CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Saturday, April 9, 2011

JIFUNZE KUPAMBA CHAKULA ILI KUONGEZA MVUTO KWA WALAJI

MUONEKANO WA CHAKULA NI KIVUTIO TOSHA KWA MLAJI. JITAIDI PAMBA CHAKULA KATIKA SAHANI ILI KUVUTIA WALAJI KWANI MTU ANAANZA KULA KWA MACHO HATA KAMA CHAKULA SI KITAMU LAKINI MACHO YAKISHAPENDA MLAJI ATARIDHIKA NA MAPISHI YAKO.

 KUPAMBA CHAKULA SI HOTELINI TU HATA NYUMBANI UNAWEZA PAMBA CHAKULA CHAKO NA KIKAVUTIA SANA

WALI NYAMA, YAI LA KUKAANGA NA SALSAHuu ni muonekano wa chakula safi sana na kwa muonekano wa macho na hata kwa ladha ni safi sana

Pika wali wako saafi kisha kaanga yai kwa pembeni jicho la ng'ombe ( fried egg sun side up) kisha tengeneza salasa ya embe, nyanya na kitunguu weka pili pili manga chumvi na limao na pili pili mbuzi kiasi sio lazima.

kupamba katika sahani, chukua kibakuli au kikombe cha chupa ya chai kisha weka wali humo na kandamiza vizuri kisha geuza na weka katika sahani pembeni kama picha inavyoonyesha. Kisha weka salsa pembeni na yai la kukaanga.

Juu ya wali weka nyama au, kuku ya mchuzi mzito au samaki kisha juu yake unatupia karanga zilizookwa au korosho.

chakula hiki kitakua na muonekano safi sana na mlaji atafurahai mchanganyiko wa ladha.
 
 
 
VIAZI VYA KUKAANGA NA MCHANGANYIKO WA MBOGA MAJANI


 Viazi ulaya ( Irish potato) oka kwenye oven pamoja na chumvi na mafuta kiasi na kitunguu swaumu

pili chukua pili pili hoho pamoja na nyanya mbivu pia oka kwenye oven lakini hakikisha zinaiva wastahi tu zisipondeke au kuiva sana pia kumbuka kuziwekea chumvi na mafuta kabla ya kuzioka.

Kisha kata kata kitunguu maji slice, majani ya kitunguu mabichi changanya katika viazi mchangayiko wote huo wa mboga majani hizi mbichi na zile za kuoka pia.

kumbuka kuweka pili pili manga na tomato ketchup kidogo.

Hapa mlo kamili unakua umekamilika kwa wale wasio tumia nyama na pia kwa wanaotumia nyama chakula hiki unaweza kula nanyama ya samaki, kuku au mbuzi na ng'ombe pia.

BADILISHA MUONEKANO BORA WA CHAKULA NYUMBANI KWAKO FAMILIA IFURAHIE MAPISHI BORA NA CHAKULA SAFI1 comment:

Anonymous said...

aisee hii kitu kiboko sana
nimeipenda asa mie uwa nachagua sana chakula yani mara nyingi nakosa hamu chakula kikiwa kilekile...apa nimeifunza kitu safi

asante