CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Tuesday, December 29, 2009

CHEF ISSA PIA ANAPENDA SANA SOKASiku ya graduation Timu ya culinary aka machef tulikabidhiwa kombe la ushindi upande wa soka na mmatumbi nilipiga goli mbili safi na kuisaidia timu yangu kunyakua ubingwa mashindano yalikua ni ya pale shuleni tu kila idara walikua na timu yao. Baadhi ya wachezaji wa timu ya Culinary kabla ya mechi wengine walikua wanapasha misuli
Chef Issa Akishangilia baada ya kufunga goli dhidi ya timu ya Uongozi wa hotel na matukio

Namshukuru mungu ilikua ni good time si mchezo maana kila baada ya tukio kinachofata ni misosi ya nguvu hapa ilikua BBQ night baada ya Sport day kumalizika spring mpaka summer jua huwa linazama saa 3 usikuHii ilikua kona ya salad na cheese kibao pamoja na nyama kavuHii ilikua kona ya vyakula vya mboga mbogaNa hapa haswa ndio ilikua ni BBQ yenyewe unachagua unachokitaka mpishi anarushia kwenye moto haraka naona wengi walipendelea kula mbavu za kondoo au sausage au hamburger steak na salad.
6 comments:

Anonymous said...

Kaka kumbe na soka unatandika hahahahaha duh inapendeza sana

Anonymous said...

nimeona hilo BBQ mhhh full kujiramba

Anonymous said...

usisahau recipe zetu za chapati na makongoro hahahahahahaaaaa

Anonymous said...

very professional mpaka raha unapangilia na kinapangika na kinaeleweka na kinalika na kinatamanisha big up chef mzalendo kweli ni culinary chember nakuunga kwa mikono na miguu yote minne Mdau USA

Anonymous said...

chapait chapati chapati kweli kabisa wengine tukikaanga badala itoke kurasa inakuwa kama mtu unatafuna ngozi kama una mgeni ni aibu tunaomba hili pishi usichelewe kuliweka kwa kweli

Anonymous said...

Sasa,hizo hapo mwisho nahisi ndio hamburger steaks,sasa kama mimi niko uswahilini naziweka juu ya jiko la mkaa au?Na je hapa DSM naweza kuzipata wapi au ni lazima nitengeneze?kwa kweli hii blog itatusaidia wapenzi wa mamabo haya.
KT