CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Wednesday, June 15, 2011

JIFUNZE KUANDAA SALAD HII YA AVOCADO NA NJEGERE

KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI YA AVOCADO NA NJEGERE

Muda wa maandalizi dakika 30

Muda wa kupika dakika 15
Chakula kinatosha watu 2
MAHITAJI

480 gram njegere za kijani mbichi (chickpeas)

1 kubwa parachichi lililoiva limenye maganda (avocado)
1 fungu la gili gilani chop chop
120 gram kitunguu maji chop chop mimi natumia kitunguu cheupe (white onion)
1 pili pili hoho toa mbegu za ndani
1 limao kamua maji yake
1 kijiko kidogo cha chai chumvi
120 gram nyanya mbivu chop chop bila mbegu za ndani


JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA HAPO CHINI



Menya njegere zako kisha weka katika jagi la kupimia na upime kisha unaweka katika steamer mimi nilitumia hii hapo chini bamboo steamer ni kama chujio kwa chini unaweka juu ya sufuria yenye maji yaliochemka



Chemsha katika mvuke kwa dakika 6 mpaka 8. Kwenye maji unaweza chemsha kwa dakika 2 mpaka 3.


Kisha weka katika blenda au food processor pamoja na chumvi, limao na majani ya gili gilani



Saga mpaka iwe laini kabisa.



Kisha toa njegere katika blenda na uweke katika bakuli ´lenye avocado uliokwisha menya na uchanganye vitunguu chop chop, pili pili hoho chop chop na majani ya giligilani uliobakiza.



Kisha weka katika bakuli utakalo tumia mlaji na upambe juu pamoja na nyanya chop chop na majani ya gili gilani kwa kuongeza utanashati wa rangi. We enjoyed them along with tortillas, tortilla chips, tacos pia kwa chapati inapendeza sana.



Muonekano safi baada ya kupamba katika bakuli





WAANDALIE FAMILIA KWA KUBADILI LADHA YA CHAKULA NA KUBORESHA AFYA YA FAMILIA YAKO NAIMANI WATAIFURAHIA SANA


2 comments:

Anonymous said...

kinavutia!
asante chef

Magreth said...

Sijaoni parachichi limetumika wapi?