JIFUNZE KUTENGENEZA WALI WA MCHANGANYIKO WA NYAMA YA KUKU NA CHEESE
MAHITAJI
4 vifua vyakuku (kata kata vipande vidogo)
360 gram ya maji
5 gram kitunguu swaumu
5 gram kitunguu swaumu
1 kijiko kikubwa cha chakula graham masala
1 nyanya ya kopo
500gram sawa na nusu kilo ya mchle
240 gram shredded cheddar cheese
1 kopo la mtindi halisi usio na ladha
1 parachichi au avocado safi lilioiva
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAEEZO HAPOCHINI
Weka kikaango katika jiko kasha pata moto wa kutosha mwagia vipande vya kifua cha kuku na kasha weka kitunguu swaumu, chumvi, pili pili manga na kama unamajani ya giligilani au parsley mwagia kuongeza ladha zaidi ila sio lazima na mafuta ya kukaangia.
Endelea geuza geuza isishike chini na kuungulia ndani ya dakika 5 tu itakua imeshaiva kabisa
Kisha mimina maji kwenye kikaango ay sufuria, weka graham masala kasha weka nyanya ya kopo na mwisho miminamchele na koroga vizuri funikia chakula kiendelee kuiva.
Hakikisha umefunika vizuri chakula kiendelee kuiva pole pole nivizuri kabla maji hayajakauka ukaonja chumvi na kuongezea
Hapa maji yote yameshakauka na wali wetu na mchanganyiko wa kuku umeshaiva safi kabisa
Wali bado ukiwa wamoto mwagia cheese kwa juu itayeyuka mara moja na kutengeneza mvuto kwa macho na harufu safi sana na ladha ya kipekee mdomoni
Ukichota wali kwa chini huu ndio muonekano wake
Baada ya kupakua unaweza mwagia juu mtindi pamoja na parachichi na ukaendelea kufaidi zaidi na family yako.
2 comments:
Nimependa hicho chakula Chef hadi mate yani mate yanitoka, tupia maelezo yake nasi tujue kujipikilisha
graham masala ndio garam masala?ama ni vitu viwili tofauti ?
Post a Comment