CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Monday, June 7, 2010

WAPENZI WA PASTA NA NYAMA

MAHITAJI

1 kilo Nyama yeyote ile iwe kuku, mbuzi au ngombe
300 gram nyanya ya kopo au fresh ila katakata iwe ndogo ndogo kwa mchuzi
50 gram kitunguu swaumu
100 gram karoti
100 gram kitunguu maji
100 gram pili pili hoho
1 paketi la macaroni
300 gram viazi ulaya

JINSI YA KUANDAA FATILIA CHINI KATIKA PICHA


Huu ni muonekano wa nyama ya mbuzi naipenda sana



Weka kitunguu kwenye kwenye mafuta ya moto kisha kaanza mpaka kiwe na rangi ya kahawia


Kisha weka kiuongoa aina ya paprika kuongeza ladha kama hauna usiweke


kisha weka nyama kaanga pai mpka iive kumbuka kuweka maji kikombe kimoja kidogo kusaidia isiungue


huu ndio muonekano wa macaroni


Baada ya nyama kuiva weka viazi ulaya vibichi kaanga pia mpaka viive


kisha weka unga wa binzali kuongeza ladha


Kisha weka kitunguu swaumu kuongeza ladha  na harufu safi pia na kukata harufu ya nyama ya mbuzi


Kisha weka karoti na pili pili hoho pamoja na nyama ya kopo


Weka makaroni kwenye maji moto yaliyokiwsha chemka sana chemsha kwa dakika 7 tu


weka chumvi kwenye makaroni yaliyopo jikoni wakati yakiendelea kuchemka 


Baada ya makaroni kuchemka toa weka katika bakuli kisha yapoze ma maji baridi sana ili yasipondeke


Kisha chuja vizuri makaroni yako wasiwe na maji na chukua nyama yako ya mcuzi iliyokweisha iva changanya na makaroni yako yaliyoiva pia koroga ya changanyike vizuri


Kisha weka makaroni yako kwenye bakuli la kioo au la chuma ili uyaoke kwemye oven mchuzi ule ushikane safi na macaroni yako kua na muonekano na ladha safi


Kisha weka katika oven na oka kwa dakika 10 kumbuka kuweka aluminium foil kwa juu ili yasiungue

BAADA YA DAKIKA 10 MACARONI YAKO YATAKUA SAFI NA TAYARI KWA KULIWA WAPAKULIE FAMILIA YAKO YAKIWA YA MOTO KUMBUKA KUWEKA USAWA MACARONI , KIAZI NA NYAMA USIWEKE MAKARONI TUPU HAHAHAAAAAAAA





Tuesday, June 1, 2010

WAOOOOOOOOOOOO!!!!! SAMOSA SAMOSA SAMOSA ZA NYAMA

SAMOSA NI KITAFUNWA MAARUFU SANA DUNIANI KOTE KINAPENDWA NA WATU WA RIKA ZOTE WAKUBWA KWA WATOTO

MAHITAJI
1/2 Unga wa ngano
1 kilo nyama ya kusaga
1/2 kilo ya kitunguu
1 carroti
1 pili pili hoho
1/2 maji baridi
1/2 kijiko cha chai chumvi

Huu ndio muonekano a mahitaji yako

kata kitunguu,pili pili hoho na carroti kwa vipande vidogo

huu muonekano wa mboga zilizokatwa

Kaanga vitunguu vikisha iva weka pembeni

Kaanga nyama ya kusaga kisha weka chumvi ili iive na nyama mpaka ikauke maji yote ili samosa iwe na ladha nzuri

kisha weka karoti baada ya nyama kukauka vizuri

kisha weka pili pili hoho

kisha weka vile vitungu vilivyokwisha kaangwa mchanganyiko utakua safi
kisha weka kitunguu swaumu kaanga kiasi na chukua mchanganyiko huu weka pembeni upoe ili nyama na manda visiharibike

chukua unga nusu kilo weka maji nusu kikombe
kanda mchanganyiko wa maji na unga mpaka uwe ngumu ikiwa laini itakatika katika

sukuma mduara mdogo kisha paka mafuta ya kula juu yake
mwagia unga kiasi kuzunguka mduara wote kusaidia manda zisishikane baada ya kuchomwa
kumbuka kusukuma kisha paka mafuta halafu nyunyizia unga kisha zipandanishe kwa juu mpaka zifike
miduara 5 zitatoa samosa 20

