CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Friday, November 19, 2010

JIFUNZE KUTENGENEZA MCHANGANYIKO SAFI WA KIAZI NA BILINGANYA


 RECIPESAFI KABISAYA MCHANGANYIKO WA CHAKULA HIKI CHA MBOGA MAJANI

MAHITAJI

 250 gram kiazi mabatata ( kiazi ulaya)
250 grams bilinganya ( egg plant)
1 kitunguu maji katakata
1 kijiko kidogo cha chai mbegu za cumin (cumin seeds)
1-kijiko cha pili pili ya unga (chilli powder)
1/2 Tangawizi mbichi menya na isage
2 kijiko kidogo cha chai coriander powder
1/2 kijiko kidogo cha chai unga wa manjano (turmeric powder)
1/2 kijiko kidogo cha chai garam masala
1 fungu la majani ya giligilani kwa kupambia na harufu safi
1 kijiko cha chai maji ya limao kuongeza ladha
5 gram chumvi


JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI



Chukua bilinganya zako kisha kata kata amaumbo madogo na hakikisha unaweka katika bakuli yenye maji ili kusaidia zisiaharibike rangi yake nzuri. 



Weka mafuta ya kupikia ili yapate moto katika kikaango. yakishapata moto weka cumin seeds, Kisha pili pili, tangawizi , na vitunguu maji endelea kukaanga.



Vitunguu vikilainika, Weka viazi mbatata, chumvi na turmeric powder. kisha mwagia kijiko kimoja cha maji ili kufanya unga wa manjano usiungulie katika kikaango.



Kisha ongezea bilinganya na  unga wa giligilani (coriander powder) na garam masala koroga ichanganyike vizuri


  
 Funika mfuniko wa sufuria au kikaango chako na acha kwa dakika 8 mpaka 10 hakikisha bilinganya inaiva vizuri.



Baada ya chakula chako kuiva katakata majai ya giligilina na pamba kwa juu husaidia kuleta harufu nzuri na kuongeza ladha ya chakula




Chakula hiki unaweza kula na ugali, wali au chapati pamoja na mtindi safi kabisa na ukafurahia sana sana.


No comments: