CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Thursday, March 24, 2011

JIFUNZE KUTENGENEZA WAFFLE YENYE LADHA YA ZAFARANI AU SAFRON


KITAFUNWA HIKI NI SAFI SANA WAKATI WA CHAI ASUBUHI NA CHIMBUKO LAKE NI NCHINI BELGIUM KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA

MAHITAJI

480gram whole wheat graham flour ( au tumia unga wa ngao wa kawaida)

4 mayai vunja tumia ute mweupe tu
1 lita ya maziwa
30 gram olive oil
3 kijiko kikubwa cha chakula sukari ( Pia unaweza tumia asali badaya la sukari na inapendeza sana na unga graham)
2 kijiko kidogo cha chai baking powder
1/2 kijiko kidogo cha chai chumvi
2 gram ya saffron ( weka kidogo sana)


JINSI YA KUANDAA FATILIA Ă…ICHA NA MAELEZO HAPO CHINIHuu ni muonekano wa unga wa ngano anina ya Graham


Katika bakuli changanya unga, sukari, chumvi na baking powder.Chemsha maziwa yawe ya vugu vugu pamoja na saffron hakikisha unakoroga vizuri kisha weka pembeni katika bakuli

Kumbuka: Kama umetumia asli badala ya sukari, Basi hutakiwi kuweka sukari katika unga unatakiwa uweke asli katika haya maziwa.Piga ute mweupe wa mayai mpaka uwe na mapovuKisha chukua mchangayiko wa maziwa na changanya katika unga.
Kisha ingezea mafuta ya olive.


KIsha ongezea ule ute mweupe wa mayai kisha tumia mwiko na changanya pole pole mpaka unga wote uchanganyike vizuri.


Koroga pole pole mpaka mchangayiko wooote uchangayike vizuri.Hakikisha unawasha jiko lakupikia wafle kama maelezo ya kiwandani yanavyoelekeza, kisha weka mafuta kiasi na mwagia juu mchanganyiko wa unga.Hakikisha unaweka mchnaganyiko kiasi isijae kabisa maana inaumuka pia sambaza ienee jiko lote.
Muda wa kupika ni dakika 3 mpaka 5 lakini inategemea na maelekezo toka kiwandani. Muonekano huu safi wa rangi ya kahawia ni kua waffle yako imeiva na inaonekana safi sana.

 

Kawaida lazima iwe crispy unapotafuna kw amara ya kwanza kisha ukiendeleea inakua laini. Saffron sio kwajili ya kuongeza rangi ya njano tu au ya rangi ya chungwa lengo hasa ni kuongeza ladha.Unaweza kula kama ilivyo wakati wa chai asubuhi au  uka sliced matunda kama strawberries au blueberries, pia unaweza nyunyiza icing sugar au maple syrup. And oh yes kisha ukinywa na kikombe cha freshly orange juice ukawa umeanza siku na yummy breakfast Pia unaweza zikata katika muonekano huu hasa unapompatia mtoto
NI TAMU SANA HII WAFFLE WAANDALIE FAMILIA WAFURAHIE CHAI YA ASUBUHI
3 comments:

Flora said...

Kaka Issa,

Kwa kutusaidia naomba kabla hujaweka pishi jipya hakikisha umeandaa na maelezo kabisa kwa sababu mara nyingi ukitanguliza picha unatuacha njia panda (unasahau). Pamoja na hayo ninaisubiria hii kwa hamu.

Anonymous said...

HII BLOG SASA INANIBOA YANI KILA SIKU NIKIJA HAPA HAMNA JIPYA NAA ULISEMA UNAKUJA KWA KISHINDO AU NDO UMESHAISHIWA NA RECIPE????

Anonymous said...

mmh,watoto wangu,wanazipenda.mimi hununua super market za ready made,wakaziweka kwenye toast,wakajilia yamekwisha.ila nitajifunza kuzipika mwenyewe,kwani naamini ukipika mwenyewe zinakuwa na test nzuri.itanibidi ninunue hicho kimashine maalum cha kutengenezea