RECIPE SAFI KABISA YA MKATE WENYE TUNDA AINA YA EMBE LA KUIVA PAMOJA NA KARANGA
MAHITAJI
240gr unga wa ngano
180gr sukari
1/2 kijiko cha chai baking powder
1/4 kijiko cha chai chumvi
1/4 kijiko cha chai unga wa mdalasini
2 ute mweupe wa yai piga ulainike
60gr mafuta ya mboga majani (vegetable oil)
1/2 Kijiko cha chai vanilla ya maji
240gr vipande vya embe iliyoiva
120 gr ya karanga au korosho chop chop
JINSI YA KUANDAA FATILIA MAFUNZO HAPO CHINI KATIKA PICHA
Katika bakuli, changanya mayai, mafuta ya mboga majani ( vegetable oil) na vanilla.
KIsha chukua bakuli jingine na changanya unga wa mdalasini, chumvi, unga wa ngao,sukari na baking powder. Kisha chukua ule mchanganyiko wa mayai na mafuta changanya kwenye mchanganyiko wa unga na sukari mpaka uloane vizuri.
Ndani ya mchanganyiko wa unga changanya karanga zako au korosho pamoja na maembe kwa kutumia kijiko plastiki au mbao.
Kisha chukua chombo chako utakachotumia kuokea na kipake mafuta na umimine mchanganyiko wako safi kabisa ulio tayari kwa kuokwa.
Choma katika moto wa 350F kwa dakika 50-60 au mpaka ukishaona mkate wako umekua na rangi safi ya kahawia na ukichoma na kijiti cha mabo kiataoka kisafi hakina uji uji wa unga.
Acha ipoe kwa muda na kisha uweke mkate wako kwenye wavu au wire rack.
Huu ni muonekano wa kipande cha mkate baada ya kukatwa
Hakiisha mkate wako unapoa kabisa kabla ya kukata kata vipande. Kila kipande cha embe katika mkate wako sio tu kuweka ulaini wa mkate ila kina weka ladha safi na halisi ya tunda lenyewe. Utamu na ulaini wa mkate wenyewe unaweka mwanzo mzuri wa siku endapo utatumia kama kitafunwa kwa chai ya asubuhi! Kama umepika jioni unaweza kula kwa chai ya saa10 jioni na ukaumalizia kesho yake kwenye chai ya asubuhi.
FURAHIA NA FAMILIA YAKO KWA KITAFUNWA SAFI KABISA WAKATI WOWOTE.
1 comment:
hii itakuwa nzuri sana kwa mama yangu. kaka tupe recipe tupate baraka za wazazi, wow! ntampa surprise mama yangu nikienda home Inshallah
Post a Comment