CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Thursday, June 2, 2011

JIFUNZE KUANDAA CAROT HALWA

KAA TAYARI KWA KUJIFUNZA KUTENGENEZA KAROTI HALWA

Kuandaa ni dakika30 

Kupika ni dakika 30
Idadi ya watu kula ni 2

MAHITAJI
 
480 gram ya karoti ya kukwaruzwa (grated)
240 gram ya maziwa
1 240 gram ya fresh cream
120 gram ya samli (ghee)
240 gram ya sukari
1 kijiko kidogo cha chai unga wa hiriki (cardamom powder)
1 kijiko kikubwa cha korosho zivunje vunje


JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA HAPO CHINI



Pasha kikaango katika moto, kisha weka samli iyeyuke na weka karoti, kaanga mapaka upate harufu nzuri ya kuiva (distinct aroma).




Kisha weka maziwa pamoja na cream pika kwa dakika 10 mpaka maziwa na cream yakaukie kwenye caroti (absorbed).


Kisha weka sukari pamoja na hiriki pika mapaka ishikane kabisa.


KIsha chukua chombo chochote au kikombe na weka halua yako kisha mimina katika sahani juu yake weka zile korosho zilizo kaangwa au kuokwa kama pambo kwajuu na pamoja kuongeza ladha. Pia unaweza tumia Zabibu kavu (raisins)na zinapendeza sana.



HUU NI MUONEKANO WA HALUWA IKIWA KATIKA SAHANI TAYARI KWA KULA WATENGENEZEE FAMILIA YAKO WAFURAHIE.


6 comments:

Anonymous said...

kumbe upo kaka nilizani umesafiri

Anonymous said...

tunashukuru sana kwa kutujali japo upo mbali.
thanks.

Anonymous said...

nimesha ambatanisha cv na vyeti naomba kama nitafanikiwa au sintafanikiwa basi atujibu.
asante nina imani nitafanikiwa napenda sana kufanya kazi katika hayo mazingira.

emu-three said...

Mchongo safi sana huo, tutauchangamkia shukurani mkuu!

Anonymous said...

kaka tunasubiri recipe

Anonymous said...

tume kumiss sana.