CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Monday, May 17, 2010

JUISI YA AVOCADO AU PARACHICHI
JUISI HII YA PARACHICHI INA VIRUTUBISHO VINGI SANA KATIKA MWILI NI TIBA KWA AFYA YA MLAJI TENGENA KWAJILI YA FYA YA FAMILIA YAKOKata parachichi nusu kama inavyoonekana katika pichaKisha toambegu ya kati kati chukua kijiko toa nyama ya ndani weka katika blenda kwajili ya kusaga pamoja na matunda mengine

Mahitaji

1 parachichi lililoiva
2  ndimu safi zenye maji ya kutosha
50 gram maji safi ya baridi
2 vipande viwili vya papai la kuiva
3 sukari kijiko kikubwa cha chakula
2 asali kijiko kikubwa ca chakula
5 gram chumvi

Kwa ladhazaidi unaweza ngezea jani la fresh mint sio lazima 

Jinsi ya kuandaa:

WEka katika blenda parachichi, vipande vya papai, jani la mint kisha anza kusaga wakati unasaga unaongezea maji kiasi ili mchanganyiko usiwe mzito sana ukashindwa kuchanganyika . Mwisho kabisa ongezea asali, chumvi, limao na sukari kisha blend vizuri upate mchanganikio safi na wenye ladha safi.

Kisha weka katika friji ipoe nakushauri juisi hii kunywa muda wa mchana wakati huu mwili unakua umejiandaa kupekea virutubisho vilivyopotea. Safi sana kwa mtu mzima na mtoto pia ni nzuri sana kwa wale wanaozingatia mlo safi ili wasiongezeke uzito.  


MPATIE MWANAO AU MUMEO GLASI MOJA ANGALAU KILA BAADA YA SIKU 2 JUISI HII INA LADHAYA KIPEKEE6 comments:

ruky said...

Asante chef. kwema lakini? maana ulikuwa kimya kidogo.

Anonymous said...

mmmh! itakuwa tamu sana let me go & try

hellen

Bennet said...

Nisipoweka sukari si takuwa poa tu

Disminder orig baby said...

kaka upo?
asante sana kwa juice nzuri kama hizi. nyumba zetu zina furaha kubwa sana kwa matunda ya mafunzo yako. Mungu akuzidishie.

Flora said...

Hi Chef,nilikua na swali nje ya topic hii. Nauliza juice ya passion inatengenezwaje? Ukizingatia tunda lenyewe lina mbegu nyingi unazichambua kwanza ama unablend na mbegu zake tu na hazina tatizo? Naomba jibu tafadhali.

Anonymous said...

asante kaka kwa huduma yako