CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Friday, November 19, 2010

JIFUNZE KUTENGENEZA KIAZI CHA BINZALI NYEMBAMBA ( CUMIN au JEERA)


 RECIPE SAFI KABISA YA KIAZI HIKI KWA MATUMIZI YA NYAMA CHOMA


MAHITAJI

500 gram viazi vidogo vidogo osha vizuri na usivimenye
1 kijiko kikubwa binzali nyembamba (cumin seeds)
1 kijiko kidogo cha chai unga wa pili pili (chilli powder sio lazima)
1 kijiko kikubwa cha chakula unga wa giligilani (coriander powder)
1 kijiko kidogo cha chai mchanganyiko wa tangawizi na kitunguu swaumu (ginger-garlic paste)
1kitunguu kikubwa katakata
1/2 kijiko kidogo cha chai ungwa wa turmeric
5 gram za chumvi

JINSI YA KUANDAA FATILIA MAFUNZO HAPO CHINI



Chemsha viazi mpaka viive wastani. Hakikisha haviivi vikapondeka


Katika kikaango weka mafuta yakupikia yachemke, kisha kaanga mbegu za binzali nyembamba (cumin seeds) zikishabadilika na kua na rangi ya kahawia na harufu safi ongeza kitunguu maji na a ginger-garlic paste pamoja na chumvi kaaanga mapaka vilainike.



Kisha weka unga wa tumeric, unga wa giligilani na unag wa pili pili. kumbuka kuweka kijiko kimoja kikubwa cha maji ili viungo visiungulie katika chombo unachopikia.



Kaanga kwa dakika 2 mchanganyiko wako utakua umekauka kabisa.



Kisha ongeza moto uwemkali kabisa na weka viazi vyako vya kuchemshwa na kaanga kwa dakika 5. Kama una muda wa kutosha na hauna njaa sana acha moto mdogo na kaanga viazi vyako kwa dakika 2 hadi 3 mapak vianze kupata rangi ya kahawia kwa chini.




Hakiksiha unapopika dakika mbili kabla ya kuzima jiko lako katakata majani ya giligilani na rushia kwa juu kaanga kisha toa viazi katika jiko.


Huu ni muonekano wa viazi vikiwa vimeshaiva





WEKAKATIKA SAHANI SAFI NA WAPATIE FAMILIA YAKO WAFURAHIE KIAZI HIKI CHENYE LADHA SAFI SANA UNAWEKA KULA NA CHAPATI AU NYAMA CHOMA NA UTAFURAHIA SIKU YAKO.

UNAWEZA MENYA MAGANDA YA KIAZI BAADA YA KUCHEMSHA NA BADO UKAFURAHIA SANA CHAKULA CHAKO NA WENGI WETU TUMEZOEA KUMENYA VIAZI. USIPOMENYA MAGANDA YA KIAZI UNAKUA UMELINDA LADHA HALISI NA HARUFU NZURI YA KIAZI


5 comments:

Anonymous said...

kaka uko juu kama nyotaaaaaa!!!

Mija Shija Sayi said...

Hii sjawahi iona kabisa. Safi.

shamim a.k.a Zeze said...

hey CHEF ISSA

nisaidie kwenye hili mie ni mpenzi wa indian na chinese food

sasa kwa wahindi kuna viungo hivi wanawekaga kwa chakula especially kwenye sosi au michuzi yao inanivutiaga saana

unaweza nipa sample sa kama kopo...maana nanunuaga like beef. chicken au mutton masala lakini siipati ile ladha

plz advice

mama Iqra

Nancy said...

Hi Chef,

Ina maana viazi havitolewi maganda hata baada ya kuvichemsha? Anyways I luv your recipes

Anonymous said...

Familia yangu imefurahia sana haya mapishi ya viazi,ila mie nilibadili kidogo,baada ya kuchanganya viazi na viungo nikaviweka kwenye oven kwa dk 15.Delicious.Asante kwa kushare.