CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Sunday, May 23, 2010

JUISI YA TUNDA PASSION


UNAWEZA TUMIA TUNDA LOLOTE KATI YA HAYA MAWILI JINA NI MOJA LAKINI YANATOFAUTINA LADHA MOJA NI TAMU NA MOJA NI CHAHU PIA UNAWEZA CHANGANYA YOTE MAWILI NA UKAPATALADHA SAFI SANA YA JUISI YAKO
Huu ndio muonekano wa passion tunda ya ganda la zambarau ambayo huwa ni tamu sanaNa hii ndio picha ya passion tunda ya ganda la njano ambalo huwa ni chachu kiasi


MAHITAJI
4 sukari vijiko vikubwa vya chakula 
3 passion tunda makubwa
1 lita ya maji baridi 
1 juisi ya limao

 JINSI YA KUANDAA
Kwanza kata tunda lako la passion nusu kisha toa juisi na mbegu zake zote zilizopo ndani wka katika bakuli.

Kisha chukua sukarina maji pamoja na mbegu na juisi weka katika blenda saga kwa muda wa dakika 1.5 mpaka 2 zima blenda ili mbegu zisi pondeke na kuaribu sura ya juisi yako.

kisha toa tumia chujio chuja juisi yako na weka katika bakuli au chombo chochote safi onja sukari kama inatoshakisha ongezea juisi ya limao na weka katika friji ipoe tayari kwa kunywewa.

 unaweza ongeza vipande vya barafu (ice cubes) kwajua la miezi hii wakati wa mchana utafurahia kinywaji chako baridi na safi 
baada ya chakula familia itafurahia kwa kuburudika na kinywaji hiki safi na baridi kwa afya
5 comments:

Flora said...

Hi Chef. Asante kwa kujibu swali langu.

shamim a.k.a Zeze said...

he bora umerudi nilikumiss

bora umeanza na juice...mie napenda saana passion iyo ya juu huwa ni tamu na ina harufu nzuri...naweza inywa hata yenyewe bila kumix

tatizo hii ya pili nikiinywa kata kama ikiwa imemixiwa na embe au na chochote naskia kiungulia saaana.

JE KUNA KITU NAWEZA MIX ILI NISIHISI KIUNGULIA

Mama Iqra

Anonymous said...

Zeze changanya na papai kwani papai huwa linasaidia kumaliza kiungulia. Hata kama umekula maharage kitaisha. @ Nagira

Anonymous said...

zeze u may changanya na parachichi na chungwa walau moja inakata kiungulia kabisa
pam

Anonymous said...

NAKUSHUKURU SANA ISSA, MUNGU AKUBARIKI SANA KWA ELIMU HII, NILIKUWA SIJUI MAPISHI MENGI NIMEANZA KUJIFUNZA KWA KUTUMIA HII BLOG YAKO.