CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Thursday, November 10, 2011

JIFUNZE KUTENGENEZA WALI WA MANJANO

KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA NA RAHISI YA KUANDAA WALI HUU WA MANJANO NA KWA GHARAMA NAFUU SANA FAMILIA YAKO IFURAHIE

MAHITAJI

1 au 2 Saffron ( zafarani ya orange)


4 kijiko kikubwa cha chakula Olive oil
1 kitunguu kikubwa kata kata
1 pili pli hoho katak kata vipande vidogo vidogo
1 kijiko kidogo cha chai kitunguu swaumu cha kupondwa
240 gram mchele wa basmati
340 gram za maji ya vugu vugu
5 gram ya chumvi
majani kiasi ya giligilani kwa kupambia na kuongeza ladha
JINSI YA KAUNDAA FATILAI PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi: dakika 15

Muda wa mapishi: dakika 15
Idadi ya walaji: watu 2 

 

Katika kikaango weka kitunguu maji na safron pamoja na mafuta katika moto mdogo kisha endelea kukaanga pole pole. 


Baada ya mafuta kubadilika rangi ya orange. Kisha toa katika moto na acha ipoe kwa dakika 10 kisha yachuje hayo mafuta.


Kisha chukua kijiko kimoja kikubwa cha mafuta na weka katika kikaango. Kisha chukua tena kitunguu maji na kitunguu swaumu endelea kukaanga mapak vilainike. Kisha ongeza pili pli hoho na endelea kukaanga mpaka iwe laini.


Kisha weka mchele na endelea kukaanga pole pole mpaka mchele utaponukia na kubadilika rangi na kulainika.


KIsha ongeza maji na ufunike iendelee kuiva kwa dakika 8-10 kwa moto mdogo mpaka iive.


Baada ya kuiva kataka majani ya corriender na pamba katika wali wako.


Hakikisha unampatia chakula hiki mlaji kikiwa chamoto.Unaweza kuongeza ladha ya chakula hiki kwa kuweka karanga au zabibu kavu au hata korosho kavu

9 comments:

Anonymous said...

my friend,

Lovely and delicious pictures unfortunately there are no recipe
Please post some in order to understand quickly, thank u and God bless

Anonymous said...

Asante kwa kutufundisha pishi hili,ila hamna maelezo au ni computer yangu tu,
Good day

Anonymous said...

Asante kwa kutufundisha pishi hili,ila hamna maelezo au ni computer yangu tu,
Good day

Anonymous said...

Hey i am big fun of your blog
i almost everyday visit this blog
mimi tatizo langu ni hizo picha basi uwe unaweka na maelezo at least kutupa idea tufanye nini?

Anonymous said...

kaka tupe mambo. loh nime miss sana nipo busy tu.

Shangwe

Anonymous said...

Wee kaka wenzio Thanksgiving tunataka kupika wewe hata jinsi ya kupika hutuwekei mbona umekuwa mvivu hivoo kunani??

Anonymous said...

Pishi linaonekana zuri tatizo hakuna mahitaji (ingredients)

robsson said...

kaka please tupe maelezo ya pishi hili mkuu tuingie jikoni bana....

Anonymous said...

Issa , twaomba maelezo tafadhali