JIFUNZE KUTENGENEZA CHAPATI YA AINA YAKE KWA KUTUMIA NAFAKA ZA AINA 15 PAMOJA NA MCHELE WA BROWN, NI TAMU SANA NA FAMILIA ITAFURAHIA SANA
MAHITAJI
240 gram mchele wa Brown
240 gram nafaka aina 15 Mchanganyiko
2 pilipili nyekundu kavu
1 Tangawizi osha na umenye
120 gram tui la nazi, nazi ya pakiti au kopo inafaa
majani ya Curry kwajili ya ladha
majani ya giligilani kwajili ya ladha
5 gram chumvi
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAFUNZO HAPO CHINI
Muda wa maandalizi : Masaa 8 hadi siku 1
Muda wa mapishi : Dakika 15
Idadi ya walaji : Watu 5
Picha inaonyesha mchanganyiko wa nafaka kiswahili chake ni kigumu lakini ukiangalia katika picha unaweza jua pia n a sio lazima uweke aina zote 15 unaweza tumia hata aina 5 na ikafaa majina ya nafaka hizo kwa kiingereza ni dried beans, peas, and lentils : Northern, Pinto, large Lima, Yellow eye bean, garbanzo, baby Lima, Green Split Pea, Kidney, cranberry bean, small White, Pink bean, small red, yellow split pea, lentil, navy, white kidney, black bean.
Loweka nafaka zote katika bakuli 1 kisha loweka mchele wa brown katika bakuli jingine loweka kwa usiku mzima.
Kesho yake asubuhi, Chuja maji vizuri
Kisha chukua nafaka zote na uziweke katika food processor/ blenda.
Weka tui la nazi pamoja na chumvi, majani ya gili gilani na majani ya curry kisha saga
Hakikisha umesaga vizuri kisha mimina katika bakuli pembeni
Kisha chuja mchele wa brown mimina katika processor ilie ile uliotumia mwanzo kusagia nafakla wala usihangaike kuiosha
Saga mpaka upate kimiminika.
Kisha chukua mchanganyiko wa zile nafaka changanya na mchanganyiko wa mchele.
Hakikisha mchanganyiko wako unachanganyaika vizuri na kisha ikiwa nzito unaweza ongeza maziwa au maji kiasi upate kimiminika kizito cha wastani.
Kuongeza ladha na sio lazima kama unapenda unaweza kuongezea kitunguu maji chop chop na pili pili ya kijani.
Chukua kikaango kisafi na mwagia mafuta kwa juu kisha kata kitunguu nusu na tumia kusambaza mafuta katika kikaango chako
Mwagia unga kati kati ya kikaango.
Chukua kijiko na kisha tumia kusambazia pole pole ukitengeneza mduara
Hakikisha unaweka mduara safi na mwembamba ili chapati yako iwe laini na kavu pia.
Ukishaona inaanza kua ya kahawia unatakiw akuigenuza
Hakikisha unatumia moto wa kati na choma chapati yako kwa dakika 5 au 6 tu iwe imeiva pande zote 2
Kumbuka kunyunyizia mafuta tu kila unapomaliza kugeuza ili upande ambao haujaiva nao uive uwe wa kahawia na kunukia harufu safi sana
Unaona inavyopendeza na ni kavu na laini safi kabisa
Chapati hii inapendeza sana kula ikiwa yamoto, pika kiasi tu ili mlaji aweze kula ikiwa fresh na yamoto kwa matumizi yajayo tafadhali weka unga huu katia friji na unaweza kuutumia hata baada ya wiki 1 waandalia wateja hotelini au nyumbani famia wafurahie kitafunwa hiki.
2 comments:
Hellow kaka,
Hakuna kitu nachukia kama hii kitu watu kuiba kazi za wenzao. Ebu cheki hii blog nadhani inakopy na kupest kazi za watu alafu haiandiki source 'http://wotepamoja.com'
Pamoja
Sasa ufunge tu blog maana tukakupigia kura ukashinda na hata kukidhi haja zetu ushatubwaga ni hayo tu, ama tafuta mtuu akusaidie
Post a Comment