CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Saturday, November 27, 2010

JIFUNZE KUTENGENEZA WALI NA NYAMA PAMOJA NA YAI LA KUKAANGA


WALI HUU UNAWEZA KUPIKA KWA KUTUMIA AINA TOFAUTI ZA NYAMA MFANO NYAMA YA KUKU, NG'OMBE, MBUZI, KONDOO, SAMAKI KAMBA MAPISHI YA NYAMA ZOTE MTINDOO NI HUU HUU.


MAHITAJI

1 kikubwa Kitunguu
1 fungu Spinach
5 gram Chumvi
1 kg Wali ulioiva
5 Mayai
1 fungu majani ya korienda
1 kg nyama ( mbuzi au kuku au samaki kamba au ng'ombe)
2 kijiko kikubwa cha chakula Mafuta ya kupikia
1 kijiko kikubwa cha chakula Soya sauce
1 kijiko kikubwa cha chakula Oyster sauce
1 kijiko kikubwa cha chakula Hp sauce
1 kijiko kikubwa cha chakula Tomato sauce
1 fungu la Spring onion
10 gram Kitunguu swaumu cha kusagwa
10 gram Tangawizi yakusagwa


JISI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO CHINI



Kwanza kabisa unaanza kuandaa marination ili isaidie kuweka ladha safi katika nyama na kuifanya iwe laini, changanya katika bakuli Soya sauce, HP sauce, Tomato sauce, Oyster sauce, 5 gram kitunguu swaumu, 5 gram tangawizi, 1 kijiko kikubwa cha chakula mafuta ya kupikia na majani ya korienda



Kisha kata kata nyama na weka katika huo mchanganyiko wako iache katika friji kwa muda wa masaa 2 itakua tayari.



Kisha kata kata kitunguu na weka kijiko kimoja cha mafuta yakupikia katika kikaango na kaanga kwa dakika 1 tu


Kisha chukua mchanganyiko ule wa nyama na weka katika kikaango chenye vitunguu na uendelee kukaanga katika moto wa wastani kwa dakika 10 hadi 15 nyama yako itakua imeiva.



Chukua wali uliokwisha iva kisha weka katika sahani kama inavyoonekana katika picha



Juu ya wali weka spinach iliyokaangwa au iliyochemshwa hakikisha unasambaza vizuri juu ya wali wako



Kisha unaweka juu yake mchangayiko wa ile nyama yako saafi na tamu kuliko zoooote hahahahahahahaaaaaaaa!!!!




Mwisho kabisa unakaanga yai jicho la ng'ombe au "fried egg sun side up " kisha unaliweka juu ya nyama katika sahani kama muonekano wa picha hap juu.

FURAHIA NA FAMILIA YAKO MAPISHI HAYA MAARUFU SANA NCHI ZA MASHARIKI YA MBALI NI RAHISI KUENGENEZA HALICHUKUI MUDA MREFU NA NINAFUU KWA GHARAMA.



3 comments:

Anonymous said...

jamani hapa umeniacha hoi mahitaji na maelezo kidogo katika kila picha.

Flora said...

Hi Chef,

Tafadhali tunaomba kabla ya kutuwekea pishi jipya uhakikishe umemaliza kutupa maelezo ya pishi lililotangulia kwani mara nyingi huwa unaishia " kaa tayari kwa kupata recipe safi" tu.

Asante

Anonymous said...

Nasubiri na la hapa....maelezo ya mahitaji na jinsi ya kulipika hili sosi

lulumbu