KAA TAYARI KWA RECIPE HII SAFI SANA YA KEKI ILIYO NA MCHANGANYIKO WA MABOGA
MAHITAJI
240 gram siagi
240 grama sukariya kahawia
30 gram sukari ya chenga
480 gram unga wa ngano
2 Kijiko kidogo cha chai baking powder
1 Kijiko kidogo cha chai bicabonate of soda
1 Kijiko kidogo cha chai unga wa mdarasini
1 Kijiko kidogo cha chai unag wa tangawizi
1/2 Kijiko kidogo cha chai unga wa kungu manga (nutmeg)
1/3 Kijiko kidogo cha chai unga wa karafuu
1/2 Kijiko kidogo cha chaichumvi
1/4 Kijiko kidogo cha chai unga wa pili pili manga (black pepper)
2 ute mweupe wa mayai, piaga na mchapo iwe laini
120 gram maziwa ya maji changanya na 1 Kijiko kidogo cha chai vanilla essence.
KWAJILI TA KUTENGENEZEA FROSTING
3 Kijiko kikubwa cha chakula siagi iyeyushe katika joto la chumba sio kweye moto
360 gram sukari ya unga
1/2 Kijiko kidogo cha chai vanilla
1 Kijiko kidogo cha chai chenga chenga za ganda la limao (lemon zest)
1/4 Kijiko kidogo cha chai juisi ya limao
JINSI YA KUANDAA FATILIA MAELEZO KATIKA PICHA KWA CHINI
Washa oven katika moto wa 350F (175 C). Kisha katika bakuli, piga kwa kutumia mchapo au mashine siagi pamoja na sukari kwa dakika 5.
Weka katika bakuli nyingine safi na kavu unga wa ngano, baking powder, baking soda, mdalasini, tangawizi, kungu manga, karafuu, chumvi, na pili pili manga.
Kisha weka ute mweupe wa mayai ndani ya mchanganyiko wa sukari na siagi changanya mpaka ichanganyike safi kabisa.
Kisha ongezea unga pole pole wakati huo huo unaongeza mchanganyiko siagi na mayai pamoja ule mchanganyiko wa maziwa na vanilla.
Kumbuka wakati unachanganya unga wa ngano ndio uwe wa mwisho kabisa endelea kuweka pole pole mpaka upate mchanganyiko safi kabisa mzito usiweke unga wote kwa mara moja.
Kisha weka uji mzito wa maboga yaliyochemshwa yakapondwa pondwa nadni ya mchanganyiko wako wa keki.
Changanya pole pole mpaka mchanganyiko wote uchanganyike safi kabisa na kua rangi moja.
Kisha weka karatasi maalumu kwajili ya kuokea keki zako, kama hauna basi kumbuka kupaka mafuta mashimo hayo ya kuokea keki ili isiungulie. Pia jitaidi kuweka robo tatu ya shimo usijaze mpaka juu kabisa maana zikiwa zinaiwa huwa zinapanda na kujaa.
baada ya kujaza acha ikae nje katika hewa kwa dakika 2 tu ili kutoa mapuvu na kuruhusu mchanganyiko wako ukae sawa.
Chona keki zako mpaka ukichoma na kijiti katikati kitoke kisafi kabisa, kwamuda wa dakika 20 hadi 25. Kisha toa keki zako na zipoze juu ya waya.
JINSI YA KUANDAA FROSTING
,
Changanya zest ya limao na siagi katika bakuli kisha piga na mchapo au mashine
Polepole mimina sukari ya unga na endelea kuchapa na mchapo au mashine mpaka iwe laini. Kisha ongeza vanilla na juisi ya limao.
Baada ya hapo paka frosting juu ya keki yako kuongeza ladha safi sana. Hii sio lazima unaweza weka au usiweke.Ubora wa keki yako ni supa hasa maana ndani ni sponji, laini na tamu kama unavyoona katika picha ilivyoiva safi kabisa.
HUU NI MUONEKANO HALISI WA KEKI YAKO BAADA YA KUIVA NA KUPAMBWA NA FROSTING SAFI SANA KWA LADHA BORA NA MLAJI ATAFURAHIA SANA UNAWEZA KULA KWA CHAI MUDA WOWOTE ULE.
1 comment:
Kaka Issa asante kwa maelekezo ya mapishi mazuri.Ni maelekezo rahisi sana hata kwa mimi nisiependa kupika. Ombi langu leo ni kama utaweza kutuwekea mapishi ya maandazi? Nitakushukuru sana kaka maana ni miaka mingi tokea nimekula maandazi, huku tulipo hivyo vitu ni adimu sana. Mimi si mpishi mzuri lakini nipo tayari kujaribisha maandazi kama utanisaidia. Kingine, je unaweza kuboresha site kwa kutuwekea option ya ku-type mapishi ili kuyaona badaya ya kutafuta kwa kuangalia tarehe? sijaona option ya kutype na ndio maana nauliza, samahani sana kama nitakuwa nimekukwaza na hili swali langu.
Post a Comment