kisha usukume mduara huo wenye samosa 5 mpaka upate chapati moja nene na pana usawa wa kikaango chako

choma katika kikaango kwa moto wa wastani ili usiunguze choma dakika 2 kila upande kisha geuze
kisha toa ikiwa ya moto anza kuzibandua kwa haraka kabla hazijapoa moja baada ya nyingine

kisha kata kati kwa kati pande nne kwa usawa

kisha kata kuzunguka manda hiyo ili kuweka mzunguko sawa
kisha chukua unga kiasi na maji changanya iwe nzito itatumika kama gundi angalia picha jinsi gundi ilivyopakwa kwa juu

kisha kunja upande wa kuli hakikisha unaandamiza ili gundi ikamate

kisha kunja upande wa kushoto kandamiza pia ili gundi ishike

huu ndio mkunjo wa manda ukiwa na umbo la v 
chukua kijiko kisha weka nyama katika manda yako


paka gundi kwa juu kisha funga manda yako


huu ndio muonekano wa sambusa mbichi

choma katika mafuta yenye moto wa wastani ili zisiungue na ziwe kaukau

samosa zkiwa katika moto kumbuka kuzigeuza mara kwa marazisiungue upande mmoja


Nusu kilo ya nyama yakusaga inatoa samosa 40 - 50 kwa matumizi ya nyumbani
Kwa biashara nusu kilo ya nyama ya kusaga na kilo ya vitunguu, karoti 5 napili pili hoho 5 unapata samosa 100
Maandalizi sio magumu sana ila samosa huwa inauzwa ghali sana kokote duniani

HUU NDIO MUONEKANO WA SAMOSA IKIWA IMESHAIVA SAMOSA HII NI SALAMA ANAWEZA KULA MTU YEYOTE KWA WALE WANAOPENDA PILI PILI UNAWEZA WEKA PILI PILI MBUZI AU PILI PILI MANGA ILI KUONGEZA LADHA ZAIDI FURAHIA NA FAMILIA YAKO. UNAWEZA KUZIHIFADI KATIKA FREEZER KWA MIEZI SITA.



DAGAA A KIGOMA YAM YAM!!!!!!!!!!!

DAGAA NI WAZURI NA WATAMU SANA ENDAPO UTAWAPIKA VIZURI KWA AFYA YA MLAJI
MAHITAJI
1/2 kilo ya dagaa wa Kigoma au wa Mwanza
2 nyanya kubwa
50 gram kitunguu swaumu
1 pili pili hoho kubwa
1 bilinganya saizi ya kati
35 gram mafuta ya kupikia
JINSI YA KUANDAA FATILIA MAFUNZO CHINI KATIKA PICHA

Muonekano wa mahitaji yako

weka mafuta katika kikaango yakipata moto kaanga vitunguu maji na kitunguu swaumu


kisha weka nyanya fresh iliyokwisha katwa katwa

kisha funika ichemke taratibu ili nyanya iive

baada ya dakika 5 funua nyanya itakua imelainika

weka mchanganyiko wa pili pili hoho na bilinganya pamoja na dagaa walioosha safi kabisa kwa maji

badaa ya hapo koroga vizuri mchanganyiko wote uchanganyike safi kabisa

kisha weka kitunguu swaumu hicho ni kifaa maalumu cha kuponde kitunguu kinauzwa madukani

Kisha weka binzali ya kopo iliyochanganywa na tui la nazi kama huna basi kuna nazi weka tui kuongeza ladha sio lazima

Nazi kawaida huwa ina mafuta lakini mafuta haya ni salama kwa mlaji ikiwa huli mara kwa mara pia yanasaidia kukaanga mchuzi wako uwe safi na mboga zilainike vizuri



HAYA NDIO MAPISHI YA DAGAA WA KIGOMAKUCHANGANYA PILI PILI HOHO NA BILINGANYA WAPIKIE FAMILIA YAKO WAFURAHIE CHAKLA HIKI UNAWEZA KULA NA MAHARAGE NA WALI AU UNAWEZA KULA NA UGALI KAMA WENGI TULIVYOZOWE NYUMBANI NA INAPENDEZA SANA SANA