CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Saturday, September 15, 2012

JIFUNZE KUTENGENEZA JUISI YA TIKITI MAJI NA LIMAO

 
JUISI YA TIKITI MAJI NA LIMAO NOI SAFI SANA SANA
 
 
MAHITAJI
 
5 kg ya Watermelon
180gram juice ya limao 
80 gram ya asali mbichi
1 fungu majani ya Mint
vipande vya barafu au Ice Cubes,
 
JINSI YA KUTENGENEZA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi : dakika 15
Muda wa mapishi : dakika 15
Idadi ya wanywaji : Watu 4
 
 
Kiwango cha limao kinaweza kua gram 120 hadi gram 240 hii hutegemea na kiwango cha sukari katika tikiti maji au
 
 
Kata kata watermelon katika vipande vidogo, menya ngozi na kumbuka kutoa mbegu.

 
Chukua vipande vya watermelon saga pamoja na juice ya limao

 
Kisha ichuje katika chujio safi baada ya kuisaga

 
Kisha weka ice cube pamoja na majani ya mint katika jagi.

 
Kisha mimina juice katika jagi lako lenye barafu na mint

 
Kisha mimina asali mbichi kwenye mchanganyiko wa juisi na ukoroge ichanganyike.

 
Kihsa mpatie mnywaji ikiwa ya baridi weka ice cubes na majani ya mint kwa kupambia.

 
Huu ni muonekano safi kabisa baada ya kupamba kwa jani la mint na kuongeza ice cubes ili mnywaji afurahie kinywaji baridi

 
 
KINYWAJI HIKI NI SAFI SANA NA KINONGEZA HAMU YA KULA WAAANDALIE FAMILIA WABURUDIKE
 
 
 


2 comments:

Anonymous said...

badala ya asali si naweza weka sukari?afu wengine hatuna ivo vipimo vya gram sasa ndimu ziwe ngapi au limao ngapi???

nathan sm said...

majani ya mint nitayapata wapi mtwara kaka!!