CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Thursday, December 31, 2009

KARIBUNI SANA KATIKA LIBENEKE LA CHAKULA

Ndugu zangu namshuku sana mwenyezi mungu kwakuniwezesha kumaliza masomo yangu salama Pia natoashukurani zangu za dhati kwa Familia yangu yooote kwa sapot yenu kubwa.

Mimi chef Issa nimeamua kuanzisha libeneke la fani ya chakula ambapo wale wote wenye taaluma hii na wapenda chakula cha aina yeyote watapata fursa ya kujifunza kutoa maoni na kufundisha pia mapishi ya aina mbali mbali tutakaribisha recipe mbalimbali toka kwa yeyote atakaye penda kuchangia mawazo lengo nikubadilishana ujuzi ili kila mmoja wetu afaidike na utaalamu wa mapishi ya ladha zote, mchango wowote ule utaheshimiwa sana.

Tutakua na historia ya vyakula toka mataifa ya ulaya magharibi ambayo ni maarufu kwa vyakula vyao toka enzi hizo vikipikwa kwamtindo wa zamani tuliouzoea na pia vikibadilishwa kwamtindo mpya wa kisasa vikibaki na majina yaleyale hubadilika kwa kunakishiwa kwa mitindo mbalimbali pia tutapata wasaha wakujua historia ya vyakula na utambulisho kinatoka nchi gani na hasa tutagusa mataifa mama kwa nchi za magharibi katika sanaa hii ya chakula ikiwa ni Spain, England, France, German, Austria, Switzerland na Italy pia tutaangalia utaalamu sifa na aina za cheese, utundu wa kutengeneza na kunakshi chocolate na historia yote kwaujumla pia tutapata nasaha ya kuona vifaa mbalimbali na kujifunza kuchonga matunda na mboga ktk maumbile tofauti mfano tunda kama apple unatengeneza bata mzinga inapendeza sana.

Hakika ushirikiano wenu ndugu zangu utaifanya blog hii iwe chuo bora cha kubadilishana utaalamu wa fani hii ya chakula. Kwasasa nakaribisha maoni yenu tuanze na nini baada ya maelezo yote hapo juu ili blog hii iboreshwe zaidi na kila mmoja wetu afaidi? Pia nashughulikia uwezekano wa kufundisha kwa njia ya video hapa hapa katika blog yetu wanajamvini na ma chef wenzangu wazalendo karibuni sana sana sana. Nawatakia kheri ya mwaka mpya 2010 cheers!!

3 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Ni faraja kuona wenye fani wanaamua kuikuza na kutusaidia wengine kwa njia hii.
Karibu saaaaana kwenye ulimwengu wa ku-blog na kwa pamoja tutaweza.
Blessings

Anonymous said...

tunashukuru sana kwa ujio wa blog hii, mi ni mpenzi wa mapishi na napenda sana kupika nachokuomba uwe unatuandikia kwa kiswahili haswa kwenye mahitaji,
na kama hicho kitu kwa TZ hatutaweza kukipata labda tunaweza kutumia nini badala yake (mf. sprout)

Kijo

Alex Nkondola said...

Yes ni kweli bado una changamoto kubwa ni bora kuonyesha picha ya kitu maana kama vingine huku TZ ni aghalabu kukipata tafuta mbadala wake. Chef Alex.