ya kukamuli juisi kama huna tumia greater kwaruza kama ilivyokua kwenye karoti.
Katika bakuli kubwa changanya apple jusi na juisi ya limao, sukari na maji baridi. changanya vizuri. Kisha muhudumie mnywaji pamoja na barafu.
Kinywaji hiki utapata glasi 2 tu.
GREEN APPLE LEMONADE JUICE ( Juisi ya tunda apple la kijani na limao )
MAHITAJI
3 nyekundu apples, menya na toa kokwa ka kati kati
2 limao kamua Juisi
1 kijiko kikubwa cha chakula sukari
240gr maji safi baridi sana
JINSI YA KUANDAA
Tumia mashine ya kukamuli juisi kama huna tumia greater kwaruza kama ilivyokua kwenye karoti.
Katika bakuli kubwa changanya apple jusi na juisi ya limao, sukari na maji baridi. changanya vizuri. Kisha muhudumie mnywaji pamoja na barafu.
Kinywaji hiki utapata glasi 2 tu.
UKIFATILIA VIZURI NA KWA UMAKINI ZAIDI UTAJICHUKULIA POINT ZA KUTOSHA KATIKA FAMILIA KWA KUWATEKA KWA LADHA SAFI YA VINYWAJI MCHANGANYIKO WAKATI WA CHAKULA AU KABLA NA BAADA YA CHAKULA FURAHIA NA FAMILIA YAKO.
4 comments:
mimi huwa nafatilia sana mapishi yako hongera kwa kutufutisha mapishi mazuri!
misswhite,zanzibar
im waiting for the recipe usiache tuma
Asante kaka!!
Hizi juisi zinatamanisha kweli.. Tunasubiri recipes kwa hamu.
Nakutakia Eid njema
Mama Jeremiah
Asante sana kaka, be blessed.
Post a Comment