CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Sunday, December 19, 2010

JIFUNZE KUPIKA PILAU SAFI NA RAHISI WAKATI HUU WA SIKUU


RECIPE SAFI KABISAYA PILAU KWA MSIMU HUU WA SIKU KUU ZA KUFUNGA MWAKA. UNAWEZA PIKA KWA KUTUMIA MCHANGANYIKO WA MBOGA MAJANI TU AU UKAPIKA KWA AINA YEYOTE YA NYAMA KWA KUTUMIA MTINDO HUU HUU NA IKAPENDEZA SANA SANA.

MAHITAJI

  240 gram za mchele wa basmati au mchele wowote mrefu, Loweka katika maji kwa dakika 20
  1 kijiko kidogo cha chai mbegu za binzali nyembamba ( cumin seed)
   1 kitunguu kikubwa kata kata
  1 Nyanya kubwa kata kata
   3  spring onions ( majani ya kitunguu) 

  1 bay leaf
   3 cloves ( Mbegu za Karafuu )

3 cardamom ( mbegu za hiriki)
  1/2 kijiko cha chai kidogo turmeric powder ( Unga wa manjano)
   5 gram kitunguu swaumu
  1 pili pili mbuzi kata kata
    5 gram unga wa tangawizi au ya kusagwa
    1 kijiko kidogo cha chai garam masala
   600 gram coconut milk (Tui la nazi) sio lazima kama hutumii nazi basi weka maji kawaida
   5 gram chumvi
    1 fungu la giligilani kwajili ya kupambia
  1 jikiko kidogocha chai maji ya limao (sio lazima)
JINSI YA KUANDAA FATILIA HAPO CHINI  Katika sufuria weka kijiko 1 kikubwa cha chakula mafuta kisha kaanga mbegu za binzali nyembemba, bay leaf, karafuu, mbegu za hiriki, kitunguu swaumu, pili pili mbuzi, tangawizi na chumvi.
 Kitunguu kikashalainika weka nyanya pamoja na unga wa manjano na  garam masala. Kaanga kwa dakika 2.


Pilau hii nimepika sio ya nyama, kwa wale wapenzi wa nyama wakati umeweka vitungu na vile viungo vyote weka pamoja na nyama kaanag vyote kwa pamoja kwa dakika 10 kisha ndio uweke nyanya na viungo vingine vinavyofatia.


Nyama yako ili iwe laini chukua papai lililoiva baada ya kukatakata nyama pondea papai katika bakuli lenye nyama kisha weka chumvi kidogo, soya sauce kidogo, kitunguu swaumu na tangawizi kwa ladha zaidi. Nyama hii iweke kwenye friji kwa dakika 45 tu iwe ndani katika mchanganyiko huu itakua laini sana na utaipika kwa muda mfupi sana na familia watafurahia.
   Kisha ongeza mchele hakikisha unauweka bila maji. Hakikisha una ugeuza geuza mpaka mchele ubadilike rangi na kutoa harufu safi baada ya kuukaanga.

 Kisha ongeza tui la nzai au maji kwa wale wasio tumia nazi endelea kukoroga ichanganyik vizuri. Funika na mfuniko kisha pika kwa dakika 10 au mpaka mchele wako utakapo iva na kua wali.


Kisha ugeuze wa chini uje juu na wajuu uende chini. Binafsi huwa napenda kuongezea njegere zilizochemshwa nikahifadhi katika friji mwisho kabisa pilau hii ikishaiva. 
 
 

Kwa kuipendezesha pilau yako sasa mwagia kwa juu majani ya kitungu na majani ya giligilani.  Kisha huwa na mwagia kwa juu maji ya limao kwa sababu kuu mbili. Moja ni kuongeza ladha. Pili inasaidia kupunguza kiwango cha sodium.


Hakikisha unampitia mlaji chakula kikiwa chamoto. Kwa wale wapenda samli unaweza weka kijiko kimoja pia itaongeza harufu na ladha safi katika pilau yako.
HUU NI MUONEKANO SAFI BAADA YA PILAU YETU KUIVA FURAHIA NA FAMILIA YAKO KWA MAPISHI SAAFI NA RAHISI KUANDAA KUMBUKA LIMAO AU PILI PILI SI LAZIMA KUWEKA NI PENDEKEZO LAKO TU HASA KAMA UNAMATATIZO USIWEKE TUMIA VIUNGO VINGINE NA BADO PILAU YAKO ITAPENDEZA SANA.5 comments:

Anonymous said...

Swalama chef Issa?
First of all great website my brother and you are making a lots of people have good time with different recipes they can try from your website.

Can you put more information not only the pictures of dishes,pics with info is more helpful as it assist on step by step cooking.

Once again thanks for your help.

mama Jeremiah said...

Asante Chef Issa.
Nilikuwa nataka nikuandikie kukuomba utupatie recipes za kufurahia Xmas!
Asante sana..
Ninaisubiri kwa hamu hii Pilau Recipe

Mama Jeremiah

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante sana kwa mwandalizi huo Je unaweza kunitumia maelezo? ningefurahi sana.

waridi said...

Hi chef naomba utuwekee recipe soon kwani ck yenyewe ndo inakaribia na mie nilitaka nijaribu kumpikia shemejio pilau.

mwajuma said...

napenda kubashiri ya kwamba, kutakuwa na design mpya ya kutumia matumba katika kutengeneza style mbalimbali mfano kutumia tango nanasi tikiti kutengeneza shepu mbalimbali kama vile kama vile ndege, au nanasi unaweza ukadesign kibakuli cha kuwekea matunda hehe wapenzi wa libeneke la mambo ya fruit. asante