JIFUNZE JINSI YA KUPIKA CURRY KWA MBINU MPYA KWA MAPISHI TOFAUTI
MAHITAJI
240 gram mtindi halisi ( yoghurt)
2 kijiko kikubwa cha chakula unga wa dengu
240 gram maji masafi
3/4 kijiko kidogo cha chai Turmeric powder
1 kijiko kidogo cha chai pili pili nyekundu ya unga
5 gram chumvi
1 kijiko kikubwa cha chakula mafuta ya kula
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
Tumia mchapo kwa kupiga mtindi au Yogurt
Mpaka ilainike kabisa kama unavyoona kwenye picha.
Kisha weka kwenye mtindi unga wa dengu, Turmeric, pilipili ya unga nyekundu na chumvi.
Piga piga mpaka ichanganyike vizuri kabisa.
Kisha ongeza maji na endelea kupiga piga mpaka ichanganyike vizuri kabisa
Baada ya kuchanganyika vizuri weka pembeni uendelee na atua nyingine
Chukua kikaango kisha weka katika jiko lenye moto na umimine mafuta ya kupikia pamoja na samli. Mafuta yakipata moto weka jeera na ikianza kupasuka ongeza vitunguu maji na kitunguu swaumu.
Hakikisha unakoroga mpaka kitunguu kiwe laini, ongezea majani ya curry na uendelee kupika kwa dakika 2. Punguza moto uwe wa wastani
Endelea kukoroga na pole pole mimina ule mchanganyiko wa mtindi na viungo. Hakikisha ulipunguza moto ili kuhakikisha mtindi hauungulii kwa chini.
Wakati inaendelea kuiva, menya mayai na uweke pembeni. mimi nilitumia mayai 10 in this recipe but 8 should be good enough for 4 people normally.
Hakikisha unaendelea kukoroga mara kwa mara. Zoezi hili linachukua muda kwani unatakiwa kua mvumilivu pika kwa dakika 20 mpaka chuzi wako uwe mzito, unaladha ya kuiva na rangi safi ya njano, tastes cooked and looks yellow.
Onja tafadhali uone kama inatakiwa chumvi zaidi. Unaweza ongezea sukari kijiko kimoja kidogo cha chai kubalance test safi .
koroga vizuri ichanganyike.
Kisha weka mayai na acha ichemke kwa dakika 5.
Mpatie mlaji ikiwa yamoto pamoja rushia kwa juu majani yakijani ya vitunguu maji na giligilani au koriander. unaweza kula pamoja na wali, mkate au chapati
MUONEKANO SAFI KABISA WA CHAKULA HIKI
1. kwa nyama ya ngombe, mbuzi, kondoo, kuku au samaki unatakiwa kuichemsha kwanza iive vizuri kasha una ichanganya kayika mchuzi huu wakati tulioweka mayai na uache ichemke kwa dakika 10 ili nyama ipate ladha ya mchuzi na viungo.
WAANDALIE FAMILAI YAKO WAFURAHIE
2 comments:
du asante sana kwa mapishi mazuri ..ninaushauri mdogo tu ambao naamini utasaidia ili kuleta tija iliyokusudiwa.
1.jitahidi utumie lugha moja sahihi mfano kiswahili kuliko kuchanganya lugha mbili kwa wakati mmoja...
2.zingatia mtiririko wa maelezo huku ukijulisha majina rahisi ya viungo unavyotumia katika kuelewesha vizuri
3.tumia lugha ya kitaalamu zaidi ya mtaani
nimeipenda mno
Post a Comment